CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
Umetukana wakati unalalamika hakuna uhuru. Sidhani kama kuna mwanasiasa duniani atakupa nafasi kwa sababu unajua kumtukana!Presha ya nini na makala ndeeefuu ya kuhalalisha upumbavu wa serikali hovyo kabisa za mavi za Kiafrika?
Upo hapa kutetea miserikali ya kingedere za Kiafrika zinapofanya mambo ya chooni!?
Mnaotetea udhalimu sijui mmetokea wapi aisee!
Kama nyie ni miungu-monkeys endeleeni na uchaguzi wenu mkiwa wenyewe,yanini mnawafatafata opposition?
Fanyeni yenu,fungeni matako!
Umetukana wakati unalalamika hakuna uhuru. Sidhani kama kuna mwanasiasa duniani atakupa nafasi kwa sababu unajua kumtukana!
.Hivi kuna mantiki kususia uchaguzi wa local government lakini kushiriki bungeni? Bungeni mnajadili maendeleo ya wapi kama sio ya mitaa na vitongoji?
Japo kujitoa ni ujinga (kwa mujibu wa Aikaeli Mbowe). Mlipoamua kususa uchaguzi mngesusa na bunge ndio walau ingekuwa na mashiko. Nyie mnaagiza wa chini yenu kususa na kutoa ushirikiano kwa local government lakini nyie wa juu mnatoa ushirikiano kwa serikali kuu!
Tukisema mmejali posho za bunge tutakuwa tumekosea? Mnavyojadili bungeni vitaenda kutekelezwa wapi? Kenya? Mbinguni? Ubeljiji? Sio vitaenda kutekelezwa mitaani na vitongojini? Kwa hiyo mmeagiza wa chini yenu wasitekekeze hata mliyiafiki bungeni?
Hivi wanachama wenu watapata wapi leseni za biashara? Watapataje mikopo? Watakataa matibabu na elimu?
Lakini kubwa zaidi ni je mnayemsusia anaumia au ananufaika?
Uamuzi huu mtaujutia milele.
Mwaka huu kulikuwa na uchaguzi wa local government na ubunge (deputies) hapa Togo. Uchaguzi wa nafasi ya raisi ni 2020. Ni Kura ya raisi tu.
Muungano wa vyama (ukawa ya Togo) ukiongozwa na chama kikuu cha upinzani kinaitwa -ANC (wameiga ANC ya Madiba) vilichukua uamuzi kama wenu. Vyama "vidogo" walivyovidharau vikashiriki. Sasa ukawa ya Togo haina hata mjumbe wala mbunge wala diwani. Zero! Wakati wakisusa walijitapa mno! Tumewaachia! NI uchafuzi sio uchaguzi! Hatuwezi kushiriki dhuluma! Tambo kibao.
Vile vyama vidogo ndivyo sasa vina theluthi ya wabunge.
Sasa majuzi UKAWA imeandika barua France na EU kuomba eti uchaguzi urudiwe! Wamejibiwa kuwa uamuzi wa kurudia au kutorudiwa ni wa Serikali na raia wa Togo. Waombe kukutana na Serikali!
Sasa wameandika barua kuiomba Serikali iitishe kikao! Serikali imejifanya haina masikio[emoji38][emoji1][emoji3]
Siku zinaenda! Uchaguzi wa raisi unakuja mwakani. Sasa UKAWA hii imeanza kugombana! Baadhi wameandika barua ya kuomba radhi. Maana kwa mujibu wa hizi katiba za makoloni ya mfaransa ili ushiriki uchaguzi wa raisi lazima uwe umeshiriki uchaguzi wa "Deputies" aka WABUNGE
MBOMBO NGAFU! MCHAGA KANYIMWA HELA
Yumkini waomba radhi watasamehewa ila uchaguzi wa raisi katiba hairuhusu.
Ala Ala kina CHADEMA na ACT. Kabla ya kuchukua maamuzi sampuli hii muwe mnatafiti nchi nyingine ilikuwaje?
Sio leo mtu anadai ni ujinga na makosa kususa kesho anatangaza kususa.
Hiki kipengele cha sifa ya kushiriki uchaguzi mkuu mnaonaje tukikiiga? Yaani ukisusa uchaguzi wa Local Government unakosa sifa ya kushiriki uchaguzi wa Serikali Kuu?
Ingefaa?
Ndani ya demokrasia ukitoa mawazo ya kipumbavu utaambiwa mpumbavu waziwazi bila kupindisha maneno! Unachotakiwa kufanya ni kutoa mawazo yako bila bila kukejeli au kukandia mawazo au maamuzi ya wenzako!Matusi ndiyo demokrasia? Kutoheshimu mawazo ya wengine ndiyo Demokrasia? Tukisema na wewe ndo wale wale kasoro rangi tutakuwa tumekosea? Tofauti yako ni nini?