JamboJema
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 1,143
- 209
Kumekuwa na malumbano yasiyo na tija kati ya CCM na CHADEMA huko Muganza kiasi cha kuathiri kwa kiwango kikubwa mstakabali wa maendeleo ya wanamuganza. Ilikuwaje?.....Mwaka 2010 kabla ya uchaguzi mkuu WDC waliamua kujenga zahanati ya kijiji.
Wakati huo Diwani akiwa kutoka CCM. Mkakati wa ujenzi ukaanza na kuonekana kusimama kupisha uchaguzi. Baada ya uchaguzi, diwani wa CHADEMA akapatikana.....bahati mbaya[kama ndivyo ilivyo] wenyeviti wa vijiji wa Kata hii wote ni CCM. Mpango wa ujenzi wa zahanati 'ukagomewa' na waCCM hawa. Jitihada zote za diwani hazikuzaa matunda!
Mwaka jana, watoto waliomaliza darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika kata hii yenye shule moja tu ya sekondari - Zakia Megji, wanazidi idada ya madarasa yaliyopo. Watoto 138 wanakosa vyumba vya kusomea. Hakika ni kama vyuma vinne vinavyopungua. WDC ikaamua madarasa yajengwe. Siasa za CHADEMA zikapita kwa wananchi kuwa ni kwa nini wachangie madarasa hali zahanati haijajengwa. Wananchi wakagoma kuchanga!
Muziki ni kuwa, wenyeviti wa vijiji (CCM) wamekubali kuchangisha ili madarasa yajengwe; wananchi wanazuiwa na CHADEMA kuwa kwa nini watekeleze mradi wa pili wakati wa kwanza(zahanati) haujatekelezwa. Wananchi wengi wanaona CHADEMA wako sahihi na matokeo yake si zahanati wala madarasa vinavyojengwa!
Imegeuzwa kuwa zahanati ni sera ya CHADEMA na shule ni sera ya CCM. Hii ndio siasa tunayoijenga watanzania!