CHADEMA / H. Polepole na Siku ninayoingoja kwa hamu!

Character X

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
331
Reaction score
382
Comrades salaam,

Ninayaandika haya kwa mara nyingine ikiwa ni katikati ya kipindi cha mawazo kinzani juu ya hoja zenye tija kabisa kuhusu Tanzania yetu wakati kama huu ambapo wengi wetu tumeonyesha hamu ya kuona mabadiliko katika taifa letu na hata kufikia hatua ya kutafuta kuyapata mabadiliko hayo kwa gharama yeyote,tukidhani kwa hatua tuliyofikia hatutajali., yeyote mwenye nia yakutuunga mkono katika kuyapata mabadiliko hayo naaje tupambane kwa pamoja, lakini baadhi yetu wamechangia mawazo yao kwa kuchallenge hatua yetu hii wakionyesha wasiwasi wakuyapata mabadiliko ya kimfumo huku wakikejeli kuwa tutakachokipata mwishowe ni mabadiliko ya sura tu!

Kwanza kabisa niseme wazi, Naitamani Sana siku watanzania watakapo iondoa CCM madarakani.. i can not wait for that day to come., nikiri pia kwamba, kwangu CCM must go! and it must go now!

Wandugu, hoja ya mabadiliko ya kimfumo ni nzuri na makini, tena yenyekuangalia mambo kwa undani wake. lakini ni maoni yangu kuwa mabadiliko hayo ya kimfumo (Transformation) ambayo ndugu Hamphrey Polepole na wenzake wamekuwa wakiyazungumza sana, wakidai kuwa tunacho takiwa kukitafuta ni transformation na sio change! haiwezi kupatikana tukiwa na CCM hii madarakani. Change of party Must happen kwanza ili Transformation ya kweli iweze kufanyika.

Change haitabadilisha sura tu lakini pia akili na mitazamo ya policy makers na wenye dhamana, transformation ya kweli itatokea pale ambapo Change ya minds zilizopo itafanyika halafu ndipo jaribio la kubadilisha mifumo ikafanyika! ndipo itabadilisha utendaji.

Nimuhimu sana watanzania kufanikiwa kuiondoa CCM madarakani this time. muhimu sana!, muhimu sana kufahamu kwamba wanauwezo na mamlaka ya kufanya hivyo.

Naingoja kwa hamu siku watakapo gundua uwezo wakubadilisha watawala upo mikononi mwao, siku watakaposema aahaa kumbe yeyeyote aliyeko pale tukiamua tunamtoa tu, kumbe tukiwanyima kura wanaondoka, kumbe sisi ndo mabosi wao, kumbe tukiamua kuwawajibisha inawezekana..

Naitamani siku watanzania watapata Elimu yenye ubora., elimu itakayo watengeneza watanzania responsible! watakaofahamu kuwa siasa ni maisha, na maisha yetu sote hutegemea siasa yetu ilvyo, wakafahamu kuwa kujitenga na kutoa michango kimawazo na kihali katika kuongoza siasa na sera za nchi hii eti kwakujifanya kutokuwa mwanasiasa sio sifa! badala yake nikujinyima fursa ya kuipeleka nchi yao pale inapopaswa kuwa, huku tukiendelea kulalama kila kukicha juu ya uonevu wa wanasiasa, mabavu ya watawala flani, umimi wa watu flani wenye dhamana.

Naitamani siku uonevu na mabavu na kiburi cha watu wachache kitakapo sawazishwa, siku ambapo polisi watafahamu kuwa wao sikitengo ndani ya chama, siku usalama wataifa watakapo fahamu wao ni usalama wa "Taifa" na si Usalama wa "Chama" siku utakapo chorwa msatari ang'avu, kutenganisha shughuli za chama na shughuli za serikali! siku ambayo mihimili iliyo pewa jukumu la kuisimamia serikali itafanya shughuli ya kuisimamia serikali na siyo ya kuyasimamia matakwa ya chama-serikali.

Naingoja kwa hamu siku ambapo wakulima watapiga hesabu zao kwa umakini, kwa uelewa wa elimu ya uchumi wa kilimo waliyo nayo, na kuona kuwa kilimo kitawapa faida, waka ingia kwenye kilimo kwa biashara na sio kuimbiwa nyimbo za kilimo kwanza huku wakizuiwa kuuza mazao yao wenyewe waliyo yazalisha kwa jasho lao wenyewe katika masoko ya nje yenye kuwapa faida zaidi kwa mitaji yao.

naitamani siku wahasibu, waaalimu, madaktari, wamama wa nyumbani, ma house girls, madereva wa masafa marefu, mafundi mechanics, seremala, wachungaji na viongozzi wa dini, watu wote bila kujali tabaka lao la maisha, watakapo amka nakufahamu kuwa nchi hii ni yetu, na ulinzi wa rasilimali zetu ni jukumu letu sote na si la wanasiasa wachache!.,

naingoja siku ambapo uhuru wakujieleza utakapo zaliwa ndani ya nchi yetu, siku ambayo wafanya kazi ndani ya taasisi za kiserikali hawata ogopa kutoa mawazo yao kwauhuru eti kwa hofu ya kufukuzwa kazi., naitamani sana siku Nidhamu ya Woga itakapo iacha nchi yetu!

Na chukia Uwoga! nauchukia Unafiki., lakini zaidi sana na chukia Uonevu na Ubabe!! eeh Mungu tusaidie.,

Tunahitaji mabadiliko yenye tija, na naomba nikuhakikishie hayatunayo yapigania yana tija hakika yake!

Tuungane pamoja kwanguvu zetu tuiweke nguvu ya kuongoza hatma ya tanzania mikononi mwa watanzania. and that can be done this year!

comrades,
Nawashukuru sana
 
Brother character x, real u have touched me. we real need true tranformation right now.! fifty years of loosing is enough. let we join together our hands to get the new country of our desire.! Together we can.!
 
H.Polepole ukweli huo anaujua sana wakimahitaji ya watanzania juu ya mabadiliko ya kichama na serikali ili mapinduzi ya kiuchumia na kijamii yatokee,tatizo jamaa kishamegewewa chake ndo maana anajalibu kucheza na misamiati ili kuchota akili za watu
 
Mimi nikisoma uzi ukifika tu kuikataa CCM basi huwa naishia hapo japo na kumpongeza aliyeposti. Hongera sana mkuu japo sikumalizia kusoma ulichoandika mwishoni kwani sina muda huo.
 
Si ajabu mkurugenzi wa tbc anaogopa yaliyomkuta Tido
 
Ukwel ni kuwa huwez kuwa ccm ...uache kuitetea ....polepole ni mnafiki...kwa nn hampingi Samia suluhu ...aliye ua katiba ya warioba ???!
 
Comrades salaam,

Ninayaandika haya kwa mara nyingine ikiwa ni katikati ya kipindi cha mawazo kinzani juu ya hoja zenye tija kabisa kuhusu Tanzania yetu wakati kama huu ambapo wengi wetu tumeonyesha hamu ya kuona mabadiliko katika taifa letu na hata kufikia hatua ya kutafuta kuyapata mabadiliko hayo kwa gharama yeyote,tukidhani kwa hatua tuliyofikia hatutajali., yeyote mwenye nia yakutuunga mkono katika kuyapata mabadiliko hayo naaje tupambane kwa pamoja, lakini baadhi yetu wamechangia mawazo yao kwa kuchallenge hatua yetu hii wakionyesha wasiwasi wakuyapata mabadiliko ya kimfumo huku wakikejeli kuwa tutakachokipata mwishowe ni mabadiliko ya sura tu!

Kwanza kabisa niseme wazi, Naitamani Sana siku watanzania watakapo iondoa CCM madarakani.. i can not wait for that day to come., nikiri pia kwamba, kwangu CCM must go! and it must go now!

Wandugu, hoja ya mabadiliko ya kimfumo ni nzuri na makini, tena yenyekuangalia mambo kwa undani wake. lakini ni maoni yangu kuwa mabadiliko hayo ya kimfumo (Transformation) ambayo ndugu Hamphrey Polepole na wenzake wamekuwa wakiyazungumza sana, wakidai kuwa tunacho takiwa kukitafuta ni transformation na sio change! haiwezi kupatikana tukiwa na CCM hii madarakani. Change of party Must happen kwanza ili Transformation ya kweli iweze kufanyika.

Change haitabadilisha sura tu lakini pia akili na mitazamo ya policy makers na wenye dhamana, transformation ya kweli itatokea pale ambapo Change ya minds zilizopo itafanyika halafu ndipo jaribio la kubadilisha mifumo ikafanyika! ndipo itabadilisha utendaji.

Nimuhimu sana watanzania kufanikiwa kuiondoa CCM madarakani this time. muhimu sana!, muhimu sana kufahamu kwamba wanauwezo na mamlaka ya kufanya hivyo.

Naingoja kwa hamu siku watakapo gundua uwezo wakubadilisha watawala upo mikononi mwao, siku watakaposema aahaa kumbe yeyeyote aliyeko pale tukiamua tunamtoa tu, kumbe tukiwanyima kura wanaondoka, kumbe sisi ndo mabosi wao, kumbe tukiamua kuwawajibisha inawezekana..

Naitamani siku watanzania watapata Elimu yenye ubora., elimu itakayo watengeneza watanzania responsible! watakaofahamu kuwa siasa ni maisha, na maisha yetu sote hutegemea siasa yetu ilvyo, wakafahamu kuwa kujitenga na kutoa michango kimawazo na kihali katika kuongoza siasa na sera za nchi hii eti kwakujifanya kutokuwa mwanasiasa sio sifa! badala yake nikujinyima fursa ya kuipeleka nchi yao pale inapopaswa kuwa, huku tukiendelea kulalama kila kukicha juu ya uonevu wa wanasiasa, mabavu ya watawala flani, umimi wa watu flani wenye dhamana.

Naitamani siku uonevu na mabavu na kiburi cha watu wachache kitakapo sawazishwa, siku ambapo polisi watafahamu kuwa wao sikitengo ndani ya chama, siku usalama wataifa watakapo fahamu wao ni usalama wa "Taifa" na si Usalama wa "Chama" siku utakapo chorwa msatari ang'avu, kutenganisha shughuli za chama na shughuli za serikali! siku ambayo mihimili iliyo pewa jukumu la kuisimamia serikali itafanya shughuli ya kuisimamia serikali na siyo ya kuyasimamia matakwa ya chama-serikali.

Naingoja kwa hamu siku ambapo wakulima watapiga hesabu zao kwa umakini, kwa uelewa wa elimu ya uchumi wa kilimo waliyo nayo, na kuona kuwa kilimo kitawapa faida, waka ingia kwenye kilimo kwa biashara na sio kuimbiwa nyimbo za kilimo kwanza huku wakizuiwa kuuza mazao yao wenyewe waliyo yazalisha kwa jasho lao wenyewe katika masoko ya nje yenye kuwapa faida zaidi kwa mitaji yao.

naitamani siku wahasibu, waaalimu, madaktari, wamama wa nyumbani, ma house girls, madereva wa masafa marefu, mafundi mechanics, seremala, wachungaji na viongozzi wa dini, watu wote bila kujali tabaka lao la maisha, watakapo amka nakufahamu kuwa nchi hii ni yetu, na ulinzi wa rasilimali zetu ni jukumu letu sote na si la wanasiasa wachache!.,

naingoja siku ambapo uhuru wakujieleza utakapo zaliwa ndani ya nchi yetu, siku ambayo wafanya kazi ndani ya taasisi za kiserikali hawata ogopa kutoa mawazo yao kwauhuru eti kwa hofu ya kufukuzwa kazi., naitamani sana siku Nidhamu ya Woga itakapo iacha nchi yetu!

Na chukia Uwoga! nauchukia Unafiki., lakini zaidi sana na chukia Uonevu na Ubabe!! eeh Mungu tusaidie.,

Tunahitaji mabadiliko yenye tija, na naomba nikuhakikishie hayatunayo yapigania yana tija hakika yake!

Tuungane pamoja kwanguvu zetu tuiweke nguvu ya kuongoza hatma ya tanzania mikononi mwa watanzania. and that can be done this year!

comrades,
Nawashukuru sana

Nimekuelewa sana mkuu.
 
huyu polepole hana mana kwasababu Samia Suluhu alikua anahusika na uchakachuaji wa katiba ambayo wao waliipagania lkn maoni yetu yakatupwa halafu leo anashindwa kumkosoa Samia anakomaa na lowassa
 
Pole pole anatakiwa achapwe viboko saba maana kichwani hazimtoshi!!
 
Na chukia Uwoga! nauchukia Unafiki., lakini zaidi sana na chukia Uonevu na Ubabe!! eeh Mungu tusaidie.,

Hapa ndo umesema kila kitu.
Watanzania tuna woga wa kijnga sana. Tumejawa na unafki usio na kipimo. Kila siku tunaonewa tunaumia ila bado tunawachagua walewale waliotummiza.
 
Back
Top Bottom