MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Nimeshangazwa sana kuona
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikitoa tamko la kutoshiriki Uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata 14 zilizopo kwenye Halmashauri 13.
Nimezisoma sababu zilizotajwa na CHADEMA kutoshiriki uchaguzi huo, kwa kweli sababu hizo hazina mashiko.
Kwa mfano hili suala la CHADEMA haitashiriki uchaguzi huo kutokana muda wa Kampeni kuwa mdogo (Julai 1 hadi 12, 2023) haliingii akilini, wanashindwaje kufanya kampeni katika muda huo? Au wanaukata wa fedha za kuendesha kampeni? Hapana! Mbona mwezi March 2023 walianza kupokea ramsi ruzuku kutoka Serikali, hivyo chama hicho kina pesa za kutosha za kuendesha kampeni hizo, au fedha za ruzuku zinaishia mifukoni mwa viongozi wajanja ndani ya chama .
Mbona vyama vingine ikiwemo ACT - Wazalendo havijalalamikia kuwa muda huo wa kampeni mdogo. Sasa ninachokioana ndani ya CHADEMA ni UOGA na kukosa ukomavu wa kisiasa kutokakana na kutokuwa na uhakika wa kushinda uchaguzi huo.
Pia, ninashangaa kuona CHADEMA ikikataa kushiriki uchaguzi huo kwa kuwa unasimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri. Kwani katika chaguzi zilizopita ikiwemo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na mwaka 2015 CHADEMA ilishinda baadhi ya nafasi za udiwani katika chaguzi hizo ambazo zilisimamiwa na Wakurugenzi.
Hivyo, ninachokiona hapo CHADEMA imeamua kujificha katika KICHAKA cha muda mdogo wa kufanya kampeni na kupinga uchaguzi kusimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri ili kuficha UOGA na HOFU ya kushindwa katika uchaguzi huo.
CHADEMA rudini mchezoni ili wawape wananchi haki yao ya msingi ya kidemokrasia ya kuona kuna wagombea wengi wa nafasi ya udiwani kutoka vyama mbalimbali vya siasa na kuamua kuwachagua wagombea wanaowataka kulingana na mazingira na mahitaji yao.