CHADEMA itabaki kuwa CHADEMA tu

Baada ya Sumaye kumwaga manyanga nimeona nijikumbushe yanayoikumba Chadema kwa kukopi kupande changu hiki.
 
Kama una charisma ya kutosha muda huu si sahihi Mbowe kuondoka!

Wengine hatujui watareact vipi wakiguswa Mali zao, maisha yao, ndugu zao etc, Mbowe kaguswa vyote hivyo na kafauru.

Hiki si kipindi cha majaribio japo naamini kuna watu wenye Uwezo kama au kuliko Mbowe ila kwa utawala huu, aslani tusijaribu.

Tumeona watu wanavyotishiwa na kuyield, kuuwawa au kuteswa na kunyong'onyea twende na Mbowe then huyu akitoka naye atoke, ila, team ya uongozi ya Mbowe inabidi ibadilike ili chama kizidi kusonga mbele!

CHADEMA ina nguvu zaidi ya CCM ukizingatia idadi ya wana chama lakini kinakuwa weak kwa kutokuwa na dola tuu! Na CCM wanajua hilo na wametumia mbinu zote kupenetrate wameshindwa!

Systemic change yeyote itaiingiza CHADEMA madarakani hapo ndipo watu watazidi kuishangaa charisma na Mwalimu Nyerere maana alitabiri tayari kuwa after CCM CHADEMA watachukua nchi!!
 
Chadema imekwisha mwaka kesho 2020 huenda hata mbunge mmoja wakakosa
 
Aisee CDM haiingiliki nimeamini - CDM ni imani...huna imani hukai humo yaani utaondoka mwenyewe tena mchana mchana kweupe na magodoro yako kichwani !!
 
kaka ille safu ya mashambulizi inarudi ile ile....mtaa wa saba salaam kwenu... mkishindwa hoja msikimbilie kuwaita police..
 
Chadema imekwisha mwaka kesho 2020 huenda hata mbunge mmoja wakakosa
Kwa uchafuzi wanaweza kukosa ila kwa uchaguzi Hata zaidi ya 70% watachaguliwa! Kwa akili yako unafikiri kwanini huyo bwana anaogopa uchaguzi?

Lubuva ilikuwa 10m vs 4m fikiri kwa kina utaelewa!
 

Moments kama.hizi zinaleta nafasi ya kujitafakari. Sio vizuri kuzibeza
 

Umetoa hoja nzuri na ya msingi sana. Mimi naomba kuchangia kwenye hili moja tu;

Kwamba, CHADEMA na vyama vilivyo nje ya dola kwa ujumla wanapaswa kuwa na watu (wanachama) watiifu ktk taasisi nyeti za umma (serikali) hususani TISS, JWTZ, POLISI na Mahakama...

Yes, nakubaliana na wewe 100% na ndiyo njia ya pekee kuwaondoa CCM madarakani....

SWALI NI; How?

Moja ya zana (tools & weapons) muhimu kuzitumia kufanikisha hili ni;

FEDHA

- Hii ndiyo silaha wanayotumia watawala wengi na vyama vyao ktk nchi za ki-Africa na dunia ya tatu kuhakikisha wanabaki madarakani....

- Wanahakikisha kuwa vyama vya upinzani vinakuwa dhaifu (weak) kiuchumi (kifedha) ili washindwe kujiimarisha na kuwa na ushawishi ktk jamii/watu...

- Na ndiyo maana ya hizi harakati zinazoendelea sasa za kununua wabunge, madiwani na wanachama wengine maarufu wa vyama hivi...

- Tukumbuke vyanzo vikuu vya fedha ndani ya vyama hivi ni RUZUKU toka serikalini na MICHANGO ya wanachama waaminifu....

- Binafsi niwapongeze CHADEMA kwani mpaka sasa kina umri wa takribani miaka 28 na graph yake ya ukuaji, inapanda tu pamoja na kupitia misukosuko mikubwa mara zote ktk chaguzi zote chini ya mfumo wa vyama vingi....

- Hata mwaka huu, wanaodhani vinginevyo, wanajidanganya. Kuna kila dalili na sababu kuwa, CHADEMA na UPINZANI kwa ujumla watazoa viti vingi sana kuanzia Udiwani hadi Ubunge....

- Na kwenye Urais, CCM wakae chonjo kwani pamoja na kuwa mazingira ya uchaguzi kwa akili na macho ya kibinadamu yanawapendelea (favour) wao, lakini lipo kosa watalifanya na ndiyo utakuwa mwisho wao...!!

SASA, KWANINI FEDHA? WATATOA WAPI FEDHA AMBAYO NDIYO POWER KATIKA SIASA?

- Ni rahisi tu kujua kuwa, FEDHA ndiyo inayowafanya TISS, JWTZ, POLISI na MAHAKAMA (majaji & mahakimu) kuwa royal kwa CCM...

- You want them to be raoyal to you, overtake what is being provided to them by your opponent...!!

- Kwa taarifa ya wote wasiojua, ni kuwa, moja ya kada za umma zenye upendeleo maalumu "kimaslahi na marupurupu" ya wazi kisheria na ya kificho ni hizi tajwa...

- Hii siyo kwa bahati mbaya. Ni kwa sababu moja tu, that is, "to maintain their royalty", kwa mtawala aliyepo madarakani - CCM..!!

NOW, WHAT SHOULD THEY DO?

1. Defenetely, hawana fedha. They are weak economically kama taasisi. Wanachoweza kufanya ni aidha kupata economic assistance toka nje wakati huohuo wawe na uwezo wa kuepa sheria za kifedha za nchi kwa sbb kwa utaratibu wa kawaida, hawawezi kukubaliwa kupokea fedha toka nje...!!

2. Kuitumia kikweli kweli slogan ya " PEOPLE'S POWER" ama kwa kiswahili "NGUVU YA UMMA" ili ku - organize "civil disobedience" dhidi ya utawala wa serikali wasiyoitaka. Sababu za kuwaambia watu, wakubaliane nazo na kisha wawaunge mkono lazima ziwe very CLEAR and GENUINE na kamwe zisiwe za kufikirika tu.....!

Lakini, ili hii ifanye kazi kwa ufasaha pasipo kuleta madhara (casualities), tunarudi palepale, kwamba, kuna ulazima ingalau wawe na ushawishi wa kiwango fulani kwenye vyombo hivi kama ikivyotokea Tunisia, Libya na Egypt...!

Huko ktk nchi hizi, ilifika mahali POLISI na jeshi wakawa upande wa umma. Wakakataa kuua watu....!

MUHIMU:

- Lazima tukubaliane kwa dhati kabisa kuwa, mpaka sasa utawala huu chini ya CCM ulishafeli kukidhi marajio ya wananchi kiuchumi na kijamii na kwa mantiki hii umeshajitegenezea mazingira yote ya kuondolewa madarakani...

- TISS, JWTZ, POLISI na MAHAKAMA wote wanalijua hili kwa ukamilifu wake. Lakini, kwa kuwa wanapata kila wanchohitaji kwa ajili ya maisha yao na familia zao, watakuwa watiifu tu kwa sbb hiyo na siyo kitu kingine..!!

- Vyama vilivyo nje ya mfumo wa serikali (upinzani) wakitumia fursa hii kwa usahihi na kwa umakini, wanaweza kuangusha mbuyu kwa kuusukuma kwa mikono tu bila kutumia greda....!!
 
Hata cuf imebaki kua cufWala msiwaze chadema mtabaki kua chadema
 
CCM wanafikiri watatawala nchi milele...kwa kuanza tunaanza na Tume huru kwanza watake wasitake.
 

Huna hoja. Huijui Chadema. Uko upande wa pili. Huwezi kuwa objective.
 
leta hoja yako acha kuzungukazunguka?? Unazingua tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…