CHADEMA na CUF vikifa CCM itashindana na nani?

CHADEMA na CUF vikifa CCM itashindana na nani?

lendila

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
5,805
Reaction score
4,374
Hivi vyama vya CHADEMA na CUF vikifa CCM watashindana na nani?
Simba ikifa Yanga itacheza na nani?

Kama watanzania lazima tukubali ushindani wa kisiasa kwa moyo mkunjufu, lazima tufanye siasa za ushindani ni tamaduni wetu, kizazi na kizazi, tusiruhusu mtu atakayeuwa timu ya Simba Yanga ibaki yenyewe, tusiruhusu watu waue ushindani wa kisiasa ulioasisiwa na baba wa taifa hili, tena baba ambaye kila mwaka tunamwadhimisha kwa mazuri yake na moja ya mazuri yake ni kuasisi mfumo wa vyama vyingi vya siasa nchini kwetu Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona mpinzani wako anatafuta njia ya kukuua ujue tayari umemshinda.
Anaogopa aibu na fedhea.
 
Na chama kipya kinaitwa ukosefu wa ajira.
 
Unaweza kufikiri ni utani lkn ni kweli ni mambo yanayotekea nchini kwetu,badala serekali itumie nguvu kubwa kuleta maendeleo,serekali inawaza namna ya kuuwa vyama shindani kwa mbinu haramu,kwanini wasibadilishe sheria,na katiba tubaki na chama kimoja?kuliko kutumia mbinu haramu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vimeshakufa kwa asilimia nyingi tu.
Mpaka dakika hii sijajua nani anaweza kugombea urais kupitia Chadema wala CUF.

CCM imejitahidi kuviua hivi vyama viwili kwa kupitia viongozi wake wenye njaa na tamaa ya fedha, kiukweli CCM imefanikiwa katika hili.

Angalia trend utaelewa
1. Madiwani wa Chadema wananunuliwa.

2.Spika wa bunge anaridhia harakaharaka wabunge wa Chadema kufukuzwa.

3. Ofisi ya msajili wa vyama kumkingia kifua mtu wao (Lipumba) ilihali alishaandika barua ya kujiuzuru.

4. Viongozi wa ngazi za juu ACT kuteuliwa nafasi za serikali ya CCM.

5. Zitto Kabwe kuanza kuipongeza CCM juzi juzi, kazi ya mpinzani sio kupongeza serikali, kazi ya mpinzani ni kutafuta madhaifu ya serikali na kukosoa mwanzo mwisho.

Vyama pinzani vinazidi kua hovyo zaidi unaweza kusema CCM inaanza kua bora kuliko Chadema na CUF ya Profesa njaa.

nothing is easier than blaming others for your own problems
 
Hivi vyama vya CHADEMA na CUF vikifa CCM watashindana na nani?
Simba ikifa Yanga itacheza na nani?

Kama watanzania lazima tukubali ushindani wa kisiasa kwa moyo mkunjufu, lazima tufanye siasa za ushindani ni tamaduni wetu, kizazi na kizazi, tusiruhusu mtu atakayeuwa timu ya Simba Yanga ibaki yenyewe, tusiruhusu watu waue ushindani wa kisiasa ulioasisiwa na baba wa taifa hili, tena baba ambaye kila mwaka tunamwadhimisha kwa mazuri yake na moja ya mazuri yake ni kuasisi mfumo wa vyama vyingi vya siasa nchini kwetu Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app

Watashindana na ACT chama kisichokuwa na ushindani wa kweli
 
Back
Top Bottom