CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!

Katika muendelezo wa kuwafikirisha, nimeona leo niwaandikie kuhusu hali ya Upinzani na kampeni zinavyoendelea hapa nchini, ambapo hali ya sintofahamu ikiendelea kudhirihi kwa CHADEMA na Kambi yote ya Upinzani hapa nchini, wachambuzi mbalimbali, wasomi na waandishi wameendelea kuandika wakijaribu kuonyesha tatizo lililoikumba kambi hiyo, wengi wao wakisema FEDHA, vipande vya rupia vilivyoingia CHADEMA vimewafarakanisha. Nami Binafsi ktk muendelezo huo huo wa kuchambua hali hiyo nitaeleza CHANZO ama SABABU halisi ya SINTOFAHAMU inayoikumba kambi ya Upinzani.

Kwa Muhtasari sana, niseme CHANZO na SABABU HALISI ya Upinzani kukosa muelekeo na kufikia hapa tulipo ni OMBWE la UONGOZI katika kambi hiyo ikiongozwa na CHADEMA..Mimi niliwahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, tena Kiongozi Mkubwa katika jumuiya yake ya Vijana, nilipata fursa ya kushiriki, kuhudhuria na kuchangia katika vikao na mikutano mikubwa, muhimu na nyeti ya Chama hicho.

Ilikuwa bayana kwetu kuwa, ilipofikia CHADEMA ilihitaji UONGOZI mpya utakaokuja na dira, maono na tafakuri mpya ambayo ingeki-transform chama hicho kuwa chama kamili cha siasa na kuondoa uongozi wa hamasa na mihemko ya kiuanaharakati..

Nikiwa ndani ya Vikao vya CHADEMA nikaliweka hili BAYANA kuwa tunalo ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA, sikueleweka, nikaonekana natishia maslahi ya wakubwa na nafasi zao kwenye Chama, nikaonekana ADUI na nikapewa jina MSALITI.

Ukweli ni kwamba FEDHA ambayo leo imetajwa mara kadhaa kuwa ndio sababu kuu ya mfarakano ndani ya CHADEMA, imepata njia kutokana na Ukweli kuwa CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi ambao umekosa Vision na Mission, ndio maana wakadhani FEDHA na UMAARUFU wa mtu ni mtaji wa wao kuingia Ikulu, wakasahau misingi, dhamira, imani na kiu ya Watanzania.

CHADEMA haina tabia ya kujitafakari, haijisahihishi, na wamezoea kuishi kimazoea, wanadhani kila siku ni jumapili na kila walisemalo watanzania watalikubali tu madhari limesemwa na wao, na kwamba kila muongeaji basi anasikilizwa. SIO HIVYO...!!

Leo waongeaji wa CHADEMA na WATETEZI wakuu kwenye mitandao ni YERICKO NYERERE, A man with 0.001 IQ, Anaishi katika uongo na uzushi, mpaka kila mmoja amemmpuuza, Mwanakijiji, Chahali na WATABE wengine wa maandishi yenye adili, wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, inajivunia kuwa na YERICKO. Wasomi, watumishi, na wanataaluma wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, wanajivunia madereva bodaboda.

Moja ya sifa ya Mwerevu, ni yule ambae haumwi na nyoka mara mbili, anayejikwaa akaanguka kisha asiishie kuangalia alipoangukia bali hugeuka kwa umakini na kutazama alipojikwaa, ni nini hasa kimemuangusha..Popularity ya CHADEMA na Upinzani imeshuka na inaendelea kushuka kwa kasi, HAWAJIULIZI.

Viongozi wameacha kuchangia hoja za msingi ndani ya Vikao, wameshikwa na woga na wengine wamesusa, Mwenyekiti Mbowe ambae Mimi binafsi nilishamuita ZERO tukiwa ndani ya Kikao changu cha Mwisho nikiwa KAMANDA wa CDM, ameendelea kwenda Mrama kwa kasi ya ajabu...kila jipya analoliamua ni baya kuliko la jana..
 
Acha umbea toka lini ccm ikawa mshauri wa CHADEMA:what::banghead:ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni nikuambie kitu hii nchi ni yetu sote tunajua baya na jema kwa hiyo usipoteze pumzi kutuambia hii nyeusi wakati ni nyeupe ni m.baya jully angalizo ukiwa mnafiki ujanani uzeeni utakuwa mchawi.
Wewe hautakuwa wa Kwanza kuniona Mimi ni mnafiki, lakini pia hautakuwa wa Mwisho, wapo waliokutangulia na wapo watakaufuata baada yako.lakini HOJA yangu itabaki imara na haitabadilika kuwa CHADEMA kuna OMBWE la UONGOZI..ni hoja ambayo nimeisema na kuisimamia tangu nikiwa CHADEMA na nitaendelea kuisema na kuisimamia hata sasa..

Mimi sio katika wale ambao wanataka UPINZANI ufe kabisa, na wala sio katika wale wanaoamini kuwa salama ya CCM ni Upinzani dhaifu..mimi naamini kuwa NGUVU ya CCM, Uimara wake na UTENDAJI wake utakuwa bora zaidi kukiwepo Upinzani Madhubuti, ambao utawakumbusha CCM wanapojisahau..

Mimi ni MwanaCCM, tena sio tu mwanachama bali ni Mtumishi wa CHAMA, naamini katika CCM lakini kama nilivyotangulia kusema kuwa SIAMINI kuwa salama ya CCM ama ya TANZANIA ni kufa kwa Upinzani...siamini hivyo.
 
AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!

CHADEMA haina tabia ya kujitafakari, haijisahihishi, na wamezoea kuishi kimazoea, wanadhani kila siku ni jumapili na kila walisemalo watanzania watalikubali tu madhari limesemwa na wao, na kwamba kila muongeaji basi anasikilizwa. SIO HIVYO...!!

Hapo juu Ben Saanane tafadhali tia neno.

Leo waongeaji wa CHADEMA na WATETEZI wakuu kwenye mitandao ni YERICKO NYERERE, A man with 0.001 IQ, Anaishi katika uongo na uzushi, mpaka kila mmoja amemmpuuza, Mwanakijiji, Chahali na WATABE wengine wa maandishi yenye adili, wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, inajivunia kuwa na YERICKO. Wasomi, watumishi, na wanataaluma wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, wanajivunia madereva bodaboda.

Viongozi wameacha kuchangia hoja za msingi ndani ya Vikao, wameshikwa na woga na wengine wamesusa, Mwenyekiti Mbowe ambae Mimi binafsi nilishamuita ZERO tukiwa ndani ya Kikao changu cha Mwisho nikiwa KAMANDA wa CDM, ameendelea kwenda Mrama kwa kasi ya ajabu...kila jipya analoliamua ni baya kuliko la jana..

Kama umeamua kujizungumzia wewe fanya hivyo kwa uhuru wako.Lakini hili la kuwaunga unga watu wengine wenye masilahi zao binafsi kwenye andishi zao na ambao bila uwapo wa Chadema hawana cha kuandika haipendeze na inakuanika jinsi gani ulivyo mtu kichwani.

Baki kuandika kinachokukera au ulichokisahau CDM.
 
Last edited by a moderator:
Wewe hautakuwa wa Kwanza kuniona Mimi ni mnafiki, lakini pia hautakuwa wa Mwisho, wapo waliokutangulia na wapo watakaufuata baada yako.lakini HOJA yangu itabaki imara na haitabadilika kuwa CHADEMA kuna OMBWE la UONGOZI..ni hoja ambayo nimeisema na kuisimamia tangu nikiwa CHADEMA na nitaendelea kuisema na kuisimamia hata sasa..

Mimi sio katika wale ambao wanataka UPINZANI ufe kabisa, na wala sio katika wale wanaoamini kuwa salama ya CCM ni Upinzani dhaifu..mimi naamini kuwa NGUVU ya CCM, Uimara wake na UTENDAJI wake utakuwa bora zaidi kukiwepo Upinzani Madhubuti, ambao utawakumbusha CCM wanapojisahau..

Mimi ni MwanaCCM, tena sio tu mwanachama bali ni Mtumishi wa CHAMA, naamini katika CCM lakini kama nilivyotangulia kusema kuwa SIAMINI kuwa salama ya CCM ama ya TANZANIA ni kufa kwa Upinzani...siamini hivyo.

Jully bana ccm upo kimaslahi zaidi zaidi ya hapo miafrika ndivyo tulivyo.
 
AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!

Hapo juu Ben Saanane tafadhali tia neno.

Kama umeamua kujizungumzia wewe fanya hivyo kwa uhuru wako.Lakini hili la kuwaunga unga watu wengine wenye masilahi zao binafsi kwenye andishi zao na ambao bila uwapo wa Chadema hawana cha kuandika haipendeze na inakuanika jinsi gani ulivyo mtu kichwani.

Baki kuandika kinachokukera au ulichokisahau CDM.
BEN SAANANE..unamuita BEN aje kunijibu mimi..? tena kuijibu HOJA ya Ombwe la Uongozi ndani ya CHADEMA..? Labda nisema katika usiyoyajua. BEN ni miongoni mwa watu ambao hawaamini katika Uongozi uliokuwepo sasa ndani ya CHADEMA, nimezungumza nae mengi lakini pia tumeshirikiana kulieleza hili nikiwa ndani ya CHADEMA, ingawa mwenzangu alifanya KIUNAFIKI, alitawaliwa na woga na ubinafsi.

Na kuhusu kuwazungumzia makundi mengine, unaweza kwenda kujiridhisha kwenye tafiti mbalimbali zinazoendelea kuhusu kukubalika kwa vyama vya siasa na makundi mbalimbali ya kijamii..kisha angalia makundi hayo ya Wasomi, Wanataaluma na Watumishi wanaikubali kiasi gani CHADEMA..sio unatokwa na povu tu hapa, jiridhishe kabla haujatetea uozo.
 
Bado unaipenda chadema.......ila ccm imekupenda zaidi
 
Mkuu naihifadhi hii thread yako mpaka tarehe 27 oct baada ya matokeao kutangazwa. Hii itasaidia vijana wenye vichwa vigumu kama jiwe wawe na vichwa vyepesi kuelewa mambo.
Unamjua Muhammad Saeed Al-sahaaf...mna mioyo pacha...Hautoamini.
 
BEN SAANANE..unamuita BEN aje kunijibu mimi..? tena kuijibu HOJA ya Ombwe la Uongozi ndani ya CHADEMA..? Labda nisema katika usiyoyajua. BEN ni miongoni mwa watu ambao hawaamini katika Uongozi uliokuwepo sasa ndani ya CHADEMA, nimezungumza nae mengi lakini pia tumeshirikiana kulieleza hili nikiwa ndani ya CHADEMA, ingawa mwenzangu alifanya KIUNAFIKI, alitawaliwa na woga na ubinafsi.

Na kuhusu kuwazungumzia makundi mengine, unaweza kwenda kujiridhisha kwenye tafiti mbalimbali zinazoendelea kuhusu kukubalika kwa vyama vya siasa na makundi mbalimbali ya kijamii..kisha angalia makundi hayo ya Wasomi, Wanataaluma na Watumishi wanaikubali kiasi gani CHADEMA..sio unatokwa na povu tu hapa, jiridhishe kabla haujatetea uozo.

Vipi unamuogopa Ben Saanane -si nimemwitisha akupe facts?.Haraka ya nini na matusi ya nini?
 
KUPOTEA...hivi unajua tafsir ya neno kupotea..??
Subiri shughuli yangu utaiona BUNGENI...MTANYOOOKA tu.

mzee wa vyeo vya sadaka ndo anasepa kama uteuz ule wa madc hukuambuliwa ujue unagundu.
 
hili taifa lina HASARA huyu dada eti naye atakuwa mbunge,wa bunge lijalo
 
Back
Top Bottom