Elections 2010 CHADEMA Haijawafikia wapiga Kura


Mazee unaweza kutengeneza perception ya kwamba CCM ina support kubwa kuliko ilivyo, na wengine wakapiga kura kwa kufuata perception hii.

Kuna watu kibao wanapiga kura kwa kuangalia nani yuko popular, na bendera nyingi ni zipi, sad as it may sound.
 
Chadema na chama chengine cha siasa kitapata tabu kubwa kushinda hadi kitakapogeuka kuwa household name.

Yaani katika kila mazungumzo hata yasiyohusiana na siasa kiwe kinatajwa.

Vitu ambavyo wengi tunavichukulia kuwa ni vidogo Kama kuweka bender a ya ccm japo kuwa HUIPENDI vikiweza kuondoka na kuwa replaced na vya vyama vya upinzani kutaashiria kuja kwa mageuzi.

Wazanzibari wanawake hawavai mchanganyiko wa kijani na nyeusi au manjano wakati wowote wakiwa nchi yoyote seuze Tanzania. Ukiwauliza wanakwambia hawawezi kujihusisha na ccm hata kwa rangi tu hata akiwa nje ya nchi.

Katika mazungumzo Yao hata sehemu haihusu ( Mimi huona hivyo) itatolewa reference nzuri ya Cuf na mbaya ya ccm. Ukimuuliza hata mkutano mmoja hajawahi kwenda.

Hapa najaribu tu kuonyesha lie culture ya upinzani ilivyoweza kuingia katika mazingira ya maisha ya kila siku na ndio maana sanduku la kura kule hutoa ushindi kwa upinzani.

Tunahitaji kupenyeza idea za chama kwenye levels zote za kijamii ili hata Yule asiyekuwa na nafasi ya kusikiliza siasa akienda kupiga kura chama cha karibu kwake kisiwe ccm
 
Nadhani CHADEMA wanahitaji kuwa open minded na kutafuta mkakati makusudi ambao utawafanya wawafikie watu kwa ukaribu na sio kupitia kwenye majukwaa tu. Hio ndio inawafanya watu wawe karibu na kukiamini chama.
 
Mazee unaweza kutengeneza perception ya kwamba CCM ina support kubwa kuliko ilivyo, na wengine wakapiga kura kwa kufuata perception hii.

Kuna watu kibao wanapiga kura kwa kuangalia nani yuko popular, na bendera nyingi ni zipi, sad as it may sound.
Nadhani invincible amesahau ile hadithi kauli ya 70% ni bendera!!!
 

Kwanza hizo picha umezi-crop! Pili, ile ya katikati si rahisi kujua jinsia wala umri kwa jinsi ilivyo ndogo, mwishio mimi sipo kwenye hizo picha lakini mwaka huu nitapiga kura - nampa Dr. Slaa!!!!!!!!
 
Advantage ya ccm ni idadi kubwa ya wananchi wasio na mwamko wa kisiasa, wasio jua haki zao, wasio na uelewa wa nini kinachoendelea katika serikali ya nchi yao. Hawa ndio watakao ichagua ccm na sio wasomi au wenye mwamko wa kisiasa au wanaojua haki zao, au wanaojua nini kinachoendelea katika nchi yao.
 
Kwanza hizo picha umezi-crop! Pili, ile ya katikati si rahisi kujua jinsia wala umri kwa jinsi ilivyo ndogo, mwishio mimi sipo kwenye hizo picha lakini mwaka huu nitapiga kura - nampa Dr. Slaa!!!!!!!!

watu kujifanya mnaelewa bwana!! hizo picha zimechukuliwa kwenye mitandao kama zilivyokuwa, hakuna cha croping hapo wala nini. Ila pamoja na wewe kupigia kura Dr. Slaa kama ambavyo wengi tutafanya, tunajaribu kufikiria namna ya kuwaleta wale wanaokosekana kwenye hili kapu waongezeke, maana kura ya wewe na mimi tu hazitatosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…