Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
Katika miaka ya 2010-2013 ni wazi kuwa CHADEMA imezidi kupata umaarufu na kukubalika zaidi kwa raia wa Tanzania. Hii imetokana na juhudi kubwa ambazo zimefanywa na wanachadema. Pamoja na propaganda mbalimbali kama udini,ukabila,ukanda na sasa ugaidi duru za kisiasa za ndani na nje ya nchi bado zinaiweka chadema katika nafasi kubwa zaidi kama chama Kikuu cha Upinzani.
Katika nyakati za kupigania uhuru historia inatueleza kuwa TANU ilikumbana na na vikwazo lukuki kubwa zaidi ni viongozi wake kubambikwa kesi za uchochezi na kutotii sheria za kikoloni, mmojawapo akiwamo Nyerere lakini mapambano yaliendelea. TANU iliendelea na harakati zake za kuunganisha watanzania na kupinga vita utawala wa kikoloni mpaka walipofika mahali na kuona sasa nchi hii inapaswa kutawaliwa na wazalendo.
Ni katika spirit hiyo ambapo CHADEMA inapaswa kuendeleza, kwa hali ilivyo sasa ni wazi kuwa pamoja na tuhuma zote hizo hakuna hata ngome moja ya chadema ambayo imetetereka, hii ina maana kuwa wananchi wapo nyuma na wanaunga mkono juhudi zenu. Ni vema ikafahamika kuwa CCM imepoteza uwezo wake wa kupambana kisiasa na sasa inataka kuua upinzania ili ishinde kirahisi,
Ni wito wangu kwa CHADEMA kuwa kazi imekwisha, kilichobaki ni kujiimarisha ndani na nje ya chama na kuendelea kutetea wananchi