CHADEMA Kaskazini: Tuna ushahidi madiwani wanaohamia CCM wameshawishiwa kwa fedha,ajira

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Gulugwa.jpg
gulugwa2.jpg

Katibu wa Kanda ya Kaskazini Mhe.Amani Golugwa, leo Agosti 1 amekutana na wajumbe wa Kamati maalumu za kazi za Kanda ya Kaskazini. Mhe.Katibu amezungumza na kamati hizo sambamba na kupanga mipango muhimu ya utendaji wa kamati hizo. Taarifa maalumu kuhusu viongozi wa kamati hizo na wajumbe wake itatolewa mapema wiki hii.

Aidha, katika kikao kingine siku ya leo Katibu wa Kanda ya Kaskazini amekutana na Kamati Tendaji ya Baraza la vi...jana BAVICHA Jimbo la Arusha kwa lengo la kuimarisha Baraza hilo liimarike zaidi, Mhe.Katibu amelitaka Baraza hilo kuwaunganisha vijana wenzao kadri wawezavyo.

Katika kikao hicho cha Kamati ya utendaji ya Bavicha Jimbo la Arusha Mhe. Golugwa aliongozana na Katibu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Elisa Mungure ambaye kwenye hotuba yake aliwataka vijana kuwa na nidhamu na Katibu wa baraza hilo mkoa wa Arusha mhe.Jenipher Mwasha.

Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo la Arusha Mjini mhe. Innocent Kisanyage kwa niaba ya Baraza na vijana kwa ujumla aliomba viongozi wa chama kuwathamini vijana na kufanya kazi kwa ukaribu na vijana.

Uongozi wa chama mkoa wa Arusha, umeahidi kila baada ya miezi miwili itakuwa ukifanya vikao vya mashauriano na kamati tendaji za wilaya kwa lengo la kuwa karibu na viongozi wa vijana.
 

Attachments

  • gulugwa3.jpg
    gulugwa3.jpg
    8.9 KB · Views: 19
Back
Top Bottom