CHADEMA kunajisi mkutano CCM

bavicha kwenda Dodoma kizuia mkutano ni jambo la msingi?? una amini ni kqeli wataenda Dodoma?
Mikutano kwa ccm ni sawa kwa wapinzani hapanaalafu mnajinasibu nchi hii inautawala wa sheria? Je ni kweli tunademokrasia nchi hii?
 
KUKOSEKANA KWA HAKI KUNAWEZA KUSABABISHA MACHAFUKO
Mimi Mwanzoni nilikuwa kikisikia magaidi nadhani hawana akili. Lakini sasa hivi naanza kuona kuwa mtu yeyote anaweza kuwa gaidi hata mimi mwenyewe. Make haki inapotolewa kwa upendeleo kwa baadhi ya watu fulani na wengine wakanyimwa haki hiyo. Vitendo vya kigaidi haviepukiki. Viongozi wetu waache upofu. Magaidi mnawatengeneza wenyewe. Kama mataifa yaliyoendelea yanaangaishwa na ugaidi sembuse Tanzania. Tunajidanganya tu eti tunaulinzi wa hali ya juu. Ugaidi ukianza hamtaweza chochote.
 
Kwahiyo mikutano na vikao kwa ccm ni sawa kwa upinzani hapana?
jibu: kwa ccm ni sawa, mikutano ya chadema haina tija wala maana yoyote!! nimefurah sana ilivyokatazwa na kama watakaidi, naamini jeshi la polisi hawatatuangusha, ni mwendo wa virungu tu!!
 
hakuna watu waoga kama hao bavicha , alafu nauli ya kwenda Dodoma hawana ,pili hayo matamko yao hayana madhara yoyote! mwisho kabisa, naliamini sana jeshi la polisi, ikitokea wakaenda najua polisi hamtatuangusha wananchi!!
 
jf mmoja hapo juu made my day! ati yamkini vijana wa ccm wakavuruga mkutano ili jk asimkabizi uenyekiti jpm.
 
jf mmoja hapo juu made my day! ati yamkini vijana wa ccm wakavuruga mkutano ili jk asimkabizi uenyekiti jpm.
 
Hakuna chama cha hovyo kama chadema,waliowapa kura wameliwa,kila sikuu usanii tu,toka lini polisi wakasaidiwa kufanya kazi na bavicha
Ni vizuri kama polisi wakikaa pembeni tuone nani atajaribu kuzuia ccm isifanye vikao vyake
Nani mwenye haki ya kusaidia polisi?Juha wewe
 
WAMEMALIZA SHUGHULI KINACHOBAKI NI MACHO NA MASIKIO YAKO KUSIKIA KILE KITAKACHO ENDELEA

NB: kuwa wa mwisho kusema ndio busara itakapopimwa usiwahi kutamka ya moyoni mwako unaweza kuaibika kwa msimamo wako mzuri.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kulisaidia Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilitoa zuio la mikutano ya siasa ya wazi na ya ndani nchini kote, hata hivyo CCM imepanga kufanya Mkutano Mkuu tarehe 23 Julai mwaka huu mjini Dodoma.

Kwenye mkutano huo, Dk. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM atakabidhi mamlaka hayo kwa Dk. John Magufuli ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa chama hicho.

Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) limepanga kuzuia mkutano huo kwa madai ya kulisaidia Jeshi la Polisi kusimamia agizo lake kwa vyama vya siasa nchini.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Slaam viongozi wa Bavicha wamesema, hatua hiyo ni katika kuhakikisha wanalisaidia jeshi kutekeleza amri iliyotolewa na Rais Magufuli ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa hadi mwaka 2020.

“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokwenda Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM. Kwa sababau Jeshi la Polisi limezuia mikutano yote ya siasa kwa sasa.

“Pia ni katika kuunga mkono kauli ya Rais Magufuli kwamba, hakuna mikutano ya vyama vya siasa mpaka mwaka 2020. Huu ndio msiamamo wa baraza.

“Mikutano yetu sisi kama Chadema tunazuiwa lakini CCM wanafanya. Mahafari ya chama cha mapinduzi yanafanyika. Ni jana CHASO (Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema) Morogoro tumezuiwa lakini UVCCM (Umoja wa Vijana wa CCM) Mkoa wa Morogogo wamefanya na picha zipo. Hii sio haki, kama mbwai na iwe mbwai,” amesema Patrick ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo.

George Tito, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya amesema “… ni kwamba, huko mikoani vijana wameshajipanga. Wana ari kubwa ya kwenda Dodoma.

“Tumeamua kufikia hatua hii kwa sababu tumekuwa tunaona hakuna haki katika nchi hii. Kuna mahafali yanafanyika vyuo vikuu, wenzetu CCM wanaruhusiwa sisi Chadema tunakatazwa.Vijana wa Chadema wamekuwa wakikamatwa bila sababu za msingi,” amesema Tito.
Kama kweli sheria ni msumeno basi hao vijana wana haki ya kusema hivyo
 
Back
Top Bottom