CosaNostra
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 382
- 139
Kwa bahati nzuri tuko Tanzania ile ile ya 1995 ambayo Mrema alivuma sana na tukaamini atapata urais. Mrema hakuwa na kashfa yoyote ya ufisadi wakati ule, ila CCM waliweka kigezo cha elimu ya chuo kikuu ambayo Mrema hakuwa nayo. Watu kama Mrema (wa enzi zile) na Lowassa wa sasa wanasumbuliwa na kitu kimoja.
Nilweka uzi hapa mwezi May, wakati Lowassa yupo CCM,kuwa "KINACHOMSUMBUA LOWASSA NI HIKI" unaweza kurejea uzi huo.
Watu wa dizaini hii kamwe hawariziki kuwa chini ya mtu au mfumo fulani, Lowasa alikuwa anangojea tu muda wake ufike CCMimpe bendera kugombea urais. Amekosa huko na kuja CDM kwa lengo lilelile. Nachoamini ni kuwa kamwe CCM hawataiachia nchi kwa Lowasa - IWE IWEJE - HAWATAWEZA, bora Dr. Slaa wasingeweka nguvu kubwa na mbinu kumzuia.
Kwa hiyo nachosema Lowasa hatapata urais wa Tanzania.
then what?
Baada ya uchaguzi - naamini UKAWA watapata wabunge wengi sana, kitakachobaki kwa Lowasa na timu yake, wakwasi wa fedha - Rostam, Chenge, Karamagi, na wengineo watataka kuongoza chama ili kulitawala bunge. CHADEMA mnayoiona leo itatawaliwa na fedha, fedha za mafisadi.
Hapo ndipo mtakapotafuta namna ya kumwondoa msiweze kwa kuwa kundi lake litakuwa limeiteka CHADEMA na mtabaki na majuto.
Iko siku mtakumbuka thread hii. Nimesema!