Ndugu Wanabodi,
Nimefuatilia kwa muda mrefu siasa za CHADEMA pamoja an Washirika wao wa NCCR, CUF na NLD nimegundua kuwa kila kitu katika chama hichi kikubwa cha upinzani nchini ni MKOPO.
Ni mkopo kwa sababu zifuatazo:
1. Mgombea Urais wao Bw. Lowassa amekopwa kutoka CCM
2. Mgombea Mwenza wa Urais - Bw. Duni ( BABU) amekopwa kutoka CUF
3. Wafanya kampeni - Masha, Chizii, Mungai, Yule mzee toka Singida, Mgeja - wamekopwa toka CCM
4. Sera ha kuanzisha viwanda, elimu ya bure ya msingi (isipokuwa ya chuokikuu) imekopwa toka CCM
5. Sera ya Majimbo - imekopwa toka Marekani
6. Fedha za Kampeni 2015 - zimekopwa kutoka kwa EL na kwa baadhi ya Wafanyabiashara toka Kaskazini
7. Viongozi wengi wa CDM ASILI wamekopwa toka ukanda mmoja wa nchi
Maswali yangu ya msingi hapa ni:
1. Je, CHADEMA hawakujiandaa kugombea Urais mwaka huu au hiyo ndo staili ya maandalizi yao?
2. Kama EL hata shinda uchaguzi Kama amabavyo dalili zinavyoonesha, CDM watamrejeshea pesa zake?
3. Je, Kama EL hatoshinda uchaguzi atarejea CCM kama inavyosemekana?
Naomba tuchangie bila matusi. Najua vijana wa UKAWA wana mafunzo mazuri ya matusi.