CHADEMA haiwapiganii Wananchi masikini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA haiwapiganii Wananchi masikini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by William Mshumbusi, Jul 12, 2012.

 1. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kufanya siasa ni kitu kigumu sana. Na sisi tuko pembeni tu tukiwasukuma wenzetu wajitoe muhanga bila kuogopa kuwapigania wanyonge.

  Ni nani atakaebisha kuwa CHADEMA ni chama cha kufata upepo tu. Na matukio makubwa ya ajabu na yakutisha ni upepo tu na hayaachi madhara yoyote kwa viongozi.


  Mifano.EPA, RICHIMOND, ishu ya katibu wizara ya madini kuhonga wabunge JAIRO, MGAO wa umeme USIO NA KIKOMO, IPTL, SONGASI, MIRAHABA YA 3% KWENYE MADINI, MIGOMO YA WAFANYAKAZI na vifo vingi vyenye utata kama CHACHA WANGWE, prf Chachage, Amina, katibu wa chadema arumeru, Wakili aliyekuwa akiistaki selikali swala la mgombea binafsi. Aliyekuwa katibu mkuu wa wafanyakazi wa shirika la reli na aliongoza migomo mingi tu.

  Mashambulizi kwa Kubenea, Kiwia na mbunge wa ukerewe na sasa Ulimboka
  Yote haya ni upepo tu.


  Mi naamini nchi inaongozwa na wendawazimu na wakatimwingine tunahitaji kuacti uwendawazimu kidogo ndipo kieleweke. Kwa mtazamo wa sasa wa CHADEMA ambao ni wa wastani sana 2015 ata wakishinda hawatapewa nchi kama Arusha.

  Tusipende sana kukaa nyuma ya mawazo ya viongozi wetu wa vyama bila hata ya kuyahoji. Kwa mtazamo nilionao Mishahara ya wanasiasa na posho ni hongo tosha na zinafanikiwa sana kuwaziba midomo na kuwafanya wasaau kabisa matatizo ya wananchi wao na jinsi ya kuyatatua.

  Mwaka huu kanda ya ziwa shinyanga,MWANZA, tabora wanaupungufu mkubwa wa vyakula na wanategemea kuuza pamba ili wanunue vyakula. Bei ndio hiyo 650. Toka 1360 ilipoishia mwaka jana Wabunge tunaowategemea wanakula posho tu bungeni.

  Kwanini wasitoke warudi wafanye M4C KANDA YA ZIWA tuone uzalendo wao.

  Kumbuka watu wanaotegemea Pamba ni mil 16 Tz na kati yao mil 8 wanauwezo wa kupiga kura na nizaidi ya waliopiga kura wote tanzania uchaguzi ulioisha.

  Uchaguzi unaofata wakipiga kura asilimia 20 ya waliojiandikisha mtasema watanzania wajinga? Tunatumia akili nyingi mno kuadresi vitu vidogo.

  Naomba Lema apewe uwenyekiti ata kwa miezi sita tu. Au ata nyerere au Tundulisu. Naamini viongozi watashika adabu

  Mi ustaarabu wa Mbowe unanichosha mdahalo unapokuwa wa moto mjengoni utasikia. Jamani nanihii mwachie kiongozi wako wa upinzani azungumze na akiongea ni kupoza tu.

  Mi narudia tena na tena Kwa chadema safi hatuna haja ya kuwa na wanaharakati na vyama vya wafanyakazi vitakosa kazi kabisa
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  CDM are not aggressive enough! huwezi ku compromise na CCM lazima washinikizwe kila sekunde,kila dakika hadi wajisalimishe!
   
 3. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  usiogope cdm inaenda step by step haikurupuki!
   
 4. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Aaah! Shemejiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, wewe tena?
   
 5. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Frustrations zako ni halali kabisa lakini umezitua kwa wrong person!! CCM ndio imeshindwa kuchukua hatua kukomesha mambo yote hayo. Unasikia jinsi mjengoni wanavounga mkono kwa asilimia wengine 200% matumizi ya bajeti zinazojadiliwa. Unasikia jinsi CHADEMA unaowalaumu wakipinga bajeti hizo na wakitoa maoni mbadala!!

  Nikukumbushe yafuatayo:
  a) Ni ninyi mnaobeza CHADEMA kufanya maandamano. Mnataka subira ifike 2015 Uchaguzi Mkuu.
  b) Ni ninyi mnaobeza miongozo na taarifa zinapoombwa na vyama vya upinzani.
  c) Ni ninyi mnaoaminishwa kuwa CHADEMA ni wanaharakati na mkaamini.
  d) Ni ninyi mlioukodolea wizi wa kura 2010 na kutoipigia kura UPINZANI. Hamkuwapa meno ya kurekebisha uliyoyataja.
  e) Ni ninyi mliodanganywa kwa wali, vilemba, khanga na t-shirts, fedha na lifti za maroli. Mkasahau picha kubwa!!!

  Ni udhaifu kudai CHADEMA atoke Bungeni aje kufanya M4C sehemu ulizozitaja na akiwaacha watu (wabunge wa CCM) waliosema "Kama sio elfu moja, pamba haitauzwa". Una haki gani ya kudai CHADEMA isimamie hilo wakati haiundi serikali iliyofanya maamuzi ya sh. 650??

  Tulia unyolewe, umeweka matumaini kwa CHADEMA wakati mbaya. Fanya marekebisho mwaka 2015 Ucahguzi Mkuu!
   
 6. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Neworder tuko pamoja mkuu nachoangalia chadema wanafanya nini na si wanasema nini?

  Na hapa naangalia Chadema kama Chama na si mtu kama mtu.
   
Loading...