CHADEMA isitishe maandamano

Mkuu Ngongo, asante kwa hii!, kuna watu humu tumekuwa tunakutana kwenye threads mbali mbali na kupitia michango yao humu, unajikuta unawafahamu wamesimamia wapi!, kwa jinsi nilivyokufahamu Mkuu Ngongo, nilidhani nakufahamu, kumbumbe nilikuwa sikufahamu, ila kwa uzi huu, leo ndio nimekufahamu!, hili kundi la tusio na vyama humu jukwaani ni kundi dogo lenye wachache ila ndio ndio wawakilishi wa Watanzania walio wengi ambao hawana vyama ambao mwisho wa siku wao ndio wahanga wakuu wa matokeo ya hizi harakati za vyama!.

Hongera sana Mkuu Ngongo kwa kusimama na kuhesabiwa!.

Asante.

Pasco
 
Acha waandamane siku nyingi zimepita bila kusikia vurugu na vifo; vurugu ndio mtaji wa Chadema
 

Mkuu JokaKuu Umegusia jambo la msingi sana,kwamba wa kulaumiwa ni watawala...lakini inajulikana kuwa watawala wameyafanya haya yote kwa makusudi kabisa ndio maana katika kesi zote hizo hakuna aliyewajibishwa....Hakuna polisi aliyechukuliwa hatua kwa mauaji...wala hakuna mtuhumiwa yeyote walau amedhibitiwa....

Lakini Ngongo wote tukiwa "well wishers" hasa kwa maisha ya watu waliopotea tunatakiwa tufikiri namna bora zaidi hata ya kuwashauri CHADEMA namna ya ku deal na hizo cases....Kwenda mahakamani kwangu mimi inaweza isiwe very good option...Mahakama haziko huru....maamuzi ya kesi yanaweza kufanywa kisiasa zaidi......

Umetumia ishu ya kunywa chai ikulu kama kitu ambacho chadema wasingefanya.....walau naweza kukubaliana na wewe ukiwa na maana kwamba hawa wawe adui kabisa na wasisalimiane....lakini je...hiyo ndio justice kwa waliofiwa?

Mimi nadhani CHADEMA wangeenda mahakamani kudai rulling au ufafanuzi wa kisheria kuhusu mamlaka ya Jeshi la Polisi katika ishu ya maandamano.........je ni kutoa kibali au ni kupewa taarifa tu?
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hilo swala la Bunge la katiba ni ishu ambayo hutakiwi kujidanganya kuwa analofanya Sitta hana maelekezo ya Kikwete....Analofanya sitta ndiolo maelekezo ya kikwete na ccm na serikali yao...Kile kikao cha kikwete na Ukawa ni kwamba kikwete amewapiga chenga ya Mwili UKAWA....Kikao kile hakina mamlaka ya kutoa maamuzi "enforceable" kisheria.....Ni sawa na kigenge cha kahawa tu
 
CCM isitishe bunge la katiba. Vurugu zote chanzo ni matumizi mabaya ya madaraka na.fedha za walipa kodi. Kwa nini watu wafungiwe biashara kwa kutokulipa kodi halafu wengine watumbue hela kidogo inayopatikana kwa starehe zao? Kwa kuwa walioko bungeni ni wanachama wa CCM ni kwa nini hawalipwi na chama chao?
 

Kila roho itaonja mauti, sasa kama unaogopa kufa ili ubaki ukinyanyaswa, hiyo ni habari nyingine. Watu wanaona bora wafe ghafla kuliko manyanyaso wanayoyapata hapa duniani dhidi ya Chama tawala. hakuna dhambi kubwa kama Uoga.
 
Ni kweli hoja zako zinaweza kuwa na mantiki lakini zimekosa ujasiri, je ni kweli hujaona watoto ambao wazazi wao wapo lakini bado wanakosa hayo yote??? Usiwe wa kukata tamaa kwani hata wale waliouwawa maumau ndio kwanza sasa wanalipwa nina hakika chini ya chadema wafu hawa wataheshimika kam mashujaa na nina imani hata mbinguni pia. Maisha yalipofika ni ya kujitolea na kujitoa tukiwa wachoyo kwa kuipeleka ubinafsi mbele hatuisaidii hii nchi na kama ndivyo basi mtu wa kwanza kufanya hivyo angekuwa Mbowe ambae ana kila haki ya kutumbua utajiri wake na kutia timu na mafisadi la kini leo kwa zaidi ya miaka 20 anavaa kombati akiacha suti zake za ghali zikiharibika na kufubaa kabatini,. Ukweli ni kwamba wewe utakuwa mbinafsi kwa kuona tu afueni ya maisha yako, lakini maisha kwa watu wengi sana sasa hakuna tufauti na kifo, wakati kifo na maisha havina tofauti watu wanatakiwa kuchukua hatua, ndio maana wengine badala ya kusubiri kifo nyumbani wanaona ni bora kufanya hata wizi ili pengine atatoka!!!!! Chukua Hatua Mkuu!! Nchi hii sasa imeshaharibika mtu anauwawa kwa kuiba simu pengine akamlipie ada mwanae ambae amefukuzwa shule lakini wale wa EPA na fedha za Uswiss wanatandikiwa mazuria mekundu kwa heshima kubwa. Hebu ndugu yangu fuatilia kwa makini magazeti kila siku ipo ripoti mpya ya wizi wa fedha za umma, lakini magereza yamejaa wezi wa kuku na simu. Wizi wa sasa hivi ni wa hand to mouth...... hii inadhihirisha ukata na ukali wa maisha. Unakuta jamaa wamekuja iba lakini kabla wanaanza na kutafuta chakula wale ndio waibe.........???????????!!!!!!!!! Thinka about this, think twice

 

Kwanini mnadhani maandamano ni ya kuleta fujo tu?/
 
Mimi nakubaliana kwamba iko haja ya kuwa na mikakati endelevu katika mapambano ya kudai haki. napendekeza yafuatayo:
1. CHADEMA wafanyie kazi maoni hayo ya kwamba lazima kuwe na mkakati unaohakikisha kwamba wale ambao wanakuwa wahanga wa moja kwa moja wa operesheni za kudai haki, wanaenziwa.
2. kwa kuwa wanachodai CHADEMA ni kwa maslahi mapana ya taifa, na kwa kuwa CHADEMA peke yao hawatafaulu kufikia azma hiyo, ni vema wakaungwa mkono na vyama vingine na wananchi kwa ujumla. siyo vibaya watu binafsi kujitolea kutoa misaada ya hali na mali, kuanzisha mijadala kuchambua mambo haya, kuhusiana na wanafamilia wa wahanga wa operesheni, na kutoa ushauri pia.

3. CHADEMA wasiudharau muungano wa UKAWA. wasilewe na kubweteka na kusonga mbele peke yao. ushirikiano na vyama vingine katika operesheni hii ni wa muhimu sana

Ni wakati muafaka wa kufanya mambo kisayansi zaidi na kwa matokeo bora zaidi
 
hawaandamani hao wanatafuta airtime kwenye magazeti
 
Mkuu Bulldog sijawahi kuona fujo katika maadamano yoyote,fujo utokea pale polisi wanapokataa maandamano yasifanyike.Sijawahi kusikia raia wametoa uhai wa mtu kwasababu ya maandamano ila nimewahi kusikia na kushuhudia polisi wakirusha mabomu hovyo pasipo sababu za msingi na wakati mwingine unaweza kufikiri labda mabomu yalikuwa karibu ku expire ndio maana wanayavurumisha hovyo tena wakati mwingine katika sehemu ambazo hakuna viashiria vya maandamano.

Mkuu wangu nakataa maandamano kwasababu waanga wa maandamano na mikutano ya CDM wanasahaulika baada ya muda mfupi sana.


Kwanini mnadhani maandamano ni ya kuleta fujo tu?/
 
Last edited by a moderator:

..ndugu yangu tatizo lingine ni kwamba we are so used to being abused.

..tumefika mahali mpaka tunatafuta justification ya ukatili tunaofanyiwa na CCM na serikali yake.

..mfano mzuri wa hoja yangu hapo juu ni haya malalamiko na lawama kwa CDM kwamba maandamano yao yanasababisha wananchi kumwaga damu.

..binafsi sikumbuki kusikia waandamanaji wa CDM wamejeruhi polisi au raia mwingine yeyote. badala yake ni wao ndiyo wanaojeruhiwa au hata kuuwawa na polisi. katika mazingira hayo kwanini tuwalaumu CDM badala ya Polisi?

..kule Arusha kuna watoto wameuawa kutokana na harakati za Polisi kuwafanyia vurugu waandamanaji. Pamoja na hayo hakuna anayepaza sauti kulaani ukatili huo, badala yake lawama zinaelekezwa kwa victims.
 

..YES, maamuzi ya kikao cha Raisi na Ukawa siyo "enforceable" kisheria.

..lakini kwa uelewa wangu maamuzi yale yalitakiwa yafanyiwe kazi kisheria na Samuel Sitta na Mwanasheria Mkuu.

..tatizo letu ni kwamba tunaleta mizaha kwa mambo ambayo hatutakiwi kufanya mizaha nayo.

..kama Raisi alifanya mazungumzo yale akiwa ameazimia "kuwapiga chenga" Ukawa basi naye atakuwa ni mtu anayefanya mizaha kwenye mambo yasiyostahili mizaha.

..tatizo ni kwamba wananchi tumezoea mizaha na ubabaishaji kiasi kwamba tunafikia hata kusifia mambo kama hayo.

cc Ngongo
 
Last edited by a moderator:

..CDM lazima waende kwenye hivyo vikao.

..hiyo itawawezesha kujenga hoja huku kwa wananchi kwamba walikwenda mpaka kwa Raisi lakini hoja zao zimepuuzwa.
 
Wanazi wa CDM nakumbuka nilitoa ushauri huu mapema kama angalizo lakini kwa bahati mbaya hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kufuata au kusikiliza matokeo yake kila mmoja wetu anajua.Haya endeleeni kutia pamba masikioni mwenu iko siku mtajajikuta mnaangukia pua kwa kukataa ushauri wa maana.

Mrema alikuwa hivi hivi kila anachoambiwa hakutaka kusikia, masikio yakazidi kichwaa leo hii amekuwa kichekesho mbele ya jamii.


 


Mwenye busara na utashi amekuelewa sana ila mpumbavu hajakuelewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…