Uchaguzi 2020 CHADEMA mnaingia kwenye Uchaguzi kwa misingi ipi?

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Wasalaam,
Katika kumbukumbu zangu nimekutana na gazeti la Mawio liliochapishwa Alhamisi,Januari 1-2015

Ukurasa wa tano nimekutana na habari iliyonifanya niipitie tena kuisoma baada yakusoma nimejikuta naamasika kukumegea kidogo juu ya hali ilivyo na ubaguzi unaoendelea nchini.

Nimejiuliza wakati Watanzania mnakemea ubaguzi wa rangi Marekani.Je ubaguzi wa Marekani unatofauti gani na huu wa Ccm na wakosoaji wake Tanzania?

Je Ccm wana hati milki ya kudumu ya nchi hii?

"Na Mwandishi Maalumu
Wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera imo katika hatari ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.Vita hii inachochewa na viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),wilayani umo na mkoa.

Baada ya vilio vya muda mrefu vilivyofikia gazeti hili,niliondoka kwenda uko na kuweka kambi katika vijiji vya Lukuraijo,Katera,Kitwechenkura Kagenyi na mji mdogo wa Kaisho.

Wilaya hii iko mipakani mwa Uganda na Rwanda kiasi kwamba kwa mgeni wa eneo hili huwezi kutofautisha mhamiaji na mwenyeji.Hali hii ya utata wa uenyeji na ugeni imesababisha kila wakati wa uchaguzi watu kubambikiziana tuhuma za uhamiaji haramu.

Katika uchaguzi wa serkali za mitaa uliomalizika hivi karibuni ,Ccm kikitumia sana kipengele hiki ili kuwaondoa wapinzani katika kinyanganyiro,huku chenyewe kikiwasimamisha wagombea ambao pia wana utata wa uraia wao.

Mathalani katika kijiji cha Katera mgombea wa CCM aliyepitishwa bila kupingwa Fidel Peter ni raia wa Rwanda lakini mgombea wa Chadema alinyofolewa kwa pingamizi lililohusu u aria wake.

Nilikutana na Fidel Peter Katekista wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT)na alikiri kuwa baba yake ni Mnyarwanda lakini mama yake anatoka Ngara.Nilipomuuliza ikiwa aliisha kana uraia wa baba yake,alidai mbunge na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) walimueleza kuwa"wameshalimaliza na watu wa uhamiaji''.

Aidhaa Fidel Peter alidai kuwa yeye aliombwa na viongozi hao kugombea nafasi na walimuhaidi watahakikisha anapita bila kupingwa ili kumwepusha na hatari ya kuligawa kanisa lake kama angepiga kampeini.

TEKAJI NA UGAIDI
Mbunge wa Kyerwa ni Eustace Katagira;MNEC wa wilaya hiyo ni Daniel Damian na Mwenyekiti wa Halmashauri ni Kashunju Runyogote.

Wote watatu,kwa maoni ya watu wengi niliokutana nao tishio la amani wilayani Kyerwa.
Katika utatu na umoja wao wamejimilikisha nusu ya ardhi yote wilayani humo wanahodhi na kununua kahawa yote inayolimwa wilayani humo na wanamiliki mifugo(ng'ombe) wengi kuliko Ng'ombe wote wanaomilikiwa na wananchi wote kwa pamoja.

Watatu hao wanamiliki mitandao ya kibiashara halali na haramu wilayani humo na hakuna mtu mwingine mwenye ruhusa yakufanya biashara bila kibali chao.

Matokeo ya hali hiyo,watatu hawa wana nguvu ya kumwamuru kiongozi yeyote wa serkali wilayani humo kufanya lolote wanalotaka.

Katika machafuko yanayoendelea baada ya uchaguzi wamemwamuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa George Lukas Mukindo kwenda redioni na kurejesha mapingamizi dhidi ya wapinzani ambayo awali aliyafutilia mbali kwamba hayana msingi.

Kitendo hicho kilifanywa na Mkurugenzi kwa shingo upande tena nje ya muda uliowekwa na sheria kuhusu mapingamizi.
Nilipomuuliza Bw.Mukindo kuhusu tuhuma hii,alinijibu kwa mkato,"Wenye nchi wameshasema nitaongeza nini? Kawaulize wahusika."

Tangazo la Mkurugenzi huyo lililokuja nje ya wakati na huku kampeini zikiwa zimeishaanza,ndilo chimbuko la vitendo vya kigaidi dhidi ya wapinzani na pia ndilo chimbuko la kujichukulia sheria mkononi dhidi ya wagombea wa CCM.

Hata baada ya kura kupigwa,matokeo katika vituo vingi yalitangazwa chini ya mtutu wa bunduki.
Mwenyekiti wa Halmashauri hii diwani Kashunju ametamka wazi "anayepinga aende mahakamani na ajiande kufilisika."
Nilikwenda hadi nyumbani kwa Kashunju ilikumuuliza juu ya tuhuma hizi za ubabe.Alianza kwa kunihoji ninani aliyenipa kibali cha kuingia katika wilaya yake.
Aliongeza "kwa taarifa yako hata Rais Jakaya Kikwete kabla hajapanga mkuu wa wilaya hii sharti aniulize.IGP kabla hajapanga OCD ananiuliza na ata waziri Mkuu Mizengo Pinda kabla hajapanga mkurugenzi ananipigia simu.Je wewe ninani kakutuma apa"?
Akanikazia macho uku akisisitiza nimjibu vinginevyo hawezi kuongea nami.
Nilijitambulisha kwake kwa kumpa kitambulisho changu kisha akasema "ukitaka kunijua mimi ninani kamuulize mzee Mangula ananijua vizuri au kamuulize Kanali Masawe aliyechukua alama zangu za vidole kwa kunituhumu ulanguzi wa kahawa,sasa yuko wapi?
Nilimweleza sikuja kugombana naye isipokuwa kujua ukweli wa tuhuma anazosukumiwa.Alinikatisha kwa kusema "niza kweli nenda kaandike."
Aliniacha sebleni kwake na kuondoka.

Vitisho vya namna hii yawezekana ndivyo vinavyosababisha watendaji wa serkali kama mkuu wa wilaya, mkuu wa polisi wa wilaya,Takukuru na wengine kukaa kimya wakilinda vibarua vyao.

MATESO DHIDI YA WAFUASI WA CHADEMA
Safari yangu ilinikutanisha na baadhi ya waandishi wa habari wa redio na magazeti walio Karagwe na Bukoba.Wengine wao walinitisha kuwa genge hili la watatu ni la hatari sana na kwahiyo niwe mwangalifu na nyendo zangu.
Nilionja harufu ya ukweli huo baada ya kukutana na Mwalimu ajulikanaye kwa jina la Johanes uyu ndiye aliyekuwa msimamizi msaidizi wa kata ya Kitoma,Mwenyekiti Kashunju alimwita na kmlazimisha mbele ya polis kutangaza matokeo kinyume na yalivyokuwa.
Baadae alifuatwa na Polisi watatu waliomsachi ndani ya nyumba yake na kuchukua karatasi zenye matokeo halisi ya kata ya Kitoma.Tukio ili lilifuatiwa na wananchi wenye hasira kali waliovamia shamba na nyumba ya mgombe wa Ccm aitwaye Mwarabu na kuviharibu.

Baada ya tangazo hilo ndipo operesheni malum ya kuwakamata na kuwaweka ndani watu wote walioonekana wakiishabikia Chadema ilipoanza.Hadi ninaandika habari hii wafuasi wapatao 58 walikuwa wamerundikwa katika mahabusu ya Polisi Karagwe.

Aidha vitongoji vyote vya kata Kitoma vilikuwa havina wanaume kwa sababu walikimbilia maporini kujificha kutokana na vipigo vya Polisi na mateso ya wiki nzima.Waliochoka na kujisalimisha walikuwa wanatozwa kila mtu faini ya mabati matatu sh,50,000 (elfu hamsini) na kusaini kiapo cha kuachana na Chadema.
Wale walio mahabusu jamaa zao walikuwa kuleta lakini mbili na nusu ili kapata dhamana.Vitendo hivi vinaendelea mbele ya polisi,Takukuru na kusimamiwa kwa karibu sana na mkuu wa wilaya ya Kyerwa Kanali Benedict Kitenga.
Mateso haya yamesababisha vifo kadhaa visivyoripotiwa wazi kwa hofu ya kushughulikiwa na watawala wa wilaya.Lakini kifo ambacho kimesikitisha wengi nikile cha mtoto aitwaye Ndayanabo ambaye baba yake alikamatwa na polisi nakuwekwa mahabusu huku mama yake akikimbilia porini,mtoto huyo aliachwa peke yake nyumbani nakukutwa amefariki baada ya siku mbili.Bila ata chembe ya huruma maiti ya mtoto huyo ilizikwa bila kusubiri wazazi wake kufika,mama yake aliruhusiwa kufika kaburini baada ya kulipishwa mabati na fedha nakuahidi kuachana na vidole viwili.

Mwisho wa habari.

Baada ya miaka mitano tunarudi kwenye uchaguzi uku makovu yakiwa mabichi kabisa lakini tunaingia kwenye uchaguzi uku tukiwa na tume ya uchaguzi ileile,viongozi walewale sheria zilezile uku tukidhani walotusulubu mwaka 2015 mwaka 2020 wataweza kukubali kushindwa,tunakubali kuingia kwenye uchaguzi wakati maDC wakifukuzia kuwa RC na OCD akitafuta kuwa RPC kutokana na atakavyoshughulikia wapinzani asa CHADEMA.

MAONI YETU:October 2020 mchague moja aidhaa Chadema wasishiriki uchaguzi kama walivyofanya serkali za mitaa ili kuwakinga wanachama wao na madhara yanayotokana na uhuni wa wanaCcm wakiongozwa na wakuu wa wilaya au wakubali kutawanya wanasheria kila wilaya watakao wabana wakuu wa wilaya na maOCD kutoingilia uchaguzi na badala yake mpira ubaki na wanasiasa.
 
Mkuu hao waliokamatwa na kufungwa sio ni wilaya ya karagwe?? nilikuwa huko ktk kz za kichama ...hao watu wanatokea kata ya kiruruma ktk ukanda wa bushangaro...taarifa nilizonazo ni jamaa walifungwa miaka 30 wakakata rufaa wakapigwa maisha ...nikutoe hofu kuna mchakato chama kinafanya na soon wanaweza kupata dhamana na wkt huo Mambo mengine ya kisheria yakiendelea... kiukweli ccm ni zaidi ya magaidi
 
Mumeshaanza hofu mnataka tusishiriki ili mpate mteremko, mbwa nyie tutawanyoosha.
Mkuu ccm sio watu kbs, chadema walishinda vijiji 4 katka hiyo kata lkn mtendaji akawatangaza wagombea wa ccm ambao kura zao hazikutosha..sasa bc kukatokea vulugu kubwa mno ambayo ikapelekea wale waliotangazwa walazumike kuandika barua za kupinga ushindi wao, lkn cha ajabu kbs wakakamatwa wale viongozi wetu akiwemo na mwana mama mmoja wamefungwa ...yaani wee acha tu
 
Membe ndiye mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM mwaka huu ni suala la muda tu.
 
Mkuu hao waliokamatwa na kufungwa sio ni wilaya ya karagwe?? nilikuwa huko ktk kz za kichama ...hao watu wanatokea kata ya kiruruma ktk ukanda wa bushangaro...taarifa nilizonazo ni jamaa walifungwa miaka 30 wakakata rufaa wakapigwa maisha ...nikutoe hofu kuna mchakato chama kinafanya na soon wanaweza kupata dhamana na wkt huo Mambo mengine ya kisheria yakiendelea... kiukweli ccm ni zaidi ya magaidi
Asante kwa taarifa ila wanachama walioko mikoani asa vijijini wanateswa sana na hawana mtetezi.Chukua ushauri apo juu.
 
Mkuu ccm sio watu kbs, chadema walishinda vijiji 4 katka hiyo kata lkn mtendaji akawatangaza wagombea wa ccm ambao kura zao hazikutosha..sasa bc kukatokea vulugu kubwa mno ambayo ikapelekea wale waliotangazwa walazumike kuandika barua za kupinga ushindi wao, lkn cha ajabu kbs wakakamatwa wale viongozi wetu akiwemo na mwana mama mmoja wamefungwa ...yaani wee acha tu
Nashangaa eti kuna haki za binadamu wanaishia mijini tu.
 
Back
Top Bottom