Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,306
- 25,928
Kwanza nikiri kufurahishwa na CHADEMA kupokea ushauri wangu pamoja na wa wana-JF wengine juu ya Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki. Niliwashauri humu humu JF. Niliwashauri hivi: CHADEMA, pelekeni majina zaidi ya mawili Bungeni kumaliza utata EALA. Sasa mpo kwenye mchakato wa kupata majina ya nyongeza kwa ajili ya kuwasilisha tena Bungeni kwa upigaji wa kura. Ni jambo jema na ni hatua nzuri. Kwahilo, CHADEMA mnashaurika.
Sasa shaurikeni na jambo hili lenye pande mbili. Mosi, amueni kwa vitendo kujenga ofisi zenu (Ofisi Kuu na zile za kanda na kadhalika) zenye hadhi ya chama chenu. Endesheni hata harambee ya ujenzi wa ofisi zinazoakisi ukubwa, umaarufu na umuhimu wa chama chenu. Ofisi zenu za kwenye 'maflemu' zimepitwa na wakati. Ni wakati wa kuendana na hadhi yenu.
Pili, jiimarisheni katika ngazi za chini kuanzia shinani. Imarisheni chama chenu katika sehemu ambazo watu hawajui hata uwepo wa vyama vingi. Huko ndiko walipo wapiga kura. Huko ndiko wanakochaguliwa viongozi wanaojaza Bunge letu na kutuamulia mambo yetu. Huko ndiko wanakochaguliwa wanaojadili masuala ya kitaifa. Ngazi ya chini huamua muenekano wa ngazi za juu. Ndipo msingi hasa ulipo.