KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,149
Hakuna ubishi kwamba kwa sasa chadema angalau ndio kinaonyesha upinzani wa kweli dhidi ya chama kilichopewa dhamana na wananchi kuisimamia serikali halali iliyopo madarakani kwa mujibu wa katiba.Kutokana na umuhimu wa chadema kama chama kikuu cha upinzani nadhani ipo haja ya kukitizama sawasawa cha hiki na kujaribu kuifahamu sawasawa mikakati na malengo yako kisiasa.
Kwa kuanzia je CHADEMA inao mkakati gani hasa kuhakikisha inasimamisha mgombea ubunge katika kila eneo bunge (jimbo) kwenye uchaguzi mkuu ujao tofauti na uchaguzi mkuu uliopita ambapo kwenye maeneo bunge mengi haikuwa na wagombea ubunge?
Nadhani upo umuhimu wa chadema kuwa serious kwenye eneo hili kwa kupanga mikakati kuanzia sasa ili kipate wagombea wa kweli na sio wagombea wa kuokoteza sijui wasanii wa bongo movie,bongo fleva na makapi ya ccm,no kiwe na wagombea wa kweli ambao wameandaliwa na kuiva sawasawa na hii itakisaidia sana cha kuondokana na dhana ya kuwa kina safu nyembamba ya uongozi kiasi kwamba inakilazimu kuokoteza wagombea uongozi kama ilivyotokezea kwa john shibuda kwenye ubunge na samuel sitta ambae ilibaki chupu chupu awe mgombea urais wa chadema kama sio yeye mwenyewe kuwachomolea mwishoni kabisa.Pia ipo ile kashfa ya kumsimamisha mgombea mwenza kutoka zanzibar ambae hakua na sifa,badae ikabidi afichwe na hakuwahi kuonekana tena mpaka huwa najiuliza slaa kama angeshinda angeingia ikulu peke yake bila makamu wa rais ambae ndio nembo ya muungano,wazanzibar wangeipokeaje serikali ya slaa,zipo misteps kibao ambazo inabidi zifanyiwe kazi na kutoa majawabu kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mungine.
Upi mkakati wa chadema kuhakikisha kinasimamisha mgombea wa kweli kwenye kila eneo bunge la nchi hii???
Nawasilisha.