Ndugu wanajamvi,
Napenda kuwajuza kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ktk chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa hii leo wamekubaliana kwa kauli moja ya kujiunga na shirikisho la wanachama wa CHADEMA wanao soma vyuo vikuu hapa nchini kwa kifupi CHASO.CHASO ktk mkoa wa Iringa inashirikisha vyuo vya Mkwawa,RUCO na Tumaini.
Hivi karibuni kulizuka sintofaham baina ya wanachama wa CHADEMA Mkwawa kuhusu muundo wa shirikisho hilo,hata hivyo ktk kikao cha leo wanachama wa chama cha demokrasia Mkwawa wamekubaliana kujiunga na shirikisho hilo ikwa nikuonyesha ukomavu wa kisiasa na kuimarisha zaidi dhana ya CHADEMA ya utawala wa majimbo itakayo tekelezwa kuanzia mwaka 2015 pale dola itakapokuwa mikononi mwa CHADEMA.
Katika hatua nyingine katibu mwenezi wa chama Tawi la Mkwawa alipokuwa akisoma ripoti ya chama aliwambia wanachama kuwa,CHADEMA sasa Mkwawa inaimarika kila kukicha idadi kubwa ya wanachama wamekuwa wakiongezeka nakufanya chama kizidi kuwa na nguvu.
Ndugu wanajumvi ni mtaji mkubwa sana kwa CHADEMA kuona jamii ya wasomi hususa ni waalimu wanao deal na kizazi cha kesho wanajiunga na jeshi la ukombozi.
VIVA CHADEMA.