Juma wa Juma
Senior Member
- Jan 13, 2017
- 150
- 221
Makamanda wa Chadema wilaya ya Ilemela na Tanzania nzima, ndugu wananchi na viongozi wa ngazi zote,
Kuna taarifa inasambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwa viongozi Chadema wilaya ya Ilemela wote wamejiunga CCM Leo 2/3/2015.
Sababu yao kubwa ya kujiondoa kwenye chama eti ni kile kinachoitwa Wema Sepetu kujiunga na Chadema: MWANZA: Viongozi 15 wa CHADEMA wahamia CCM
Niutaarifu umma kwamba :
1. Hao wanaojiita viongozi wa Chama waliohamia CCM, ni waongo na wazandiki kwa si viongozi tena tangu walipoondolewa na operation ya chama kata funua miezi miwili iliyopita baada ya kugundulika kuwa ni wazembe na wabadhirifu wa fedha na Mali za chama.
Aidha, Damas Kimenyi alikuwa anadaiwa na chama kiasi cha sh. 4.5m ada ya wagombea ubunge kura za maoni ndani ya chama mwaka 2015 pamoja na pikipiki 2 Mali ya chama ambazo amejimilikisha kinyume na sheria za nchi.
2. Ni kundi hili la wahuni lilitusaliti wakati wa uchaguzi mkuu 2015, mpaka ikafikia wakati wanachama wakawakataa kwenye mkutano mkuu wa wilaya uliofanyika tarehe11/1/2017 mgeni rasmi alikuwa mh Freeman Mbowe.
Napenda kutumia muda huu kukutaarifuni kuwa chama Ilemela kiko imara sana na wanachama wasibabaishwe na hizo propaganda uchwara za hao wahuni wachache.
Grayson Wanzagi Warioba
Mwenyekiti Ilemela