Chadema na kisa cha Mbuni!!!

Chadema na kisa cha Mbuni!!!

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
chama cha demokrasia na maendeleo chadema kinanikumbusha kisa kimoja cha mbuni na simba jangwani, ambapo mbuni akikimbizwa na simba kuamua kuchomeka kichwa chini ya mchanga kisha kujipa moyo kuwa mambo yameisha. kilichofatia ni simba kujipatia chakula kwa urahisi kwani body yote ilikua nje. nimesema hiyo stori kwani inafanana sana na mgogoro wa chadema.

Kuna watu wanaamini kuwa kuondolewa kwa wale wanoitwa kama wasailiti wa chama, basi chama kiko salama hapo itakuwa tunajidanganya wenyewe.ni uhakika kuwa kuna watu na wanachama ambao bado wapo chadema nchi nzima ambao kimsingi wana sympathize na wale ambao chama inawaona ni wasaliti na kuwaondoa hivo kwakuwa sasa wanaandamwa wanaweza kukaa kimya na baadae kufanya consipiracy within again.ni busara kama chama kikajitifakari kwanini chama kinapita kwenye changamoto hizi ni busara haya yakaangaliwa na yasipuuzwe, kwani tukiwa na upinzani imara regardless wamechukua nchi au la ni jambo muhimu na kwa mustakabali kwa taifa letu

1.je kuna ukweli wowote kuhusu waasisi kuingilia au kushinikiza baadhi ya mambo. chama na wapenzi wa chadema wanaweza wakapuuza suala hili lakini limetajwa maranyingi kwenye media na mitandao ya kijamii kwmb kuna wakati waasisi wanaingilia baadhi ya maamuzi ya chama. bila shaka kuna haja kama chama kuliangalia hili kama linaukweli kiasi gani badala ya kudharau kila changamoto inayoletwa na watu wenye muono tofauti

2.suala la matumizi na mapato kuwa wazi na kuonekana kutoka makao makuu hadi ngaz ya chini. kuna malalamiko mengi ambayo yapo kwenye media kwamba ngazi za chini za chama kuna ukata na aslimia kubwa ya mapato inatumika makao makuu ya chama. yapo malalamiko ya viongzi wa chini kwamba wanajitolea sana ila kama chama hakijafanya vya kutosha kuwakwamua kimaslahi. hawa viongozi wa chini ndio bomu kwa chama kwani mtu aweza kuwanunua kwa kuwa wako dhoofu li hali. kama chama wajitafakari juu ya mapato na matumizi ya chama kwani kuna malalamiko mengi juu suala la fedha ila kama mtadharau basi lakini lisemwalo lipo kama halipo laja.

3.udhaifu wa viongozi wa chama kuanzia ngazi za juu mpaka ngazi za mikoa. uongozi umekuwa unashindwa kusimamia suala la nidhamu ndani ya chama. viongozi wa ngazi za chini wanaweza kuwatukana na kuwachafua viongzi wa juu kuwa ni wasaliti wanafiki hata kama ni kweli ama si kweli kwa tuhuma husika huo si utaratibu mzuri. nidhamu ni mhimu mno kwa mustakabali kwa chama chochote. mbunge au mwanachama kumchafua kiongzi wake hadharani kwenye mitandao hata kama madai yake ni kweli si utaratibu. jeshi lolote ambalo halina nidhamu ni rahisi sana kushindwa vita hata kam lina wanajeshi wakakamavu na ujuzi mkubwa.

4.kuruhusu uhuru wa maoni kwa ngazi zote bila kushinikiza kwmb kwa maoni yako hayo wewe utakuwa msaliti wa chama au unasupport wasaliti. ni bora kusikiliza kila hoja na kujibu hoja kwa nguvu ya hoja na si kwa hoja ya nguvu.

Note:- Tanzania bila upinzani imara ni hatari kwa mustakabali wa taifa,lakini maslahi binafsi ya viongozi wa upinzani walionayo hivi sasa ni hatari zaidi kuliko sera za watawala
 
hoja zako nzuri lakini mwe! uneshindwa hata kuigawa stori yako kwenye aya mbalimbali?
 
Mkuu, edit kazi yako ili iwe na muonekano mzuri. Otherwise kazi nzuri
 
wazo zuri! Ila all we are not sure kma wanatafakar kuhusiana na uliyoyasema na kwa viongoz waliopo CDM naamin ni watu wenye uwezo wa kutafakar na kuamua kwa usahihi
 
Back
Top Bottom