Jibu maswali haya
1. Umasikini umepungua kwa kiwango gani sasa?
Usiwe mvivu wa kusoma majarida na machapisho ya BOT, TRA na TBS pamoja na majarida ya nje km The Economist, IFM, WB, nk
2. Ajira zimepungua kivipi? Tangu 2016 wahitimu wa Elimu ya Sanaa hawajaajiriwa hadi sasa
Rejea jibu langu hapo juu na kuhusu ajira ya hao wahitimu, kama wewe ni mmoja wa hao ambao hajaajiriwa, jiajiri mwenyewe kwa kuwa mtunzi wa riwaya za filamu au maigizo au jiunge na vikundi vilivyopo vya sanaa. Tumia kichwa chako.
3. Mumenunua madiwani Arusha, mkapewa uthibitisho juu hiyo Rushwa baadae mkakiri kuhusika na hiyo Rushwa lakini kwa sababu ninyi ndio mnapambana na Rushwa hiyo mkaona sio Rushwa na muhusika mkamzawadia Cheo kingine zaidi alichokuwanacho, Sasa mnapambana na Rushwa ipi?
Kama viongozi wa upinzani wanaweza kununulika basi upinzani haufai kuongoza nchi hii!
4. Utekaji, utesaji, uuaji, kutishia viongozi silaha mchana kweupe, kushambulia watu na Risasi mchana kweupe, uokotwaji wa maiti pembezoni wa fukwe ya bahari hiyo ndio Amani mnailinda kwa wananchi?
Weka ushahidi usio na shaka, ueleweke