Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Chadema Mkoa wa Dar Es salaam,Tunaunga Mkono Msimamo wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Kwakutokufanya kazi na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Ndugu Paul Makonda vile vile Tunalipongeza Jukwaa hilo Kwa kumtangaza Mkuu huyo wa Mkoa kama Adui wa Uhuru wa vyombo vya habari Nchini.
Vyombo vya habari vinapaswa kuendelea kuwa imara na kusimama kwenye Misingi yao pasipo kuogopa ama kupokea vitisho vyovyote vile kutoka ngazi yeyote ile kwani Taifa letu haliongozwi na mihemuko ya viongozi bali Taratibu na Sheria mbalimbali tulizojiwekea.
Na ikumbukwe ni Juma moja sasa toka Mkutano Maalum wa Kanda ya Pwani Uliyofanyikia kwenye Mkoa wetu wa Dar Es salaam uliyokuwa ukihutubiwa na Mwenyekiti wetu wa Taifa Mhe.Freeman Mbowe Kuazimia kwa pamoja Kwa Wabunge,Mameya,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Kutompa Ushirikiano wowote ule Mkuu huyo wa Mkoa kutokana na Matendo yake ya Kuudhi na kuzalilisha.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Jukwaa hilo la Wahariri ni hatua muhimu sana katika uhuru wa vyombo vya habari pamoja na uwajibikaji wa viongozi wa Umma pale wanapokuwa na tuhuma mbalimbali na Kushindwa kuzitolea Ufafanuzi wowote ule.
Chadema Dar Es salaam tunaamini Umma wote kwa pamoja ukisimama na kukemea vitendo kama hivi vya kihuni,kibabe,Ulevi wa Madaraka uliyopilitiza utakomesha Udhalimu Huu wa Maksudi wa kukingiana kifua Hata pale Makosa yanapokuwa dhahiri bila kuacha Shaka yeyote.
Ni rai yetu kwa mteule wake aliyemteua atasikiliza Sauti za Watu kuliko kuzipuuza na kumumchukulia hatua Kali na vikiwamo vyombo vingine sitahiki kumchukulia hatua za kisheria haraka iwezekanavyo kabla hajasababisha Madhara mengine kwenye jamii yetu.......
By Henry Kilewo
Katibu Greater Dsm ---Chadema
24/03/2017