Chadema na ccm wakatana mapanga mkoani iringa


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,064
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,064 2,000
[h=3][/h]MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wilayani Kilolo, Lunyiliko Nyaulingo amelazwa katika Hospitali ya mkoa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mgololo amelazwa Hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wanaodaiwa ni wanachama wa CCM katika kampeni za mwisho za kuwania nafasi ya udiwani.


Sambamba na hiyo Katibu wa CCM kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo, Wilhad Ngogo (40) na Yohana Mchafu anayedaiwa kuwa ni mwanachama wa CCM wanashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na matukio hayo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema watu hao walikamatwa jana kufuatia
vurugu zilizojitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya mwisho katika wilaya hizo mbili.


Alisema kufuatia mzozo huo wanachama wa CHADEMA walizuia barabara ya Iringa-Mbeya kwa kuweka magogo ili kuzuia magari kupita na kuwa Polisi wanamtafuta Rabart Sam maarufu kwa jina la Kideri kwa kuongoza vurugu hizo.


Kamanda Mungi alisema wanafanya uchunguzi wa kina juu ya matukio hayo na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.


Aidha alitoa wito kwa viongozi wote wa vyama vya siasa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kutokea.


Leo Uchaguzi wa udiwani katika kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo na Mbalamaziwa wilayani Mufindi ulifanyika ambapo Zuberi Nyomolelo (CCM) na Ezekiel Mlyuka (CHADEME) walipambana kwa kata ya Mbalamaziwa na kwa upande wa Ng’ang’ange Kilolo Nafred Chahe (CHADEMA) na Namgalesi Msuva (CCM) walipambanachanzo. CHADEMA NA CCM WAKATANA MAPANGA MKOANI IRINGA - MPEKUZI HURU
 
Z

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Messages
3,846
Points
1,225
Z

zamlock

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2010
3,846 1,225
hv kwa nn ccm wanafanya haya mambo ya kijinga? Hv unajua chadema wakiwa wana jihami kwa kutembea na visu na bastola unajua itakuwa noma sana
 
DR. MWAKABANJE

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Messages
1,959
Points
2,000
DR. MWAKABANJE

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2012
1,959 2,000
Du 2015 kazi ipo!
 
M

Mwira Mwayo

Senior Member
Joined
Mar 23, 2013
Messages
142
Points
0
Age
38
M

Mwira Mwayo

Senior Member
Joined Mar 23, 2013
142 0
CCM ni wauwaji tukubali tu kwani hata huruma hawana kabisa. Lile jeshi wanalandalia huko Mbeya si litamaliza watanzania wakati wa uchaguzi mkuu? Mungu tuondolee hawa wadhalimu.
 
Nyanidume

Nyanidume

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
2,340
Points
2,000
Nyanidume

Nyanidume

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
2,340 2,000
Chinjanen, uwanen, mfe na mpotee kabisa katika uso wa dunia, kwan mna faida gan kwetu? haya mambo ya vyama ni mambo ya kijinga kabisa. Natamani jeshi lishike hatamu then lipige marufuku vyama vyote kuliko kuona ujinga unaendelea
 

Forum statistics

Threads 1,283,462
Members 493,707
Posts 30,790,444
Top