nivoj.sued
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 221
- 190
Chadema kirudi kilikotoka
Na Kondo Tutindaga
MwanaHALISI
Toleo na. 371, uk. 3.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimehitimisha ziara zake katika kanda tano, kati ya nane inaoziunda.
Kanda ambazo chama kimemaliza ziara zake ni pamoja na Kanda ya Kati(Dodoma, Morogoro na Singida); Magharibi (Kigoma, Tabora na Katavi); Kusini (Lindi, Mtwara na Ruvuma); na Nyasa(Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa).
Miongoni mmwa kazi zilizofanyika ni kusimika viongozi—wenyeviti wa kanda, makamu wenyeviti na wahazini.
Hata hivyo, mvutano mkali ulikuwa katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa. Hapa wanasiasa wawili mashuhuri wa ndani ya chama hicho, walijitokeza kuwania nafasi hiyo.
Hawa ni Patrick Ole-Sosopi, makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa. Lakini, kinyume na matarajio ya walio wengi, “Kamati Ndogo ya Kamati Kuu,” ilitangaza kumuengua Sosopi na kumpitisha Msigwa kuwa mgombea bila kuwa na mshindani.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, alinukuliwa akisema, “uamuzi wa kumkata Sosopi umefikiwa kwa maslahi mapana ya chama.”
Binafsi, naheshimu maamuzi ya Kamati Kuu (CC), lakini kamwe sikubaliani na kilichofanyika, siyo leo, kesho na hata milele, kwa sababu tatu kubwa.
Kwanza, kitendo kilichofanyika, ni ubakaji wa wazi wa demokrasia ndani ya chama hicho. Hakijawahi kufanyika hata wakati wa ukandamizaji wa mfumo wa chama kimoja.
Wakati huo, wananchi hawakuachwa kuchagua mtu na kivuli. Kulisimishwa wagombea wawili, mmoja alitumia alama ya jembe na mwingine nyundo.
Wala maslahi ya chama hayawezi kuwa ni kumwondoa Sosopi na kumpitisha Msigwa. Maslahi ya chama yako mbali zaidi ya hapo.
Ndiyo maana hata Mbowe mwenyewe ameshindwa kueleza anachokiita “maslahi mapana ya chama,” yanaweza vipi kuharibiwa na Sosopi, lakini yakalindwa na Msigwa.
Pili, nguvu ya chama tawala—Chama cha Mapinduzi—bado ni kubwa sana. Ndicho kilichowaapisha na kuwaweka madarakani viongozi wa ngazi za juu wa vyombo vya dola, yaani majeshi, Mahakama na wengineo.
Baadhi yao wakati wanapitia kwenye michakato ya siri ya kuingizwa katika vyombo nyeti, ilibidi wapate sahihi za viongozi wa chama kila ngazi.
Wengine, wanakiheshimu chama hicho kuliko aliyewateua na kuwaapisha! Tunawaona wanavyohangaika kuokoa chama hiki kwenye chaguzi mbalimbali, ikiwamo nafasi ya umeya kwenye Halmashauri za Miji na Manispaa. Wanajua bila chama hawatakuwa na kazi. Chadema ni wahanga wakubwa katika hili.
Tatu, Chadema bado ni chama kichanga mno. Hakina dola na hivyo hakitaweza kuhimili vishindo vinavyotokana na tuhuma za ukiukwaji wa demokrasia.
Mathalani, wapo wanachama wa viongozi wa ndani ya chama hiki waliotoka CCM, wakiwamo mawaziri wakuu wawili wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
Sumaye na Lowassa waliondoka CCM kutokana na kutoridhika na uvunjifu wa demokrasia. Sumaye alijiondoa CCM baada ya kukishutumu kuharibu taratibu katika kumpata mgombea urais.
Akisema, ndani ya chama hicho kuna watu wachache wanaokwenda kwenye vikao na majina ya wagombea mfukoni, kinyume na taratibu na kanuni za chama.
Kwamba, katika mfumo huu, mtu mwenye nafasi ya juu akitaka akuingize kwenye uongozi anaweza kufanya hivyo na kama hataki anakuondoa.
Lingine ambalo limemuondoa ndani ya chama hicho ni gonjwa la rushwa. Alisema, ukipinga rushwa unaonekana tatizo.
Naye Lowassa aliondoka CCM kwa sababu zinazofanana na Sumaye. Jina lake liliondolewa kwenye kinyang’anyiro cha urais, bila hata kuhojiwa.
Hivyo basi, ikiwa Chadema itaendelea kuendekeza utaratibu huu kwa kuwa kuna baadhi ya viongozi wanataka kumbeba mgombea wao, hakutakuwa na sababu ya wanaopinga “udikteta wa CCM” kuendelea kuwa Chadema.
Wanawezaje kusimama kumtuhumu mwenyekiti wa chama walichokikimbia aliyetoa majina ya wagombea wake wa urais mfukoni, wakati huko waliko mwenyekiti wao amekuja na jina la mgombea kwenye mkoba wa kokoa?
Nani anaweza kusimama na kusema Rais John Pombe Magufuli kuwa anadumaza demokrasia, wakti ndani ya chama chao baadhi ya watu wanabebwa kwa mbeleko?
Msigwa aliachwa na viongozi wakuu kuvuruga taratibu na kanuni. Aliruhusiwa kuzunguka karibu mikoa yote inayounda kanda hiyo, kujitangaz kwa wapiga kura.
Alitumia mitandao ya kijamii na magazeti kumshambulia mshindani wake. Akawatumia baadhi ya wabunge kumfanyia kampeni na wengine wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu (CC), kutoa machapisho yanayomuunga mkono. Akawananga kwa matusi baadhi ya wagombea wenake na waliokuwa wanampinga.
Lakini, pamoja na vituko vyote hivyo, hata pale viongozi wakuu wa Chadema walipoamua kumbakisha pekee, matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa yalimwacha mwmanasiasa huyo na waliombeba midomo wazi.
Wajumbe wengi walimnyima kura. Alipata kura 62 kati ya 106 zilizopigwa. Wajumbe 44 walimpinga. Ujumbe ulifikishwa unakotakiwa.
Kwa kujibu wa taarifa za ndani ya chama hicho, jina la Sosopi liliondolewa kwa kuwa anatoka Kaskazini. Kuruhusu dhambi ya aina hii kujitokeza ndani ya chama hiki, kutaweza kukiangamiza chama chenyewe na viongozi wake.
Kwamba, katika karne ya 25, wanaojiita waumini wa demokrasia, ndio wanakuwa vinara wa kupitisha mgombea kwa kura ya ndio au hapana.
Msigwa alikuwa hapambani kushika mafasi hiyo kwa sababu anataka kujenga chama katika eneo lake. La hasha. Kama angetaka kufanya hivyo, angeweza kufanya hivyo miaka 10 iliyopita.
Alitaka uenyekiti wa kanda ili kumwezesha kuingia Kamati Kuu (CC), kulinda ubunge wake na kuwa na ushawishi kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalum. Hicho ndicho alichokuwa anakitafuta.
Ni vema basi, Chadema kikarudi kuwa chama cha umma, badala ya utaratibu wa sasa wa kutaka kukifanya kuwa chama cha viongozi au mtu mmoja.
Yawezekana nguvu ya kiongozi ni ya muhimu sana. Yaweza kuwa na maono(kama ya Baba wa Taifa); yaweza kuwa ya ubabe (kama ya Mkapa); yaweza kuwa nguvu ya uungwana (kama ya Kikwete na Mwinyi); lakini nguvu hiyo inabidi aiuze kwa viongozi wenzake kwa njia ya kuwashawishi, sio kuwatisha.
Hivyo, wote wanaopiga makofi na kushangilia midomoni lakini mioyoni wakiwa wamenuna kwa woga, wanafanya makosa makubwa yatayokigharimu chama na wao wenyewe pale mambo yanapogeuka. Tuombe Mungu wasifike huko.
kondotuti@gmail.com