Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
Jurgen Klopp na Mbowe walipaswa kuona kuwa haya yangetokea.
Matatizo ya Liverpool msimu wa baridi ni yaleyale kama yalivyo matatizo ya Chadema wakati wa uchaguzi.
Msimu wa baridi kwa Liverpool umekuwa na kawaida ya kukatisha tamaa baada ya matumaini makubwa ya msimu wa joto. Vivyo hivyo kwa Chadema, wakati wa matokeo ya uchaguzi umekuwa wa kukatisha tamaa baada ya matumaini makubwa ya kipindi cha kampeni.
Matokeo ya kusuasua kwa Liverpool ndani ya mechi 13 zilizoisha yanatia wasiwasi kwamba kuna uwezekano wa kumaliza msimu nje ya matarajio.
Maamuzi yatakayochukuliwa na wote, Liverpool na CHADEMA siku za usoni yanaweza kuleta picha mpya ya matumaini.
MPIRA NA SIASA YOTE NI MICHEZO INAYOTEGEMEA MATOKEO.
Msimu ulioisha katika mechi 13 baada ya Desemba, Liverpool ilishinda mechi 5 ika droo 4 na kupoteza 4.
Katika kipindi kama kile, mwaka mmoja baadae, Liverpool imeshinda mechi 5 ika droo 4 na kupoteza 3.
Kama Southampton akishinda Anfield, basi mtiririko wa matokeo katika msimu ulioisha na msimu huu, katika kipindi
Kinachofanana utakuwa uleule ( identical)
Kwenye uchaguzi mdogo na kwenyewe Chadema imerudia matokeo yaleyale iliyokuwa nayo awali.
Jurgen Klopp ana kikosi kidogo kama tu alivyokikuta, wakati Mbowe katika awamu hii anaandamwa na njama za kumpunguzia kikosi. Lema ,Lijuakali na makamanda wengine wamemewekwa jela, Ben hajulikani alipo na njama kibao za kudhoofisha kikosi cha Mbowe zinaendelea kufanya kazi.
Jurgen Klopp kama tu Mbowe, wamevitumia vikosi vyao kisawasawa kiasi kwamba vikosi hivi vinahitaji sura mpya ili kuleta mbinu na matumaini mapya.
Liverpool ilipaswa kusajili Januari kama ambavyo Chadema ilipaswa kuhakikisha makamanda wote wanaandamwa na njama za CCM wanakuwa huru na milango zaidi inafunguliwa kwaajili ya makamanda wapya kukipigania chama.
sadio Mane amerudi nyumbani, Senegal, kuichezea timu yake ya taifa katika kombe la mataifa ya Africa.
Kuto kuwepo kwa Mane ni pengo lisilofaa kupuuzwa, kama tu kutokuwepo kwa bunge live, katazo la kufanya siasa, makamanda kuwekwa jela na wengine kupambana na mbinu chafu za dola kila uchao. Haya kwa namna moja au nyengine yanaiathiri Chadema.
Adam Lallana anapwaya katika nafasi yake mpya kuziba pengo la Mane.
Leroy Fer wa Swansea city aliweza kuyatumia madhaifu haya vizuri katika ushindi wao wa 3 - 2 dhidi ya Liverpool.
Dr. Mashinji sio Dr. Slaa na tofauti zao kiutendaji zisipuuzwe.
Wakati msimu ulipoanza, kikosi cha Klopp kilikuwa hakishikiki, na matumaini yakawa makubwa mpaka kufunika
uwezo wa kuona changamoto za mbele.
Ni kweli uchaguzi mkuu uliopita ulileta matumaini makubwa kwa Chadema ila hauondoi ukweli kwamba upande wa pili nao haujalala.
Magufuli ni mwanasiasa dhaifu ila hatutamshinda bila katiba mpya na mbinu mpya.
Ni wakati wa kuanza kuwapima watendaji wa chama kwa matokeo ya chaguzi.
CHADEMA NEEDS A VERY HARD LOOK ON THE RESULTS OF THE RECENT BY-ELECTION.
Aluta Continua
victoria ascerta