CHADEMA isisahau kuwa inajenga mfumo!

CHADEMA isisahau kuwa inajenga mfumo!

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,828
Toka mwaka 1992 CHADEMA imekuwa ni chama cha upinzani kinachoendeshwa kitaalamu.

Ni chama kilichoanzishwa na kuendekea kwa muktadha wa kujijenga kimfumo.

Jambo hili limekifanya CHADEMA kuwa chama imara cha upinzani kinachoendelea kukua kimfumo huku kikiwekeza katika future.

Tumeshuhudia chadema ikikua na kuimarika siku hadi siku huku kikumbana na vikwazo vingi sana kutoka katika dola.

CHADEMA imeweza kuruka viunzi vingi kwa kuwa ilijengeka kimfumo na sio kimhemuko.

CHADEMA imesurvive fitina za ccm tofauti na NCCR.

Toka mwaka 2010 CHADEMA chini ya katibu wake mkuu Dr Slaa imejitengeneza na kuweza kufikia level ya chini kabisa ya kisiasa..hapa utaona kuna mitaa na vijiji bimeweza kuchukuliwa na Chadema katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hii ndio Chadema ninayoifahamu na kuipenda.

Kwa sasa CHADEMA inapita katika wakati mgumu sana ...hili jambo sio la bahati mbaya bali ni sehemu na hatua katika ukuwaji wa chama.

Chadema ilikuwa katika mchakato wa kuendelea kujijenga kama taasisi na imekumbana na sintofahamu au dialemma kadhaa...mojawapo ni suala la katiba mpya.

Katiba mpya iliifanya CHADEMA kuingia ubia na vyama visiovyoaminika au visivyo na malengo yanayofanana nayo.

CHADEMA imeingia ndoa na vyama vyenye mirengo tofauti ili tu iendelee kufahamika na kujijenga...hili sio kosa.

CHADEMA imewahi kupokea makapi ya ccm ili tu kuendelea kujijenga.

Ni ukweli usiopingika kuwa Chadema imeweza kuachana na siasa za ushabiki na kujikita katika ujenzi wa mfumo wa chama kutoka ngazi za chini.

Kwa sasa chadema inakabiliwa na changamoto nyingine au tuseme sintofahamu nyingine.

Mwaka 2012 tulishapata tetesi za EL kujiunga na Chadema,kujisafisha na kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia Chadema.tetesi hizi zimeendelea mpaka mwaka huu wa uchaguzi pale tulipoona EL anejaribu kugombea kupitia ccm na kukatwa.

sasa habari iliyoenea mjini ni kuwa baada ya kutoswa basi EL anaweza kujiunga na CDM na kuteuliwa kuwa mgombea wao.

Hii ni changamoto kwa Chadema chama ambacho kimependwa na kuonekana kuwa muhimili wa mabadiliko nchini.

Option zilizopo kwa Chadema ni mbili tu..

1.Kumchukua El na kukubali kubeba laana waliyoianzisha ya Ufisadi au

2.kumkataa EL na kuendelea kujijenga kimfumo.hapa simaanishi wakatae makapi ya ccm yaliyoumizwa na kukatwa kwa EL bali wachukue makapi na kuyaweka pembeni halafu wasimame katika kujenga mfumo wao.

yaani changamoto hii waihandle kama vile El angepitishwa na kuwa mgombea wa ccm lazima kungekuwa na makapi kutoka ccm.

CHADEMA iendelee na safari kama ilivyopanga na isikurupushwe...mapambano ndani ya ccm yawe catalyst tu.

Nawasilisha...!
 
Hakuna cha mfumo hapo,, Chama kinafuata matakwa ya mmiliki kutoka Tengeru
 
Pamoja kwamba CCM wamebadilisha chupa na kuweka mvinyo uleule, Wanachama wa Chadema tumeendelea kuwa waaminifu kwa chama chetu. Hatumchukii Magufuli, tunaichukia CCM, hivyo hatumpi kura zetu
 
hakuna habri wala longo longo yenye maana..hpa ndipo pa kucapitalize with respect km CUF na shida zao walipewa ukweli na wameitwa mezani ktk ukawa wakiwa na adabu.Km wanalpe upuuzi wanafunguliwa mlango wakaendelee kukuw ana kukomaa.
 
Pamoja kwamba CCM wamebadilisha chupa na kuweka mvinyo uleule, Wanachama wa Chadema tumeendelea kuwa waaminifu kwa chama chetu. Hatumchukii Magufuli, tunaichukia CCM, hivyo hatumpi kura zetu

Nani anahitaji kura za watu wenye akili za ki Bavicha? Li mwenyekiti lenu nimekamia madaraka hadi linaua... Chacha Wangwe... Linapiga watu... Mwigamba.... Linafukuza... Zitto.
Bila kusahau ni chama cha kifamilia. Baba mkwe Yaani Mtei mwanaye, mumewe,Ndesamburo na wanae, Lissu na dada zake. Hierarchy inayofuata ni Wamachame, halafu wachaga wengine. CHADEMA ni crime
 
Kuoa kwa Mzee mtei halafu unapewa uenyekiti bila hata kufaulu shule ya msingi ndio kuendesha chama kitaalam?
 
Pamoja kwamba CCM wamebadilisha chupa na kuweka mvinyo uleule, Wanachama wa Chadema tumeendelea kuwa waaminifu kwa chama chetu. Hatumchukii Magufuli, tunaichukia CCM, hivyo hatumpi kura zetu

Kuna watu wanataka kuingiza au kuingizwa machakani.
 
good analysis and excellent advise.hopefully CHADEMA leadership will take a note.
 
Kwa wale wanaojua kusoma alama za nyakati wanaweza kubashiri kuwa hizi ni dalili gani kwa chama tawala......
 
Pamoja kwamba CCM wamebadilisha chupa na kuweka mvinyo uleule, Wanachama wa Chadema tumeendelea kuwa waaminifu kwa chama chetu. Hatumchukii Magufuli, tunaichukia CCM, hivyo hatumpi kura zetu

Watu wengine bana bora uwe wazi tu useme haumpi kura yako sio hatumpi kura zetu kujifanya una kundi nyuma yako!huna madhara na kelele zako za kilabuni!
 
Wewe mpinga unakurupuka, huko ulipo baba mama na watoto wote wapo nec mbona husemi, juz mlitaka kurithisha kiti kwa ndugu yake umekua huoni, vaa miwani ya kuona mbali
 
Kwa wale wanaojua kusoma alama za nyakati wanaweza kubashiri kuwa hizi ni dalili gani kwa chama tawala......

Unasoma Kelele za kwenye mitandao tu unakosa usingizi unashindwa kupima nguvu ya Tingatinga linavyotikisa mikoani hilo tosha ni pigo kwa UKAWA!!
 
Kelele za kwenye mitandao tu unakosa kusoma alama za nyakati jinsi Tingatinga linavyotikisa mikoani hilo tosha ni pigo kwa UKAWA!!

Mwenye macho haambiwi tazama....wewe endelea kujitoa ufahamu tu wakati viongozi wako huko makao makuu chupi zinabana...kwa hofu ya kimbunga cha UKAWA....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom