chadema na imani ya umma wa watanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

chadema na imani ya umma wa watanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by asakuta same, Mar 5, 2011.

 1. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  hapo jana trh 4/3/2011 chadema wamehitimisha awamu ya kwanza ya ziara yao ya ukombozi kanda ya ziwa.watanzania tumeshuhudia uungwaji mkono mkubwa kwa chadema kutoka kwa wananchi kiasi kwamba ccm ,mafisadi na vibaraka wao wamebaki kutapatapa.hii yote imetokana na watanzania kuchoka na utawala wa ccm na kujenga imani kubwa kwa cdm.
  kimsingi imani ya umma wa tanzania kwa chadema haikuanza leo ,ilikuwepo toka ilipoonyesha uwezo wa kuwa na safu ya viongozi wenye uzalendo mkubwa ,uwezo mkubwa wa kujenga hoja zenye maslahi kwa umma ,kutoa fursa ya kiuongozi kwa vijana na zaidi ya yote kuwa na wabunge imara wakiongozwa na slaa kwenye bunge la tisa waliokuwa na uwezo usiotia shaka hata kidogo wa kusimamia maslahi ya watanzania ndani na nje ya bunge.
  lakini pia ni ukweli usiopingika kwenye uchaguzi kumsimamisha mgombea urais(slaa)mwenye sifa zilizotukuka kwamfano kwa uchache wake ni mzalendo ,mpiga vita ufisadi ,mwadilifu ,uwezo wa kuthubutu ,jasiri ,mkweli ,muwazi ,ufahamu wa mambo mengi ,makini ,msomi n.k na zaidi kunadi ilani ya uchaguzi iliyojenga matumaini kwa watanzania waliowengi kulizidisha uhalali wa cdm kuwa tumaini jipya la watanzania ,mkombozi wa ukweli na suluhisho pekee la matatizo yao.
  kwa niliyoyaeleza hapo juu napenda kutoa angalizo kwa cdm ,kwa kuwa upepo huu wa mabadiliko utawabeba wote wakiwemo wasiohusika ni muda muafaka kwa cdm kuja na
  1.ITIKADI YA CHAMA.
  2.KATIBA YA CHAMA ITAKAYOENDANA NA HAYA MABADILIKO.
  3.DIRA YA CHAMA.
  4.KUTEKELEZA KWA VITENDO CHADEMA NI MSINGI.
  5.MPANGO MKAKATI WA KUIMARISHA CHAMA MPAKA NGAZI YA CHINI KABISA.
  haya ni muhimu kwasababu siku zijazo wanapoelekea kushika hatamu kutahitajika timu kubwa ya watendaji mpaka ngazi ya chini kabisa karibu na wananchi kuwasaidiA kina DR. slaa kutimiza kile watanzania wanachokitarajia kutoka kwa cdm na kimsingi hawa watendaji ni lazima waandaliwe kwa msingi niliyoitaja hapo juu ili kupata watu waadilifu ,wazalendo ,wenye dhamira ya kweli ya kutatu matatizo ya watanzania n.k.
  naomba kuwasilisha.
   
 2. K

  KrnjeFzil Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lengo la CDM lipo upande wa pili wa shiling,Usitake danganya watu.
   
 3. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  hebu nijuze mjuzi wewe au usikute ndiyo umejisikia tu kutema pumba.
   
 4. M

  Mtaalaamuna Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaonekana wewe ni kipofu na kiziwi kwani huoni na husikii au una masikio hutaki kusikia na macho hutaki kutazama na kuona mwelekeo.

  Nakupa Bg Up asakuta maana hilo ndilo lililobaki Baada ya Op Sangara ni kuingia hadi uvunguni """"WA TA JI JU"""" wasiotaka
   
 5. wasaimon

  wasaimon R I P

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa kuwafahamisha watanzania habari hizo nzuri.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ni PM hlo lengo
   
 7. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  <br />
  <br />
  Hata wenzio wanandoto kama zako za kujiandaa kushika dola. Acha kujifariji na kutoa sifa za kiroho za mtu hali ya kuwa mwenye uwezo wa kutambua baadhi ya sifa hizo ni Mungu pekee.Kupumbazwa kwenu na maandamano ya watu wachache kwa maana watanzania tupo zaidi ya mil 40 mkadhani ikulu inaingilika kirahisi na huyo mzee ambae mpaka leo anamchumba huku akizini nae (hana maadili na haeshimu amri ya sita ya kutokuzini) ambayo Mungu kaiweka.
   
 8. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  punguza chuki ndugu ili ujijengee uwezo wa kupunguza hoja zako za maji taka..............na may be allah amekuandalia makazi mema peponi kwa kutokuwa na dhambi mtakatifu wewe unayehubiri injili.
   
Loading...