CHADEMA: Hatutasusia Uchaguzi Mpaka Kieleweke

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Uchaguzi wa Meya Dar es salaam unazidi kuchukua headline kila siku. Ikiwa jana tu Baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa walitinga ofisi ya Halmashauri ya jiji kutaka kujua tarehe ipi uchaguzi utafanyika lakini hawakupata majibu hayo. Leo March 5 2016Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA‘ Taifa, Freeman Mbowembele ya Waandishi wa habari ameyazungumza haya….

’Hatutaomba tena kumpata Meya wa jiji la Dar es salaam, tutadai kumpata Meya, Serikali wasifikiri watapanga wao tarehe ya kumchagua Meya, wamekuwa na utaratibu wa kutaka tarehe ya kumchagua Meya kwa kutushtukizia masaa 24 kabla, kanuni inadai siku saba, tutataka tarehe ya kuchagua na siku hiyo atachaguliwa Meya asipochaguliwa Meya siku hiyo tusilaumiane’:-Freeman Mbowe
Aidha Mbowe ametoa msimamo wa chama alipoulizwa kama watasusia uchaguzi, haya ni majibu yake…

’hatuwezi kususia uchaguzi wa Meya kwa sababu ni haki yetu kuongoza jiji kwa sababu ni maamuzi ya wananchi kwa hiyo hatuwezi kususa maamuzi ya wananchi’:-Freeman Mbowe
 
Kuweni wavumilivu msifanye vurugu tulieni tuli umeya wa jiji la Dar es salaam wa ukawa.
 
Sijui kwanini serikali pendwa ya kutoa haki na kutumbua majipu haitaki kutoa haki katika hili..... So sad and disgusting.. hatutaruhusu ucommunist nchini kwetu hata kama tutapata maendeleo ya namna gani...... democracy must lead
 
Kwa sababu naye ni jipu
 
Uchaguzi wa Meya Dar es salaam unazidi kuchukua headline kila siku. Ikiwa jana tu Baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa walitinga ofisi ya Halmashauri ya jiji kutaka kujua tarehe ipi uchaguzi utafanyika lakini hawakupata majibu hayo. Leo March 5 2016Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA‘ Taifa, Freeman Mbowembele ya Waandishi wa habari ameyazungumza haya….

’Hatutaomba tena kumpata Meya wa jiji la Dar es salaam, tutadai kumpata Meya, Serikali wasifikiri watapanga wao tarehe ya kumchagua Meya, wamekuwa na utaratibu wa kutaka tarehe ya kumchagua Meya kwa kutushtukizia masaa 24 kabla, kanuni inadai siku saba, tutataka tarehe ya kuchagua na siku hiyo atachaguliwa Meya asipochaguliwa Meya siku hiyo tusilaumiane’:-Freeman Mbowe
Aidha Mbowe ametoa msimamo wa chama alipoulizwa kama watasusia uchaguzi, haya ni majibu yake…

’hatuwezi kususia uchaguzi wa Meya kwa sababu ni haki yetu kuongoza jiji kwa sababu ni maamuzi ya wananchi kwa hiyo hatuwezi kususa maamuzi ya wananchi’:-Freeman Mbowe
nasema atakaeleta fujo tusilaumiane na ndio mtakapoijua serikali ipo
 
Mbowe hajatoa vitisho, ingekuwa enzi za Mkwere angeshaanza kukusanya waandamanaji! Magu alishasema ukimkwamisha anakubomoa!
 
Utawala wa sheria na katiba ni upi? Futeni vyama vingi basi mbaki wenyewe

Vyama vingi ni pamoja na kutochochea vurugu. Mkimfanyia kama Jk lazima awafumue. Ndani ya siku mia tu wengine washalala ndani na kupekuliwa mpaka vyumbani . Enzi za Baba Riz Lema na Nasari walifikia kutangaza Jamhuri ya kaskazini hadharani na kumtaka asikanyage Arusha. Huu ni utawala unaofaa kwa wahuni
 
Wewe nikichekesho sana Sasa meweka vyama vingi vya nini? Znz cuf wamejitoa mnawarudisha wa nini si mjipe ushindi tu mnawasiwasi wa nini kingine anayeleta figisu figisu za umeya hapan Dar ni upinzani au Ccm?
 
Hivi chadema akili zao wamezivaa kwenye soks maaana wanachoongea utadhani wakula uyonga.
 
Back
Top Bottom