Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,183
Akiongea mbele ya mamia ya wakazi wa Mtaa wa Liwiti katika Jimbo la Segerea, mwanasiana na mwanasheria mahiri nchini Mheshimiwa Mabere Marando amewaasa Watanzania kutokurudia tena makosa ya kukiweka madarakani Chama cha Mapinduzi kutokana na sera ya chama hicho ya kukumbatia rushwa na wala-rushwa.
Amewatahadharisha CCM kuwa mwaka huu hakuna nafasi ya kuiba na kuchakachua kura kwani Chadema na Ukawa wamejipanga barabara kukabiliana na aina yoyote ya hujuma kwa matokeo ya uchaguzi. Amesema CCM kimekuwa kichaka cha wezi ambapo watawala wamewekeza katika kula pesa za umma zaidi kuliko kufanya mambo ya maendeleo. Ameshutumu serikali ya CCM kwa kujitapa kujenga barabara wakati barabara zenyewe zina kile alichokiita 'expiry date' na hii inatokana na kutafunwa kwa pesa za ujenzi wa barabara na viongozi wa serikali ya sasa akitolea mfano linaweza kutolewa fungu la shilingi milioni 100 za ujenzi wa barabara lakini katika hizo milioni 70 zinatiwa mfukoni na maCCM na milioni 30 tu ndo zinapelekwa katika ujenzi wa barabara hali inayopelekea kujengwa barabara zinazochakaa baada ya muda mfupi tu.
Amewasilisha salamu za Mwenyekiti wa chama Mhe. Freeman Mbowe (MB) kwa Watanzania na hasa watumishi wa umma kuwa Ukawa haitaunda serikali ya visasi, bali kila mtumishi wa umma katika nafasi yake atahakikishiwa utendaji wa kazi wenye weledi na tija kwa taifa badala ya mfumo wa sasa ambapo watumishi wa umma wengi ni wala-rushwa. Ametahadharisha kuwa kwa watumishi wala-rushwa serikali ya Ukawa haitawafumbia macho kamwe.
Amewahakikishia Watanzania kuwa Chadema na ukawa wataomba kura kutoka kwao mpaka dakika ya mwisho kabla ya uchaguzi mwezi Oktoba.
Arcado Ntagazwa naye alikuwa na yake ya kusema akiwaita CCM kama 'nyoka wa kijani'. Amesema CCM ni wanafiki wakubwa kwani wamezinduwa kile wanachikiita sera ya elimu inayoahidi elimu bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu lakini akakumbusha kuwa ni maCCM hawahawa waliopinga sera ya elimu bure iliyokuwa katika ilani ya uchaguzi ya chadema mwaka 2010 na hiyo ndiyo sababu mzee ntagazwa akasema maCCM ni manafiki wakubwa. Amewaasha Watanzania wasikichaguwe tena CCM kwani hata hao wanaotangaza nia wengi wao si wasafi na hawana jipya.
Katibu wa Chadema Jimbo la Segerea amesema CCM Segerea ijiandae kisaikolojia kuondoka kwani Chadema na ukawa wako sawa uchaguzi huu. Amesema mwaka 2009 Chadema walikuwa na mwenyekiti mmoja tu lakini uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana kimepata zaidi ya wenyeviti 50. sasa kama uchaguzi wa mwaka 2010 chadema kilikuwa na mwenyekiti mmoja na kikapata kura 39,000 katika ubunge, je mwaka huu kikiwa na wenyeviti zaidi ya 50 unafikri kitapata kura ngapi? mambo ya cross multiplication hayo!
Chadema one love, Ikulu people's power, ubunge people's power, udiwani people's power!