Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Tunakoelekea CHADEMA ni gizani. Tunazama kwenye shimo refu ambalo hatuna ujanja wa kujiokoa.
Kasi ya Rais Magufuli katika utendaji imeshatuzidi wapinzani na sasa hatuna uwezo tena wa kuhoji utendaji wake bali tunahangaika na matamko yake. Ukiona chama cha upinzani kimepokonywa ajenda zote na chama tawala basi ujue chama hicho kinaelekea kufa. Kwani katika siasa, vyama hujipambanua kwa sera na itikadi na si vinginevyo.
CHADEMA hatuna mgombea Urais mwaka 2020. Ukipitia mitandao ya kijamii na hasa kurasa za facebook na Instagram za Makamanda, utabaini kuwa Lowasa kwa sasa si mtaji tena kwetu. Yaani ni afadhali WEMA SEPETU kuliko Edward Lowasa. Leo hii tukifanya tathmini kwenye nyoyo za wapenzi wa CHADEMA, utakuta robotatu hawapo tayari Lowasa kuwa mgombea Urais 2020. Sababu zipo nyingi na zinaelezwa na Makamanda wenyewe kupitia kurasa zetu za facebook na Instagram.
Baada ya Mechi ya Simba na Yanga ambapo kwa mara ya kwanza Lowasa alienda uwanjani tangu ajiunge na CHADEMA, tumeshuhudia hali ya kiafya ya baba yetu inavyozidi kuwa mbaya. Yaani ilifika hatua hata uwezo wa kushuka ngazi hana. Nimedokezwa na mmoja wa Makamanda walioambatana naye akisema kuwa walitumia dakika 20 kushuka ngazi kutoka Jukwaa Kuu hadi chini na hapo ni baada ya mmoja wa walinzi wake kujitolea kumbeba mgongoni. Hii ni fedheha kubwa sana.
Mtaalam mmoja wa magonjwa anasema kuwa hadi 2020, Lowasa hatakuwa na uwezo tena wa kufanya kampeni za majukwaani. Ugonjwa alionao ambao siku zote unabainishwa na Kamanda wetu MANGE KIMAMBI unamtafuna akili na mwili.
Kamanda FREEMAN MBOWE angekuwa mtaji mkubwa sana kwetu hasa kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja. Hata hivyo, elimu kwake ni kikwazo. Taarifa zilizopo ni kwamba, FREEMAN MBOWE hajawahi kufanya na kufaulu mtihani wa kidato cha nne. Kwa hali hiyo, amepoteza sifa ya kupeperusha Bendera yetu uchaguzi Mkuu wa 2020.
Kila nikiangalia makamanda wengine ndani ya CHADEMA, hakuna. Nasema tena hakuna. Si Lema, Si Sugu, wala Tundu Lissu. Hakuna atakayeokoa jahazi letu. Rais Magufuli yupo kimkakati zaidi. Kaanza na miradi mikubwa ambayo ina impact kwa jamii nzima na ndio itakuwa mtaji wao kwenye kampeni za 2020. Ujenzi wa Reli, Flyovers, Bomba la Mafuta, viwanja vya ndege nk. Akishakamilisha mirahi hii anaelekea kwenye miradi ya kijamii kama afya, maji, elimu nk ambayo atahitaji mwaka au miwili tu kuikamilisha. Tumuogope sana Magufuli.
Njia pekee itakayotusaidia mwaka 2020 ni kuwa na mtu makini kwa kujenga hoja hata kama ni za upotoshaji ili ageuze yale mazuri yanayofanywa na Rais na kuingiza propaganda zetu za uongo. Mtu pekee mwenye uwezo huo ni Zitto Kabwe. Tayari alishatuaminisha kuwa zile ndege ni mtumba kutoka Kazakhstan. Sisi sote tuliamini japo wakati umetuumbua. Ndege zinapiga kazi usiku na mchna na sasa tumefunga midomo yetu.
Bila ya Zitto Kabwe 2020, wapinzani tujiandae kukabidhi majimbo mengi tuliyoshinda kwa CCM. Hatuna namna. CHADEMA tufanye maamuzi sahihi. Tumrejeshe ZITTO KABWE kwenye chama na tumteue awe mgombea Urais 2020. Tukishindwa hilo basi tumualike ndani ya UKAWA na tukubali ACT Wazalendo ndio wasimamishe mgombea Urais kwa niaba ya wapinzani wote. Tupo tayari kuingia Ikulu kwa kumkaribisha Zitto Kabwe ama tuendelee kuisindikiza CCM?