TUKTunapotoa maoni yetu ni vyema tukafanya na utafiti kidogo. CCM licha ya kupata Bil 2 kama ruzuku kila mwezi. mabango yao yametengenezwa ka gharama za Serikali, sasa CHADEMA yenye kupata Mil 61 tu kwa mwezi inepata wapi hizo pesa?
Tatizo la Tanzania ni moyo wa uzalendo miongoni mwa wananchi kuuawa kabisa kutokana na na matendo mabaya viongozi wa CCM wanayowatendea wananchi; hali hii imepelekea wananchi kukata tamaa ya kuchangia chochote, sijui wewe.
Sijui mwanaJF TUKO umeshachangia CHADEMA shilingi ngapi mpaka sasa. Ni kutokana na kutambua athari za wananchi kuchangia vyama vya upinzani ndio maana Serikali ya CCM huwaandama watu wanaojitoikeza kuchagngia vyama vya upinzani kwa nia ya kuvidhoofisha.
Hivyo katika mazingira haya ni lazima tupongeze hicho kidogo kilichopo na tukaze buti kuelimisha wapiga kura ushindi utapatikana tuu, kwani dhambi ya ufisadi haiwezi kusafishwa na picha na mabango.