Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
CHADEMA IMENUNULIWA, UKAWA IMEKODISHWA, BORA LENDE!
Naona kuna upotoshaji mkubwa unafanywa na watu dhidi ya chama chetu cha ACT, nafikiri kuna haja ya kuweka mambo sawa au kukumbushana tu, sababu kwa watu kusahau kwao kunapelekea wakishambulie chama chetu.
Na siku zote tumekuwa waathirika wa mashambulizi kutoka CCM na CHADEMA, na hii kutokana na njia ya kisasa tuliyojichagulia kama chama, kuweka maslahi ya kichama kando pindi kunapokuwako na maslahi ya TAIFA.
Naomba nikutembeze katika nukta hizi 5 zenye lengo la kukumbusha tulipotoka na kuakisi kule tunapolekea kama chama mbadala wa CHADEMA na CCM.
1. "Act haitapata usajili wa kudumu, itakufa kama CCJ", wakatumwa na watu Mpanda na Mwanza ili kuvuruga usajili, lakini wapi, tukasajiliwa, na sasa chama chasonga mbele!
2. "Act si lolote ni kama UPDP, kinaongeza tu wingi na hakina athari yoyote katika siasa za nchi", lakini kwa chaguzi nyingi, tumekuwa wa tatu baada ya UKAWA au wa nne baada CUF, na maeneo mengine tulikuwa wa kwanza, mbele ya CCM na UKAWA.
Si kwamba UPDP siyo hadhi yetu tu, lakini sasa hata NCCR kilichowahi kuwa chama kikubwa tu, kinasuasua wakati ACT ikiivuta mkono CUF na kwa mbali kidogo akiiona CHADEMA na CCM wakiwa wametupa itikadi, ilani na sera zao jaani badala yake wanaishi kwa kutegemea "kiki" na matukio.
3. Katibu wetu mkuu aliwaandikia barua makatibu wakuu wote wa UKAWA, akiwaeleza nia ya ACT kutaka kujiunga na UKAWA kwa lengo la kufanya kazi pamoja ya kuiondoa CCM na kuwaletea maendeleo watanzania. Chama kiliomba makubaliano yalounda UKAWA na taratibu za kujiunga.
Barua yetu haikujibiwa, bali tulijibiwa na Mnyika katika mkutano wa hadhara Mwanza, na alisema wazi, UKAWA haiko radhi kushirikiana na wasaliti wa ACT, na kwakuwa hakuna hata chama kimoja kilichotujibu rasmi, kauli ya Mnyika, chama chetu iliipokea kama jibu la barua zetu. Ikumbukwe, tuliwaandikia barua makatibu hao kabla hata ya UKAWA kugawana majimbo na kabla ya sisi kuweka wagombea.
Hakukosea aliyewaita CHADEMA na viongozi wake manyumbu, sababu sasa hivi wanatutuhumu ACT kuwa tumekataa kufanya kazi na UKAWA, huku wakisahau kuwa ni wao hao ambao wameshindwa kujibu barua zetu, samahani, wamejibu, ila wamejibia kwenye jukwaa, wakisema "hawako tayari kufanya kazi na ACT"
Ni nyumbu ndiye hayawani pekee mwenye ujinga wa kusahau kama wanavyosahau wanachama wa CHADEMA au ujinga wa kujidanganya mwenyewe kama viongozi wa CHADEMA wanavyojidanganya!
4. Walisema mfadhili wa ACT ni Lowassa, na ya kwamba Lowassa katumia fedha chafu kuanzisha ACT kama mbinu yake mbadala kama mambo yakimuendea kombo ndani ya CCM, sivyo tu, zilitengenezwa na picha, Lowassa akiwa nyuma ya bendera ya ACT, hiyo ilikuwa njama tu ya kuinasibisha ACT na uchafu wa Lowassa kwa tarajio la kuikosesha mtaji wa watu ACT.
Mungu hamfichi mnafiki, kasema msemaji, na kauli hii imethibiti kwao, sasa Lowassa yupo CHADEMA, na jinsi alivyoingia hadi akapawa nafasi ya kuwa mgombea wa UKAWA, ni dhahiri, CHADEMA imenunuliwa na UKAWA imekodishwa.
Sababu haingii akilini hata kidogo kwa Mbowe kumsaliti Dk Slaa na ajenda ya ufisadi bila ya kuvurugwa akili na fedha za Lowassa.
Wakati wachungaji kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu walipokwenda nyumbani kwake Lowassa na kumuomba agombee urais, wanaChadema walisema kuwa wamehongwa, wakati wanafunzi wa UDOM walipokwenda kumuomba Lowassa agombee, wanaChadema wakasema wanafunzi wamehongwa, leo iweje kamanda mkakamavu wa kupambana na ufisadi, kamanda Mbowe anapolegea kama samaki mtungoni, tuseme tu kalegea kwasababu kaamua kulegea na si kwamba kalegezwa na pesa???
Haya na tujaalie, kwa kumridhisha mpumbavu na upumbavu wake, ni kweli Lowassa alikuwa anaifadhili ACT kwa fedha CHAFU, Je, Lowassa huyohuyo aliyeinunua CHADEMA na kuikodisha UKAWA kafanya hivyo kwa fedha za kimalaika?
Hivi fedha za Lowassa zilipokwenda katika makanisa, misikiti, vyuo, na kwa makada wa CCM, zilikuwa fesha chafu, lakini ziligeuka safi mara baada ya fedha hizo kuingia CHADEMA?
Hivi nani asiyejuwa Harry Kitilya, Sioi Sumari na mamaye Shose walikuwa wapo katika timu ya kutunisha mfuko wa kampeni za Lowassa? Na hawa wote wanatuhuma na kesi ya utakatishaji fedha?
Nyumbu kawaida yao, wepesi kujidanganya, kudanganya na kudanganywa na siku zote wao ni kama tanga, hufuata pepo uendapo. Wapate tabu wasio wajuwa, ila kwa mimi, abadani!
5. Huko juu nilisema, CHADEMA yaendeshwa kwa "kiki" na sasa hivi naona washapata "kiki". Si nyingine, Mwenyekiti wa ACT kateuliwa kuwa mkuu wa mkoa.
Tuko nao kwenye mitandao, hii "kiki" imewawehusha akili kiasi wasahau kuwa Mzee Ndesamburo bado hata hajazikwa, ni ukosefu wa adabu na hishima kuparamiaparamia mambo kwa lengo la kupata "kiki" ilihali ndani una maiti inayohitaji uangalizi wa karibu.
Haya, sasa, habari ya mjini ni kifurushi kipya, ukiparamia, unaparamiwa, jitahidini ili muzidi kuparamiwa, ndilo mulitakalo!
5 Juni 2017 Jumatatu 14:13
Dotto Rangimoto Chamchua
Dotto Rangimoto Chamchua
[HASHTAG]#JiniKinyonga[/HASHTAG] [HASHTAG]#NjanoTano[/HASHTAG]
Simu 0622845394