TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,563
Mnataka muonewe huruma?
Mwaka 2015 siyo mbali sasa nyinyi watu badala ya kuchambua chanzo cha CHADEMA kufanya vibaya kwenye uchaguzi kisomi mnakimbilia kwenye weak and unsubstantiated arguments kama vile daftari la wapiga kura,nk.Hamtakisaidia chama namna hii.
sasa mboni kabla ya uchaguzi mlijiaminisha mtashinda?....mwanakijiji aliwashauri kama mnaamini sheria mbovu, police na tume watawabeba ccm msishiriki!! mboni mlishiriki uchaguzi?
Daftari la Wapigakura ni suala la kimbumbumbu Mkuu TEKNOLOJIA? Uchambuzi huu pia ni wa kisomi kwakuwa hata mimi ni Msomi
Uchaguzi wa Ubunge wa Kalenga umekwisha na mshindi ameshapatikana. Ni Godfrey Mgimwa wa CCM. Waswahili walisema: yaliyopita si ndwele,tugange yajayo. Ndivyo inavyotakiwa kwa vyama vyote vilivyoshiriki ucaguzi wa Kalenga.Ni kwakuwa,wananchi wa Kalenga wamechagua waliyemchagua kwa matakwa yao na sababu zao. Kama alivyosema Mbunge Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa CHADEMA inayaheshimu maamuzi ya watu wa Kalenga. Lema alinena vyema sana na kidemokrasia.
Kufuatia ushindi wa Kalenga, wanachama na wapenzi wa CCM wamekuwa wakiibeza na kuikejeli sana CHADEMA. Wanafanya hivi katika upofu wa kidemokrasia.Hawajui ya kuwa uamuzi wa wananchi hautabiriki.Wananchi wanaweza kuamua chochote na muda wowote. Hizi mechi kali kati ya CCM na CHADEMA hazijaishia Kalenga.Mtanange bado unaendelea.
Wapo wanathubutu hata kusema kuwa sasa ni wakati wa uongozi wa CHADEMA kuachia ngazi. Eti kwakuwa CHADEMA imeshindwa Kalenga na katika kata 23 za Udiwani. Siamini kuwa Chaguzi Ndogo ni kipimo cha mwisho cha kufanikiwa au kushindwa kwa chama. Ni matayarisho tu ya mwaka 2015. Ingekuwa kwenye uchaguzi mkuu,hoja hii angalau ingekuwa na mshiko. Kwasasa,mambo bado haya jamani.
Kwanza, uongozi wa chama si kama kocha wa timu ya kandanda. Uongozi hutegemea watu na mawazo yao ya kujenga. Uongozi wa CHADEMA hadi hivi sasa unafanya kazi ya kutukuka na kupigiwa mfano. Umeweza kuwafanya CCM walale na mawazo kila uchao na katika kila uchaguzi wa sasa. Mapambano bado yanaendelea tena kwa kasi kubwa.
Kuna hoja ya kwamba kushindwa kwa CHADEMA Kalenga kumesababishwa na Zitto Z. Kabwe. Iko wazi kuwa Zitto hausiki na wala hakuna muda tena wa kumzungumzia ndani ya chama kwakuwa taratibu za kisheria na za kichama zinaendelea na hakuna haja ya 'majungu' katika hili. Zitto ni Zitto na CHADEMA ni CHADEMA.
CHADEMA itabezwa na kukejeliwa vya kutosha.Lakini,inazidi kuimarika na inasonga mbele. Subirini Jaji Damian Lubuva arekebishe Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wananchi wajiandikishe na kujihakiki kwa wingi, wananchi wawe na uchungu na shahada zao za kupigia kura na kutokubali kurubuniwa. Hapo ndipo demokrasia ya nchi hii itakapoonja ladha mpya. Na siku husika wala haipo mbali sana.
Itoshe kusema kuwa,CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, inaimarika na kusonga mbele. Mapambano yanaendelea hadi kieleweke. Demokrasia haina sifa ya hichohicho kuwa pale pale.
Kwani dalili ya chama kustawi ni nini.ustawi wa chama chochote ni kuungwa mkono na jamii inayoifanyia kazi,na kipimo rahisi ni kupigiwa kua nyigi sasa nyie kila kukicha mnazidi kutoungwa mkono halafu unajipa moyo.upende au ufiche uso zitto ni muhimu kwa chadema.heri uwatoe slaa na mbowe chama kitaendelea lakini zitto itachukua muda kustabilize.
Daftari la Wapigakura ni suala la kimbumbumbu Mkuu TEKNOLOJIA? Uchambuzi huu pia ni wa kisomi kwakuwa hata mimi ni Msomi
Jidanganyeni tu na kujipa moyo hivyohivyo kweli mbadala wa ccm haujazaliwa nchi. Hii
Kinachonipa nguvu zaidi ni pale ninapojiuliza "Hivi magamba watahitaji kuwa na pesa kiasi gani ambacho kitatosha kununua shahada za wapiga kura wapya zaidi ya mil.20 mara baada ya maboresho mapya ya daftari la wapiga kura sambamba watu kupewa vitambulisho vipya vingine? Maana hata mimi ninampango wa kuwa na vitambulisho vya kura zaidi ya kimoja ili wakinijia MAGAMBA niwauzie feki alafu nabaki na kile original natimba nacho kwenye kupiga kura kama kawaida! Mbona wataisoma huko mbeleni na watakoma awamu hii ya maboresho ya daftari hili! Na mimi naiomba tume icheleweshe hivyohivyo kwani vijana lazima tupige hela kwelikweli kupitia vitambulisho hivi vipya na kura tunapiga kiulainiiiii.Hiyo ndo plan ya vijana kuelekea 2015 na lazima kieleweke.
1.Watu wamepoteza/kuibiwa vitambulisho vyao vya kupigia kuraNimesema ni weak and unsubstantiated arguments yaani namaamisha ni hoja dhaifu na isiyo na ushaidi kwasababu sote hatuna uhakika kama hao wapiga kura walioachwa nje ya daftari la wapigara wanaunda idadi ya kutosha kusaidia chama kushinda au hata kama wakiandikishwa je watapiga kura?na wakipiga kura je wote wataipigia kura CHADEMA?Na ndiyo maana nikasema hiyo ni hoja dhaifu,Hapa suala ni kwa CHADEMA kubadili mbinu na mikakati tu basi!Nadhani waraka wa Dr Kitila umeweka kila kitu bayana,Ni juu ya CHADEMW kuyafanyia kazi mawazo yale.
MAJIBU SAHIHI
--------------------
Jibu ni kuboreshwa kwa Daftali la wapiga kura tuu.
Karenga ni mabibi ndio yamepiga kura kalenga sasa unafikili maCCM yangefeli kweli....
Makamanda piganieni maboresho ya daftali sasa chaguzi hizi, kwa mjini kama chalinze tutashinda tu ata kwa daftali hili.
Hongera chadema kwakushinda (ingawa hakutangazwa), kama TISS wote walikuwa pale, police nao, kauli ya mkuu wa kaaya lazima kushinda, vitisho vywa green guard na CCM mkoa, na nguvu kubwa ya kutisha vijana na watu makini kutopiga kura.... Nasema tena hongereni sanaa, SASA TUELEKE CHALINZE HAKUNA KUKATA TAMAAAAAAA...
Mungu bariki Tanzania
Mungu bariki Tendega for 2015
Mnataka muonewe huruma?