CHADEMA kushirikiana na chama cha Centre Party cha Norway

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
GGG.JPG

Habari zenu watanzania wapenda demokrasia,

Leo tarehe 28.04.2016Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Centre Party cha Norway, Knut Olsen (kushoto) wakitia saini makubaliano ya awamu ya pili ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili katika Mradi wa Elimu ya Demokrasia, leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi ya Makao Makuu ya CHADEMA. Mradi huo unaohusisha vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) unaendelea katika kata za Wilaya ya Mtwara Vijijini.
 
Kumbe na Vyama vingine vyenye uwakilishi Bungeni watasaini makubaliano ya awamu ya Pili!
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Centre Party cha Norway, Knut Olsen Leo wametia saini makubaliano ya awamu ya pili ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili katika Mradi wa Elimu ya Demokrasia .Mradi huo unaohusisha vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) unaendelea katika kata za Wilaya ya Mtwara Vijijini
 
Attachments

  • Ai7W-rInz7rsdn-oFydX_iGEoDI--5LQTP_hTmckdOCH.jpg
    Ai7W-rInz7rsdn-oFydX_iGEoDI--5LQTP_hTmckdOCH.jpg
    71.4 KB · Views: 53
muda wa mashinji kutafuna pesa za chadema umefika.. utasainiwa na hakuna elimu yoyote itakayotolewa utasikia kila siku semina za kutafutia posho tu
 
Wame sign ktk ofisi zile zine alizokataa Lowasa au mikocheni? (Hii aibu sasa kwa chama kikubwa cha siasa Tanzania)
chama sio ofisi bali ideology na falsafa na watu wanaoikubali. Kanu Kenya ilikuwa na majengo kama ccm ikaja kuuawa na vyama visivyo na ofisi, Leo Ni hayati
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Centre Party cha Norway, Knut Olsen Leo wametia saini makubaliano ya awamu ya pili ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili katika Mradi wa Elimu ya Demokrasia .Mradi huo unaohusisha vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) unaendelea katika kata za Wilaya ya Mtwara Vijijini
Yaani huyo mzungu akiweka simu karibu dirisha imeenda na mateja na akienda nyuma ya jengo anageuka mteja Kwa dada poa
 
Back
Top Bottom