CHADEMA Mbeya ni ‘insiders’ na ‘outsiders’

CHADEMA Mbeya ni ‘insiders’ na ‘outsiders’

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538


  • Kila kundi larusha tuhuma
  • Wabunge wadaiwa kuweka mizengwe

UCHAGUZI Mkuu ujao wa mwaka huu umekipasua CHADEMA mkoani Mbeya vipande viwili, kundi la wakuja, linalojulikana kama outsiders, na wenyeji insiders. Wanachama wa chama hicho hivi sasa wanatazamana kwa uenyeji wao katika chama hicho na ugeni pia.

Kila kundi linamshutumu jingine kwamba limeweka mikakati ya kuwakwamisha, na kundi la "outsiders," likienda mbali zaidi kwa kuwashutumu wabunge waliopo madarakani kuzuia wanachama wapya wenye uwezo kujiunga na chama.

"Wapo watu wanaofikiri ubunge kama nafasi ya kudumu. Mtu akiwa mbunge hataki wengine waingie, wanaona kama wanakuja kuchukua nafasi zao. Hawataki watu wenye uwezo waingie, ukijitokeza mwenye kuruhusu watu waingie, wanapata hofu," anasema Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Frank Mwaisumbe.

Mwaisumbe anatajwa kuwa katika kundi la wakuja, outsiders, ambapo ametoa ufafanuzi, katika mahojiano maalumu na Raia Mwema kwa njia ya simu, kuhusu shutuma anazotupiwa kwamba anawapiga vita wanachama na viongozi waandamizi wa chama hicho mkoani Mbeya, na kwamba anatengeneza safu yake ya uongozi wa kanda kwa kuweka watu alioingia nao.

Kiini cha mifarakano CHADEMA Mbeya;
Kuibuka kwa makundi hayo ndani ya chama hicho mkoani Mbeya kunaelezwa kuchangiwa zaidi na harakati za Uchaguzi Mkuu utaofanyika baadaye mwaka huu, ambapo wamejitokeza baadhi ya wanachama na viongozi wenye kupanga nani akiwakilishe katika nafai za udiwani na ubunge. Hata hivyo nafasi ya ubunge ndiyo yenye kuvuta hisia za wengi na kuonekana kuwa msingi wa migongano hiyo.

Uthibitisho wa nafasi hiyo ya ubunge kuwachanganya viongozi wa chama hicho mkoani humo, unajibainisha katika idadi na aina ya wanachama waliotangaza nia. Takribani viongozi wote wametangaza nia ya kugombea katika majimbo mbalimbali mkoani humo, kuanzia wale wa Ofisi ya Kanda hadi ngazi za Mkoa, Wilaya na Kata.

Yapo madai, mathalani, kwamba katika Sekretarieti ya Kanda yenye watu 12, wote wametangaza nia kugombea ubunge kwenye majimbo mbalimbali mkoani humo.

Taarifa za awali zilizolifikia gazeti hili, zinabainisha kwamba takribani wanachama 20 wa CHADEMA wamejitokeza katika kila jimbo mkoani humo, kuomba ridhaa ya chama chao kupitishwa katika nafasi ya ubunge.

Kuwepo kwa idadi kubwa ya wanachama wenye kuwania nafasi hiyo ya ubunge, katika majimbo ya mkoani Mbeya kumezua hofu miongoni mwa wapenda mabadiliko mkoani humo, wakiamini kuwa ni hatua itakayokidhuru chama kwa kuingiza siasa za makundi ndani ya chama.

Kundi la insiders linamshutumu Mratibu wa Kanda, kwamba amekuwa na mkakati wa kuwadhoofisha kisiasa, na miongoni mwa mbinu anazotumia ni kulidhibiti kundi hilo kwa kujenga taswira yenye kuwaonyesha kuwa hawatokuwa na msaada wowote kwa wapigakura wao iwapo watawachagua.

Mbinu hiyo inaelezwa kutekelezwa kwa sura tofauti, mojawapo ikiwa kupeleka vitendea kazi vya chama kwenye majimbo walipo walionyesha nia kutoka katika kundi la la wageni (outsiders).

Chanzo chetu ndani ya CHADEMA mkoani humo, jina linahifadhiwa, kinabainisha kuwa katika majimbo ambako vifaa vilishapelekwa lakini hakuna watu wake, kilitumika kikosi cha walinzi wa chama hicho maarufu kama "Red Brigade," kuvinyang'anya na kuvigawa kwenye majimbo waliko swahiba wake.

Hujuma nyingine anayotupiwa mratibu huyo, ni madai ya kufanikisha njama za kumuengua mwanachama aliyeongoza katika kura za kupata jina litakalopendekezwa katika Kamati Kuu kwa ajili ya nafasi ya Katibu wa Mkoa wa Mbeya.

Mwanachama anayetajwa kuongoza katika mchakato huo alikuwa Boyd Mwabulanga ambaye pia ni Diwani wa chama hicho katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, lakini inaelezwa alienguliwa na badala yake kupelekwa jina la Fanuel Mkisi, anayelezwa kutokea ofisi ya kanda na miongoni mwa kundi la outsiders.

Mwabulanga alikiri, katika mahojiano yake na Raia Mwema, kuongoza katika kura za mchakato huo na kwamba jina lake lilienguliwa baadaye. Hata hivyo hakuwa tayari kuingia kiundani kuhusu hujuma dhidi yake kwa maelezo kuwa ni suala linaloshughulikiwa na makao makuu kwa sasa.

Mkisi anadaiwa kuteuliwa na Mwaisumbe kushika wadhifa huo wa Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, hata bila ya idhini ya Kamati Kuu au Ofisi ya Katibu Mkuu, kama taratibu za chama hicho zinavyobainisha.

Taarifa za ndani za chama hicho mkoani Mbeya, zinafichua zaidi mbinu zilizotumika kuwa ni pamoja na kumuweka katibu wa mkoa, pamoja na wale wa wilaya kutoka ndani ya sekretarieti ya kanda ya chama hicho ambao watafanikisha mkakati wao wa kupitishwa kwenye majimbo kuwania nafasi ya ubunge.

Miongoni mwa watangaza nia kutoka sekretarieti hiyo, jimbo kwenye mabano, ni pamoja na Mratibu (Mbeya Vijijini), Mwenyekiti (Rungwe Mashariki), Makamu Mwenyekiti (Njombe), Sera-Kanda (Mbozi Mashariki), Mkufunzi CHADEMA Msingi (Mbozi Mashariki), Mwanasheria wa Kanda (Mbozi ), Hamasa (Rungwe Magharibi na Mwenyekiti CHADEMA ni Msingi (Chunya).

"Mkisi alipendekezwa na Kanda kuchukua nafasi ya Katibu wa Mkoa japo alikuwa wa pili katika kura za mchakato wa kumpata katibu, huyu naye ni kutoka sekretarieti ya kanda," kinaeleza chanzo chetu.

Chanzo chetu kinabainisha kuwa mbali ya Mbeya, mikoa mingine katika Kanda hiyo ambayo chaguzi zake za mchakato kuwapata makatibu zilivurugwa na Kanda ni pamoja na Rukwa, Iringa na Njombe.

Kwa mujibu wa taratibu za chama hicho, chaguzi za Majimbo na Wilaya husimamiwa na Mkoa, na kwa Mkoa wa Mbeya waliingiza mwakilishi mmoja kutoka kanda katika kila chaguzi. Hata hivyo, chaguzi hizo zilibatilishwa na kanda bila Ofisi ya Mkoa kuwa na taarifa na inaelezwa kuwa kanda ilisimamia chaguzi mpya iliyoitisha kinyume cha taratibu.

Mwaisumbe ajibu akiwashangaa insiders
Mratibu Kanda, Mwaisumbe anashutumiwa kuwa chanzo cha migogoro ndani ya chama hicho mkoani Mbeya, jambo ambalo yeye mwenyewe analikanusha na kubainisha kuwa ni wasiwasi tu wa walalamikaji kupoteza nafasi zao.

Mratibu huyo anashangaa baadhi ya wanachama kulalamika kuhusu wanachama wengine kutangaza nia kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao akisema hatua hiyo kwanza haina maana huyo mtu ni mgombea tayari.

"Kwa sasa watu wanaonyesha nia tu, kesho mtu anaweza kujitoa, huwezi sema hawa ni wagombea, wapo watakaoacha, watakaoshindwa kwenye kura za maoni na watarudi kuendelea na shughuli za chama," alisema Mwaisumbe akijibu swali kuhusu madai ya sekretarieti nzima kuonyesha nia ya ubunge, kisha akaongeza.

"Hizo ni siasa za hapo Mbeya, watu wana hofu za bure, kuna watu wanagombea wao, wana hofu hawatapita, sekretarieti ya Kanda ina watu 12, waliotangaza nia ni watano tu, watatu wakitoka jimbo moja".

Kwa mujibu wa Mwaisumbwe, suala la watendaji na viongozi wa chama hicho kugombea sio geni ndani ya chama hicho, ambapo ametoa mfano wa Mwenyekiti wao Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Wilbroad Slaa, kwamba ni viongozi wa chama lakini nao wanagombea.

Anatoa ushahidi zaidi wa hatua hiyo akisema kuwa takribani sekretarieti yote makao makuu ya chama chao wanagombea, wapo madiwani, Mwenyekiti Iringa anagombea Mufindi Kusini mkoani humo na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kote wameonyesha nia kuwania nafasi za ubunge na udiwani katika uchaguzi ujao.

Mwaisumbe anayewekwa kwenye kundi la outsiders, alionyesha mshangao wake akisema hayo ni mawazo mgando, na kwamba vyama vingekuwa na mtazamo huo basi visingekua.

"Kama ni suala la waasisi basi chama kingebaki na kina Mzee Edwin Mtei peke yao waliokuwa kama sita hivi, hata CCM wanachama na viongozi walipo leo ni tofauti kabisa na waasisi," anasema Mwaisumbe na kuongeza,

‘Umiliki wa chama upo kwa wanachama, na uachama haijalishi umejiunga leo, jana au juzi. Thamani ya chama ni watu kujiunga. Watu ndio wanachagua bila kujali CCM, CHADEMA au CUF.

Insiders wanajiona kuwa na haki zaidi katika chama, wakisema wao ndio waliolima shamba, hivyo ndio wenye haki ya kuvuna, wakati upande wa outsiders wao wanawashangaa, wakisema hiyo ni hatua ya kukidumaza chama. Wanaamini chama bado kinahitaji wanachama zaidi na wote wana haki sawa awe amejiunga leo, jana au juzi


Chanzo: Rai Mwema
 
Kuna tetesi pia kuwa mchumba wa dr. Slaa, mushumbusi kugombea kawe na mdee kupigwa chini
 
Mdee njoo ACT ugombee jimbo hilo hilo la kawe tunakupa tena ubunge
 
Kuna tetesi pia kuwa mchumba wa dr. Slaa, mushumbusi kugombea kawe na mdee kupigwa chini

Kumbe tetesi?! Sasa za ukweli ni hizi, Zitto anajijenga kisiasa kwa umea, uongo na unafiki na kudharau wenzake. Nyingine ni hii, Kinana ana sifa zote za kuitwa Mhuni. Ameiba mashine ya kufulia mashuka pale Mount Meru Hospital, na pia anapapasa matiti wanawake hadharani.
 
Kwa viongozi wa chadema wala si jambo laajabu.

Agombee Mara Mbili ? wakati ameisha chaguliwa kuwa MWENYEKITI wa BARAZA LA WANAWAKE wa CHADEMA... Kwahiyo ni mbunge wa kuteuliwa in waiting 2015; ni kama SOPHIA SIMBA CCM

watakuwa kwenye vile viti Maalumu vya Wanawake
 
Itakuwa heri maana CCM lazima ishinde hapo, na tujengewe mabarabara sasa.
Mdee katuletea ukame wa maendeleo.

Aliye waroga magamba atakuwa amesha kufa,angekuwa hai angewarudishia fahamu mungeweza kujitambua jinsi musivyo faa kupata jimbo hata moja.
 
positive mgongano huo.. Mwisho wa siku vijana wa Mwanjelwa huwa hawanunuliki hawahongeki Nondo kama kawaida ... Tunajua kuwa kwa sasa Raiamwema wametekwa na association of criminals in Tanzania! kila siku wanatafuta jinsi ya kuipekenyua CHADEMA kwa maslahi mapana ya CCM ....
 
Agombee Mara Mbili ? wakati ameisha chaguliwa kuwa MWENYEKITI wa BARAZA LA WANAWAKE wa CHADEMA... Kwahiyo ni mbunge wa kuteuliwa in waiting 2015; ni kama SOPHIA SIMBA CCM

watakuwa kwenye vile viti Maalumu vya Wanawake

Umesahau ya mwenyekiti aliyepita kuhamia NCCR kisa viti maalum?
 
positive mgongano huo.. Mwisho wa siku vijana wa Mwanjelwa huwa hawanunuliki hawahongeki Nondo kama kawaida ... Tunajua kuwa kwa sasa Raiamwema wametekwa na association of criminals in Tanzania! kila siku wanatafuta jinsi ya kuipekenyua CHADEMA kwa maslahi mapana ya CCM ....

Ni kweli mkuu,Raia mwema nimeishaipotezea kabisa,habari zao nyingi ni majungu majungu tu
 
Raia Mwema ya sasa hovyo kabisa!

Mhariri Ezekiel Kamwaga aliwahi kuishutumu UKAWA kwamba ilimfanyia figisu Ommy Dimpoz asiingie Marekani. Tokea siku hiyo nilimdharau sana jamaa
 
Ccm ipo kazini. Haya Nenda kawaambie watz huko nje km hamtapopolewa mawe. Nyambaaafuuuu
 
Back
Top Bottom