Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Nimekuwa nikiliandika hili mara kadhaa na wakati fulani kuzua majibishano ya kimantiki baina yangu na viongozi wa CHADEMA. Nakumbuka kabla Dr Slaa hajajiengua kwenye nafasi yake ya Katibu Mkuu, niliwahi kulumbana humu kwa hoja na mwisho wa siku niligeuka kuwa mshindi.
Nilishasema toka mwanzo kuwa Jengo la Makao Makuu ya CHADEMA ni mali binafsi ya watu walio karibu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Nilieleza wakati ule kuwa CHADEMA hupoteza zaidi ya shilingi milioni 100 kila Mwezi kama gharama ya pango la jengo hilo. Haya anafahamu vema Freeman Mbowe, Dr Slaa na hata Vicent Mashinji. Naamini siku Dr Slaa akiamua kupasua jipu hili kuna watu watatafuta pa kujificha na wasipaone.
Wanaosema kuwa CHADEMA wanamiliki Jengo la Makao Makuu ni mwendelezo wa propaganda zile zile ili ukweli usifahamike. Umiliki wa jengo hilo ni Siri Kuu ya Chama na itakuja kufichuka pindi Freeman Mbowe atakapotoka madarakani. Nendeni kwa Kamishna wa Ardhi ama Ofisi ya Ardhi Kinondoni mkaulize kama kuna nyaraka yoyote inayoonesha CHADEMA wanamiliki Jengo Mtaa wa Ufipa Kinondoni. Hakuna.
Nenda kwa Kamishna wa Ardhi kaulize kama kuna nakala ya hati ya umiliki wa Ardhi ya CHADEMA Mtaa wa Ufipa Kinondoni. Hakuna. Huu ni ulaghai wa hali ya juu sana. Na kama wanashindwa hata kuweka wazi juu ya mali wanazomiliki, hakika hiki chama hakifai hata kuongoza kitongoji. Yaani wanajifisidi wenyewe kwa fedha za ruzuku. Imagine, zaidi ya milioni 100 zinatoweka kila mwezi kulipia jengo ambalo wanadai ni lao. Laana hii itawahukumu.