CHADEMA na sera ya majimbo/kanda na mpango wa uendelezaji wake - ushauri

CHADEMA na sera ya majimbo/kanda na mpango wa uendelezaji wake - ushauri

moto2012

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
2,309
Reaction score
1,552
Wapendwa wana Jf,

Napenda kumshukuru Mungu kufikia mwishoni mwa mwaka salama, na ninazidi kumwomba atuvushe hadi mwakani salama salmini.

Awali ya yote ninapenda kuweka wazi mimi si mfuasi na sina kadi ya chama chochote cha siasa, ila nimekuwa nikifuatilia masuala mbali mbali ya kiuchumi na kisiasa na pia sera ya vyama vyetu vya siasa vilivyopo hapa nchini.

Nimevutiwa sana na sera ya CHADEMA (mimi sio mwanachama au mfuasi wa hiki chama)ya majimbo, kwangu mimi hili lingekuwa suluhu kwa yale maeneo yaliyoachwa nyuma kimaendeleo wakati maeneo hayo yana utajiri mkubwa wa rasilimali watu na mali asili, mfano Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara), nyanda za juu kusini (Ruvuma, Njombe, Iringa na Mbeya), Kanda ya magharibi (kigoma, Tabora na Kagera), Pia naomba niweke wazi kuwa ninatokea katika moja ya mikoa iliyosahaulika ilihali rasilimali zipo.

Kuna watu wanajitahidi sana kuielezea sera ya majimbo katika mtazamo hasi, lakini hata hayo matatizo ambayo wao wandhani yatachochewa kiuhalisia hata sasa yapo, ila watu hatujishughulishi kuangalia kwa undani, udugu, ukabila, udini nk ni vigezo vya mtu kuteuliwa kushika wadhifa fulani. Weledi wa kutatua matatizo ya jamii sio kigezo kwa sasa.

Faida za sera ya Majimbo ni nyingi sana, ila sitaeleza hapa, naamini wengi walishaeleza, ila kadiri mjadala utavyokuwa unaendelea nikihitajika nitaeleza.

Leo napenda nijikite zaidi katika mpango wa uendelezaji (Succession plan), ili sera hii iweze kufanikwa nashauri mambo yafuatayo yafanyike

  1. Uundwaji wa Bodi za wadhamini za majimbo-nashauri iundwe bodi ya wadhamini kwa kila jimbo, bodi hiyo na jukumu la kufanya utafiti wa vijana au watu ambao watakuja kuwa voingozi na tunu ya jimbo katika kipindi kitakacho pangwa. Bodi iundwe na watu au vijana wenye haiba katika chama. Bodi itakuwa kama kitalu cha kuzalisha viongozi wa kitaifa. (Kwa mfano kama John Mnyika na Saidi Arfi wakawa wajumbe wa bodi ya udhamini ya kanda ya kusini, Tundulisu & Msigwa Nyanda za juu kusini, Zitto Kanda ya kati nk) watapewa time frame let say ya miaka miwili wafungue tawi la CHADEMA kila kata, na katika kipindi hicho waandae viongozi ambao watachukua nafasi za uongozi wa kanda. Baada ya huo muda ifanyike tathmini kama lengo limefikiwa au la, na hiyo iwe kigezo cha kuwapendekeza Bw. Mnyika na Arfi na wengine kugombea ngazi za juu za kitaifa za uongozi wa chama kama Uenyekiti wa taifa, Ukatibu mkuu, ukatibu uenezi na hata Urais muda ukifika. Bodi ya Kanda italazimika kuleta taarifa za mendeleo ya kanda angalau mara mbili kwa mwaka katika kamati kuu
  2. Uandaaji wa makada wa chama wa kanda-Utafiti ufanyike kuanzia ngazi ya shule za sekondari, vyou vya elimu ya juu, kwa lengo la kuwatambua vijana (thorughly screening kuepuka mamluki) wale ambao wanaweza wakawa makada wa chama katika kanda husika, hao chama kiwasaidie kuwaendeleza na kuwasidia kupata mikopo itakayogharimia masomo yao na kisha wapelekwe kufanya kazi katika kanda zao, hata kama sio moja kwa moja ila watashiriki kufanya kazi za chama. Utafiti ufanyike katika vyuo vyote nchini.
  3. Kufanya utafiti wa juu ya rasilimali watu na maliasili zilizopo kila jimbo/kanda-hii itakiwezesha chama kuwatambua watu wenye ushawishi katika kanda hizo hata kama wanaishi na kufanya kazi katika kanda nyingine. Chama kifanye juhudi kuwashawishi waweze kushiriki katika uimarishaji wa chama katika kanda zao za asili kwa hali na mali. Pia utafiti wa rasilimali nyingine itaiwezesha jamii husika kutambua nafasi ya hizo rasilimali zao katika kuwaletea maendeleo na hivyo kujenga utayari wa kuzilinda
Naomba Kuwasilisha

CC BenSaanane YerikoNyerere watu8 @GodlistenMalisa
 
kusema kweli hii Sera ya majimbo ni nzuri kama itaratibiwa vizuri.Nchi yetu ina raslimali kila mahali ambazo zinaweza kuendeleza maeneo ya kanda husika katika viwanda na kuongeza ajira kwa Vijana kuimarisha elimu na ustawi Wa jamii.inaweza kuamuliwa70% ya raslimali zitumike katika majimbo ns30% zitumuke kuendesha serial I kuu DSM.Majimbo yawe na mamlaka kamili ya kuendesha zerkali zake.Kwamba italeta ukabila udini nk ni kasumba zilizopitwa na wakati Tanzania ya Leo sio Ya baada ya Uhuru.Haya yakifanywa; nani atakuja Dar? Dar sasa zitakuwa kwenye majimbo
 
Kwangu Sera ya majimbo naamini zitakuwa chachu ya kuamsha uzalendo
 
Back
Top Bottom