Chadema kuna mahali pana mushkeli,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN
Chadema kuna mahali pana mushkeli,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kintiku, Aug 6, 2011.
1. K
Kintiku JF-Expert Member
#1
Aug 6, 2011
Joined: Feb 3, 2011
Messages: 611
Likes Received: 72
Trophy Points: 45
Wananchi wengi wamekosa matumani na CCM na serikali yao..........wanahitaji mtu wa kuwapa matumaini mapya, japo haitaondoa shida walizo nazo lakini wahitaji mtu wa kuwapa matumaini katika hali ya kukata tamaa, wanahitaji mtu wa kuwasemea kuwa wamechoka na uongo wa watawala, wananchi wanahitaji mtu wa kuwaongoza namna watakavyoondokana na hali hii,
Wananchi wanaona yanayotokea, wanahitaji mtu wa ''kuwapasha'' watawala kwa niaba yao. Lakini inaonyesha CHADEMA wanashindwa kufanya kazi hiyo. Wamekuwa busy na mamabo ya madiwani wa Arusha as if hiyo ndio kazi yao. Kuongea sana bungeni sio tija wananchi wanataka zaidi ya hapo, wanataka CDM waongoze mapambano.
Matukio ya Jairo na UDA yalitakiwa yatolewa kauli kali na ufafanuzi wa kutosha kutoka CDM, lakini hakuna kitu wapo wapo tu. CDM wanahitaji kiongozi ambaye ni radical sana kulingana na hali ya nchi ilivyo sasa. Waache kufanya siasa za kigoigoi, waamke na kutekeleza kazi yao. Kila unapotokea utata au utendaji mbaya lazima CDM waseme ili wananchi wajue kuwa wao wako tofauti.
Nasema hivi kwa vile wananchi wengi husema hawa wapinzani na wao ni kama CCM wanataka kula tu. Kuepusha maneno hayo lazima CDM ifanye tofauti iwe na ukali zaidi sio kutoa kauli rahisi rahis tu.
Nadhani baadhi ya viongozi wa juu sio radical sana wanataka kutunza status quo..........................ni maoni tu
2. Mlangaja
Mlangaja JF-Expert Member
#2
Aug 6, 2011
Joined: Nov 2, 2010
Messages: 541
Likes Received: 28
Trophy Points: 45
Umenena vyema. Nilitegemea CDM wangetoa tamko kuhusu Jairo lakini kimya. Hii inakera sana. Hebu amkeni bwana. Sisi tupo tayari kuwapa nchi sasa mkiendelea kuongoza kigoigoi namna hii kuipata nchi ni kazi, habu acheni kujikita katika mambo ambayo yanapaswa kufanywa na kundi dogo. Jipangeni tuonesheni njia. Tambueni mahitaji ya wananchi. Ninyi ndo mnaotamwa sasa, msituangushe.
3. Sir R
Sir R JF-Expert Member
#3
Aug 6, 2011
Joined: Oct 23, 2009
Messages: 2,177
Likes Received: 2
Trophy Points: 135
Chadema haiwezi kuwalazimisha watu ambao hawako tayari kuleta mabadiliko. Watuu wengi wanataka kupewa Tshirt badala ya haki. ndio maana wako tayari kuipigia kura CCM kwa kuwa inawapa vitu badala ya haki zao.
4. K
Kintiku JF-Expert Member
#4
Aug 8, 2011
Joined: Feb 3, 2011
Messages: 611
Likes Received: 72
Trophy Points: 45
Kazi ya chama cha siasa ni kushawishi wananchi wakiunge mkono, sio rahisi wananchi wakaunga mkono chama bila chama kushawishi chama. Naona kama CDM kwa sasa wanapata mserereko wa hali ngumu ya maisha hivyo wanaichukia CCM
5. jouneGwalu
jouneGwalu JF-Expert Member
#5
Aug 10, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 2,680
Likes Received: 62
Trophy Points: 145
Hili nalo linakuwa na tatizo katika namna ambapo kila mtu anataka kuwa mchambuzi wa masuala ya siasa,
Mengine ni muhimu mtu ukae na utafakari kwa uchambuzi binafsi.... badala ya kudhani ni sahihi kuleta kila kitu jamvini.
Kwa mfano kwa wewe kuamini kuwa kazi ya chama cha siasa kazi yake ni kutoa matamko tu, ni upotofu wa kiuchambuzi na mapungufu katika kuangalia mambo ya kisiasa.
6. m
mechard Rwizile JF-Expert Member
#6
Sep 21, 2011
Joined: Sep 21, 2011
Messages: 945
Likes Received: 382
Trophy Points: 80
Hakika CDM inahitaji kuonyesha njia. Yapo mambo ambayo hata wakisema sana hayataleta tofauti kwa ujumla wake. Suala la Jairo kwa mfano, ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni aliyemuuliza waziri mkuu kuhusu kurudishwa kwake kazini. Jibu la swali hilo ndilo lingepelekea muendelezo au kutendelea. Waziri Mkuu alijibu, Rais amechukua hatua ya kumsimamisha Jairo ilikuruhusu tume teule ya Bunge kufanya uchunguzi wake. Na kweli Jairo amesimamishwa, na tume imeanza kazi yake! CDM ifanye nini katika mazingira kama haya? Tusuburi na tuone matokeo ya tume.
Jambo ambalo nadhani sasa ni wakati wake kulijadili ni kuhusu CDM, madiwani na wabunge wake wanatenda ilivyostahili? Zile sera zilizouzwa wakati wa uchaguzi zinafanyiwa kazi? Kwa mfano; moja ya sera za CHADEMA wakati wa uchaguzi ilikuwa elimu ya sekondari bure. Je, kwenye Halmashuri ambako CHADEMA ilishinda, sera hii inatekelezwa kwa kiwango gani? Kama haitelezwi kunatatizo gani la kitendaji? Tuelezane ni Halmashauri ngapi zinaongozwa na CDM na ni ngapi zianitekeleza sera hii kwa ukamilifu? Zilizokwama, zimekwamia wapi?
Ni wakati wakutafuta mfumo, utakao wezesha ndani ya kata ambako CDM ilishinda, sera zake, kwa mfano huo huo wa elimu ya sekondari bure inatekelezwaje? Haitoshi kusema " kwa kuwa hatukuunda serikali ya Halmashauri hatukuwa na uwezo wa kutekeleza sera hiyo". Kwa maana ulitekelezaje sera zilizokufanya uchaguliwe katika kata husika ndilo litakalokuwa swali la wapiga kura katika uchaguzi wa ujao.
Ni lazima katika kata ambazo CDM ilishinda madiwani wake wasihitajike kufanya kazi sana katika uchaguzi wa mwaka 2015. Kata hizo ziwe chachu kwa kata za jirani kwa pande nne za dunia Kata zote za mashariki, kasikazini, kusini na magharibi. Na kwa majimbo ya ubunge hivyo hivyo.
Ni lazima tuanze sasa na si baadae.
7. dedam
dedam JF-Expert Member
#7
Sep 21, 2011
Joined: Jan 5, 2011
Messages: 846
Likes Received: 16
Trophy Points: 35
manispaa ya moshi madiwani wa cdm walitaka elimu Ded akawagomea akipata sapoti na wanamagamba wenzie.uwezekano wa kutoa elimu bure upo ila baadhi ya watendaji wa serikali wanakwamisha zoezi hili kwa makusudi
8. m
mechard Rwizile JF-Expert Member
#8
Sep 21, 2011
Joined: Sep 21, 2011
Messages: 945
Likes Received: 382
Trophy Points: 80
Suala, kama hili, ndilo ambalo tunge waushauri uongozi wa CDM kuchukua hatua. Mikutano ya hadhara ya kuishitaki serikali kwa wananchi inahitajika. Wananchi waelezwe nia ya madiwani na mbunge wa CDM kutoa elimu bure imekwamishwa na serikali ya CCM, watoe ushahidi wao. Kila diwani anatakiwa kufanya hivyo kwa wanachi wake. Litolewe azimio kuwa bajeti ijayo haitapitishwa na baraza la madiwani kama haitakuwa na bajeti ya elimu ya sekondari kwa wanfunzi wote wa shule za serikali. Haki hiyo wanayo ya kupinga bajeti na hakuna ambaye anaweza kuruhusu matumizi bila idhini ya baraza la madiwani.
9. m
mechard Rwizile JF-Expert Member
#9
Sep 21, 2011
Joined: Sep 21, 2011
Messages: 945
Likes Received: 382
Trophy Points: 80
Loading...