CHADEMA Inazidi Kuimarika

CHADEMA Inazidi Kuimarika

jnuswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,270
Reaction score
549
Wana Jf wenye mapenzi mema na CDM , nifuraha kubwa kuona CHADEMA inaimarika kila kuitwapo leo, watu wengi wanaweza kufikiri kelele za maccm na wasaliti ndani ya chama (Masalia ) watakiyumbisha Chama, hilo limeshindikana kabisa

Daima wale ambao Mungu yuko upande wao lazima wawe Washindi, na wa upande wa shetani mafisadi na waliokosa uzalendo wataendelea kuaibika milele hadi tunaingia Ikulu 2015.

Ndugu zangu hoja zote zinazotolewa kukihujumu Chama (CHADEMA ) ni dhaifu mno

Uthibitisho wa Udhaifu wa baadhi ya Hoja

1. Kupinga mkakati wa chama kununua vyombo vya usafiri na kuweka ujenzi wa Ofisi ya Chama kuwa kipaumbele kama Juliana Shonza anavyodai huo ni mtazamo finyu na kuonyesha upeo finyu wa kufikiri. Ni kweli chama hakina ofisi yenye hadhi kubwa lakini huwezi ukaweka kujenga ofisi iwe kipaumbele cha kwanza wakati huna vitendea kazi vya kukuwezesha kufika waliko wapiga kura vijijini. Kwa sasa ofisi iliyopo inatosha ila chama kikijaliwa kuwa na neema kubwa ujenzi wa ofisi nzuri ni muhimu

Mimi ni miongoni mwa wadau katika chama ambao nimeshuhudia taabu na gharama kubwa tunayoipata pindi tunapotaka kuwafikia wapiga kura vijijini, mara nyingi ni kukodi gari alafu ununue na mafuta, na kipongeza chama endapo vyombo vya usafiri vitapatikana. Waacheni hao wanaojifunza siasa waendelee kupiga kelele zisizo kuwa na maana CHADEMA mbele daima.

2. Kuongelea suala la Dr. Slaa analipwa hela nyingi kwa mwezi ni upuuzi, million saba kwa mwezi ni hela ya kawaida mno. haipaswi kuwa hoja ya msingi kujadiliwa wapo watu wengi tu wanapata mishara mpaka zaidi ya million 10 kwa mwezi nchi hii hii, hiyo nasyo ni hoja ya kipuuzi kujadiliwa

3. Hoja ya kukopa fedha na kujenga Nyumba nayo haina mashiko kwanza sina uhakika kama alikopa na kama alikopa sioni shida hapo shida ingekuwa Katibu wachama amekibia chama fedha , hata kama alikopa Dr. Slaa na wengine wengi ndani ya Chama pengine wanaowania kugombea na kuingia Ikulu 2015 ni lazima wawe na hadhi ya kutosha ikiwa ni pamoja na makazi kwa maana ya kuwa na Nyumba yenye hadhi , Watanzania najua mgesema tu maneno ya kudharau, endapo Dr. angekuwa anaishi maeneo kama ya manzese, tabata, mbagala na mengine mengi ambayo ni ya kipato cha watu wa kati na wachache wa kipato cha juu, Dr. Slaa amekuwa mwenyekiti kamati ya bunge kwenye serikali za mitaa kwa muda mrefu, hakuweza kufanya madudu aina yoyote kama wale wengine wanaoomba rushwa kufunika uchafu, yeye ameweza kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa. Jamani huyo ni kiongozi muadilifu

4. Suala la Viongozi wa kitaifa Mwenyekiti na Katibu hawawezi kusikiliza ushauri wanaamua wanayoyataka ni la kitoto hasa linapotolewa na mtu kama Shonza na Mtela Mwampamba na masalia wengine. Mdogo wangu Mwampamba kukataa ajira ya kufundisha sekondari ukamua kuendelea kukaa mjini bila kazi yoyote, mimi nilijua mwisho wako lazima uwe mbaya tu.

Naomba kwa leo niishie hapa
Edit Post Reply Reply With Quote

 
Nashukuru kwa hoja yako.

Napenda kutoa changamoto kwa MASALI. TIGO (MIC Tanzania), Vodacom na Airtel ni Makampuni makubwa Tanzania
yanaingiza millions of money kila saa. Je wanamajengo yao?????

Tangu kuanzishwa kwa vyama vingi CCM imejenga office zake? ama bado inategemea zile wananchi waliolazimishwa kuzijenga?

Tafakari na Chukua hatua.
 
Leo nimeona channel10 dk slaa na heche wakikonga myoyo ya watu. Nani kama dk slaa nani kama heche nani kama chabema
 
Leo nimeona channel10 dk slaa na heche wakikonga myoyo ya watu. Nani kama dk slaa nani kama heche nani kama chabema

mkuu!

Wengine tupo madongo kuinama, hatuna access na hiyo channel. Tupe yaliyosemwa ili tujumuike pamoja nawe kufurahi!!!!
 
Hatusikii tena!waseme wasemayo ila wasifikiri watz wa leo bado akili zao ni za enzi za NCCR MAGEUZI,TLP,CUF,et al
 
Maccm inabidi wataambue wakati umewakataa hata wakiwatumia masalia, na wao kuanzisha propaganda za namna yoyote ile watanzania hatudanganyiki ng'oo
 
Tumeshazoea propaganda za CCM chadema ni kupiga kazi tu wacha hawa magamba waendelee kumwaga porojo tu...!
 
nipo pamoja na chadema bila kujali propaganda za Masalia...Masalia ni kama changamoto tu za kisiasa.!
 
Watapiga mayowe,mwisho wa siku watalala!Wataongea mengi kuchafua kwa makusudi uongozi wa chadema at the end wanaondoka kwa aibu!Chadema itazidi songa mbele!Waseme wasemalo lakini nyuma hatugeuki!We have no time to waste kujibu hoja za kitoto isiyo na mashiko!
 
Hakuna asiejua kuwa mti wenye matunda ndio upigwao mawe,Chadema ina matunda pekee ya matumaini na hakika tutapambana na vibaraka jamii ya shonza mpuuzi na hatimaye tutashinda!!!!
 
mtu anapotamka neno chadema, anagusa maisha ya kila mtanzania moja moja.
chadema ni zaidi ya chama cha siasa, chama ambacho kwa nia njema bila gharama imeamua kupigania na kukomboa maisha ya wanyonge wa nchi hii
 
Watapiga mayowe,mwisho wa siku watalala!Wataongea mengi kuchafua kwa makusudi uongozi wa chadema at the end wanaondoka kwa aibu!Chadema itazidi songa mbele!Waseme wasemalo lakini nyuma hatugeuki!We have no time to waste kujibu hoja za kitoto isiyo na mashiko!

CDM ni mpango wa Mungu,hakuna wa kuizuia,itazidi kusonga
 
Dalili za kuimarika CDM ni pale inapoanza kushughulikia uadilifu wa viongo ndani ya chama. Inafaa kuchukua nchi.
 
Hatuwezi kurudi nyuma eti kwa sababu ya propaganda za sistaduu kama Juliana Shonza ambaye kazi yake ni unafiki tu, pia huyu mtela mwenye akili ndogo kuliko wote alipata degree ya ualimu kwa kusuasua pale DUCE na huyu mwenzie mwizi wa simu Mchange aliyekimbia UDOM.... Walishindwa polisi na usalma wa taifa ndo ije kuwa hawa waganga njaa...my foot!
 
mimi nahisi nimerogwa,maana pamoja na maneno yooote wanayoyatoa masalia,nape,mwigulu,wassira na wengineo yaani bado naipenda cdm ni haijapata kutokea.
 
mimi nahisi nimerogwa,maana pamoja na maneno yooote wanayoyatoa masalia,nape,mwigulu,wassira na wengineo yaani bado naipenda cdm ni haijapata kutokea.

Nakuhakikishia kuwa hujarogwa, tuliowengi tuko kama wewe, na sababu kubwa ni kwamba bado CDM inasimamia mambo ya msingi ambayo kila ukijegeuza unakutana nayo.
 
Back
Top Bottom