CHADEMA kunajisi mkutano CCM

Hakuna haja ya kwenda huko Dodoma..
Siku ambayo CCM wanafanya hayo huko..na CHADEMA kuwe na mkutano hapo Dar..mbona ni kazi ndogo tu!

Kwenda huko ni kupoteza muda..Andaeni mkutano Dar siku hiyohiyo!!
 
Hao vijana sio wa Zamani,labda wawalipe pesa ya Maana.
Maana wanajitoa kafara na wengine kuozea Jela huku wakuu hakuna hata mmoja anaeingia kwenye zogo hilo.

Vijana wa sasa sio wale wajinga wa kizazi cha maandamani,sasahivi watu wanaaakili zao.

Yaani sasahivi CCM kama imewashikia remote Chadema,maana wanachezeshwa wanavyotaka wao,hahaha aiseee
Rudini majimboni kwenu kwanza mkaongee na wananchi na sio ujinga huu.
Chama Tawala ni habari nyingine kabisaaa
Pole sana, hoja hamna hapo.
 
Nafikiri hawa wanaosoma bure sasa huenda ndio wakawa vijana halisi wa Tanzania na kuachana na haya masaka tonge. Wajiandae kutoka manundu na kuvynjwa miguu halafu na wake zao wasaidiwe kulea. Waathirika wa Arusha wamekwisha sahaulika ndani ya chadema mwaka huu hakuna aliyekumbuka.
Huyu mjinga siwalisema ametoweka. Mbona alipopatikana hawakujulisha. Au walikuta anafanywa kitu kibaya ambacho hakifai kutangazwa.
Mbona mko bize kuota ndoto mpya
 
Tatzo ni kwamba BAVICHA mna MATAMKO mengi mno ya kuandamana TOKEA AWAMU HII imeanza na HAMNA HATA TAMKO MOJA MLILOTEKELEZA....ndio maana tunasema haya matamko ni MRADI WA HAWA VIJANA KUJIPATIA POSHO....maana hakuna cha maana wanachofanya zaidi ya kubwabwaja
Kwa hiyo
 
Wameshindwa kulinda kura mita 2000 kwny kata zao mpaka "zikaibiwa" wataweza kweli kusimamia wayasemayo?
 
Tangu lini nyumbu anayevuka mto akamzidi akili mamba anayeishi kwenye mto huo ?
 
Watanzania wenye kuweza kununua sukari basi tununue kwa wingi tuwasaidie ndugu zetu wa vijijini kule sukari bado ni bei juu na vipato vyao viko chini.

Nawashauri tu Chadema. Wasiige mbinu mufilisi kama za CCM badilisheni Mbunu za kisiasa.
Nawashangaa sana CHADEMA. Naona kwa sasa hakuna vijana kama enzi za Kina Zito Kabwe na Enzi za kina Mbowe. Serikali ya CCM haijawahi kuwa rafiki kwa wapinzani. Wala msifikiri Magufuli ni dikteta la hasha huo ndio utawa wa CCM. Utawala unaotumia nguvu kuliko akili.
Utawala wa nguvu hauangushwi kwa nguvu unaangushwa kwa akili.

Tumieni akili kuirudisha serikali ya CCM kwenye mstari wa kuomba poo.

Wamevurunda mno mwaka huu hao CCM na wabunge wao ,wamepitisha bajeti mzigo mkubwa kwa mananchi. Sijui walikua wanajadili nini bungeni.
Serikali inaweka VAT kwenye pato la watoa huduma wa mitandao bila kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wake na namna hiyo VAT itaiavyolipwa.

VAT siku zote inamwangukia mteja sasa sijajua sheria imebadilika lini.
BAVICHA wapange mikakati mikubwa zaidi za kumkomboa mtanzania kifikra.
Bado watanzania wanaishi kishabiki.
Bado tuna ushabiki wa kidini dini.Ushabiki wa kikabila kabila . Ushabiki wa Kikanda kanda. Na ushabiki wa kichama chama bila kuweka mbele maslahi ya wananchi na Taifa.
BAVICHA wamesahau namna ya kuendelea kuwaunganisha wamachinga na watu wa bodaboda nchi nzima na jukumu hili sasa limebaki kwa UVCCM. Hili kundi ni la muhimu sambamba na wasomi wa vyuo na masekondari. Wasitumike tu kwenye maandamano na migomo inayoonekana kwa macho bali tafuteni mbinu za kisayansi.
Nakumbuka wakati fulani wanawake kenya walifanya migomo ya ajabu sana ili tu kufikisha ujumbe wao.
Sio lazima mfanye migomo ya kukimbizana na polisi.
Kwa sasa Polisi na CCM lao ni moja.
Na hata suala la Lugumi lilivyomalizwa kule bungeni ni dalili ya kuwabeba mafisadi ndani na nje ya mfumo huo. Usitegemee polisi wawapende wapinzani. Wapinzani nia adui mkubwa wa wezi wa rasilimali za umma. Tulisikia gazeti moja likiwataja baadhi ya vigogo wa polisi kumiliki mashamba zaidi ya heka mil.1 na nyumba 40 za kifahari Dsm lakini hakuna hata Mbunge mmoja wa CCM aliyesimama bungeni na kusoma lile gazeti na kumuliza waziri kuhusu ukweli wa tuhuma hizo. Na hatua gani zimechukuliwa kwa mmiliki wa gazeti kama ni uongo.
CCM Walikaa kimya mana aliyetuhumiwa ni msaidizi wa kuwapigania wazidi kutawala nchi kwa ujanja ujanja.

Chadema kianzi kujiimarisha kwenye uongozi wa Mikoa ,wilaya ,Kata,vijiji na vitongoji.
Wanze pia kujenga ofisi ya makao makuu ya taifa.
Tena Rais aliwapa wazo zuri sana kwamba wahamishie makao Makuu ya CDM Dodoma. Ushauri ule ni wa muhimu sana.

Ukipita huko vijiji na hata mawilayani CHADEMA hawana ofisi kabisa. Sasa wanazungumzia mambo yao wapi? Mikakati yao inafanyikia wapi?

Chama hakiwezi kujengwa barabarani.

Kwa kweli itakuwa ni vigumu sana kwa polisi na Bavicha kwenda kwenye jengo la CCM na kuzuia mikutano ya ndani ya CCM. Mikutano inafanyika kwenye jengo lao la chama. Hapo ndio nyumbani kwao huwezi kuwazuia wasiingie kukaa kwenye majengo yao.

CHADEMA jengeni kumbi zenu za kitaifa na ofisi kila kijiji. Ni rahisi kwani watanzinia wanajitolea sana kujenga maabara na madawati ,wanakua tayari pia kujenga ofisi za chama hasa wakimtumia Lowasa na Sumaye kuhamasisha michango ya ujenzi wa maofisi ya chama inawezekana.

Ofisi za Chama huwa ni alama ya umoja na sehemu ya kuweka vijiwe huko vijijini hata vya kuuza na kunywa kahawa, kucheza drafti, kucheza bao wakati wa jioni na kujadili masuala ya kimaendeleo na sera za chama.
Ni ushauri tu wa bure kabisa. Ni kutokana na mahaba yangu kwa Demokrasia na utawala bora.
Tusipoishauri CHADEMA na wapinzani namna bora ya kuendesha siasa basi kuelekea 2020 hivi vyama vitakufa vyote isipokua vile vichanga kabisa visivyo naadhara kwa CCM vitanufaika kwa kushirikiana na CCM kuua vile vikubwa.
Demokrasia ikitoweka Tanzania ni mwanzo wa kuingia kwenye machafuko kwani kuna kila dalili ya wachache wenye nguvu kuwatawala wanyonge wengi kimabavu.

Demokrasia kwanza.
 
Tutahakikisha tunalisaidia jeshi letu
Kama ccm wamepanga kuvunja sheria basi wajiandae kutuuwa tuko tayari kufa ili mradi haki ipatikane
 
Vijana hao wanasema wanakwenda Dodoma kusaidia Jeshi la Polisi katika kuzuia mkutano wa CCM...sasa itakuwaje kama Jeshi la Polisi litakataa msaada huo?
by force watasaidiwa tu.

swissme
 
umesema kweli
 
Chadema andaeni mkutano ck hiyo hiyo police wakiwazuia ndio tujue, mchezo wa bata na kuku
 
Tutahakikisha tunalisaidia jeshi letu
Kama ccm wamepanga kuvunja sheria basi wajiandae kutuuwa tuko tayari kufa ili mradi haki ipatikane
mlisrma mtafanya mikutano kwa nguvu, mbona sijaona tena mkifanya hyo mikutano?? maneno dhidi ya vitendo, mnaongea Sana alafu vitendo 0
 
Back
Top Bottom