CHADEMA kuchambua sekta ya elimu nchini

CHADEMA kuchambua sekta ya elimu nchini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinatarajia kuandaa mkutano na waandishi wa habari ili kuchambua hali ya sasa ya elimu ya juu nchini

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho leo hii, Halima Mdee, mbunge wa Kawe, amesema kuwa chama chake kupitia kwa Suzan Lyimo, Waziri Kivuli wa Elimu, kitatoa hali halisi ya elimu ya juu ilivyo kwa sasa.

“Serikali inatumia visingizio kubagua Watanzania, na sisi hili suala hili tutalikemea, tutaendelea kulikemea na tutaanda mkutano kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina wa elimu.

Hata hivyo, Mdee amesema siku na tarehe ya kufanya mkutano huo haijapangwa na kwamba dhamira ya kufanya uchambuzi huo wanayo kama chama
 
Si ajabu wakasema elimu wakati wa utawala wa Kikwete ilikuwa bora kuliko elimu chini ya utawala wa Magufuli.
 
Unategemea watasemaje iwapo mpaka sasa no increment of salary!
 
Enzi za Kikwete mlikuwa mnapata sana matukio ya kuwapa promo ili siku hizi matukio hakuna. Shida ya siasa za kiki ni kuwa mnakosa ubunifu wa hoja zenu wenyewe kama chama ili muweze kuzisimamia. Mlisema Kikwete dikteta sasa hivi mnasema ndie rais aliyekuwa bora, milisema Kikwete dhaifu, sasa hivi mnasema ndiye aliyekuwa bora, mlihubiri ufisadi sasa neon ufisadi limekuwa msamiati midomoni mwenu, mlisema Lowassa fisadi sasa hivi ndiye think tank wenu, mlisema Sumaye fisadi sasa hivi ndiye mshauri wenu, mlihubiri demokrasia na ukomo wa madaraka lakini nyie mkawa wa kwanza kuondoa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba yenu, mlikosoa siasa za lugha ya matusi na maneno ya kuudhi lakini sasa hivi nyie ndio vinara wa lugha za matusi na maneno ya kuudhi. Kiujumla mmekuwa chama kisichokuwa na dira wala mwelekeo maalum. Mnabadilika kuliko hata kinyonga.
 
Si ajabu wakasema elimu wakati wa utawala wa Kikwete ilikuwa bora kuliko elimu chini ya utawala wa Magufuli.
It is good premature premise and it is very obvious.

Kipindi kile cha jamaa mikopo ilikuwa ipo kwa yeyote aendae chuo, watu waliwekeza sababu ukimaliza ajira zipo, madaraja ya walimu plus madai hadi walimu hewa hata wenye vyeti feki wote walilipwa stahiki zao, elimu iliajili wengi ukilinganisha na leo na ilikuwa valuable goods ukilinganisha na sasa ambapo hata hawa wenye genuine education hawana rikizo, daraja wala increment wala ajira wala nini?

Elimu isio na mahusiano na mnyororo wa thamani ni sawa na ngoma za kula daku tu.

Wapunguze mauongo jazz band pamoja na kuwepo na maprofeseri wanye majina makubwa hata increments tu zimegoma.
 
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho leo hii, Halima Mdee, mbunge wa Kawe, amesema kuwa chama chake kupitia kwa Suzan Lyimo, Waziri Kivuli wa Elimu, kitatoa hali halisi ya elimu ya juu ilivyo kwa sasa.
Huyu Suzane Lyimo alikuwa bingwa wa kuuza vyumba kwa wanafunzi UDSM.
 
Si ajabu wakasema elimu wakati wa utawala wa Kikwete ilikuwa bora kuliko elimu chini ya utawala wa Magufuli.
Ndo ukweli. Vijana waliosoma kada muhimu kama udaktari na ualimu wa science na maengineers walipata mikopo bila kubaguliwa.
 
Msemaji mkuu kuhusu elimu ya juu atakuwa Mwenyekiti Mbowe akisaidina na Kubenea(Elimu ya hapa na pale), wakati mwingine bora chama kikakaa kimya hii mikutano mara kutetea mimba,mara Sumaye kumtambulisha Sepetu,inazidi kuonyesha mlivyopoteza mwelekeo,by the way Halima Mdee ataleta lini mrejesho wa bei ya mafuta kupanda mara mbili maana ni August?,.Kukaa kimya nayo ni busara.
 
It is good premature premise and it is very obvious.

Kipindi kile cha jamaa mikopo ilikuwa ipo kwa yeyote aendae chuo, watu waliwekeza sababu ukimaliza ajira zipo, madaraja ya walimu plus madai hadi walimu hewa hata wenye vyeti feki wote walilipwa stahiki zao, elimu iliajili wengi ukilinganisha na leo na ilikuwa valuable goods ukilinganisha na sasa ambapo hata hawa wenye genuine education hawana rikizo, daraja wala increment wala ajira wala nini?

Elimu isio na mahusiano na mnyororo wa thamani ni sawa na ngoma za kula daku tu.

Wapunguze mauongo jazz band pamoja na kuwepo na maprofeseri wanye majina makubwa hata increments tu zimegoma.
Mkuu kama siyo kuchanganya R na L, una-point sana.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatarajia kuandaa mkutano na waandishi wa habari ili kuchambua hali ya sasa ya elimu ya juu nchini

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho leo hii, Halima Mdee, mbunge wa Kawe, amesema kuwa chama chake kupitia kwa Suzan Lyimo, Waziri Kivuli wa Elimu, kitatoa hali halisi ya elimu ya juu ilivyo kwa sasa.

“Serikali inatumia visingizio kubagua Watanzania, na sisi hili suala hili tutalikemea, tutaendelea kulikemea na tutaanda mkutano kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina wa elimu.

Hata hivyo, Mdee amesema siku na tarehe ya kufanya mkutano huo haijapangwa na kwamba dhamira ya kufanya uchambuzi huo wanayo kama chama
Opportunists tu hawa na wachumia tumbo.Wanachotaka kufanya ni kutafuta kick na kutaka kuhalalisha uwepo wao.Hata hivyo katika mazingira ya sasa they are obsolete
and irrelevant.
 
Back
Top Bottom