CHADEMA Geita yabeza propaganda za CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Faida Muyomba, Geita

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Geita kimewataka viongozi (CCM) kutotumia fedha za wananchi kwa kueneza propaganda wanazodai za uongo majukwaani, badala yake wafanye kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Pia chama hicho kimesema mkakati wa CCM wa kujivua gamba, hauna tija kwa Watanzania bali hizo ni dalili za kushindwa kuwashughulikia mafisadi ndani ya chama hicho.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mwenezi wa chama hicho wilayani Geita, Bw. Ignas Karashani, wakati akizungumza na umati wa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara, katika mji mdogo wa Katoro juzi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya wilaya, pamoja na madiwani, ukiwa na lengo la kuwaeleza wananchi namna wanavyopambana na ufisadi unaodaiwa kufanywa na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Alisema, "CHADEMA tunawataka CCM na Nape wao waache kuifuatafuata Chadema kwa kutunga uongo majukwaani bali wafanye shughuli zinazowaletea maendeleo wananchi."

Aliongeza, anazunguka majukwaani eti wanadai wamejivua gamba, sote tunajua kuwa nyoka hauliwi kwa kuvuliwa gamba bali kupigwa kichwa na kufa, hivyo CCM wamedhihirisha kushindwa kuongoza nchi hii wanatakiwa kujiondoa wenyewe madarakani."

Katibu huyo alisema, Watanzania wamechoshwa na ugumu wa maisha wanaopambana nao kila siku, hivyo viongozi wa CCM wanatakiwa kutafuta njia za kuwakomboa katika janga hilo na si kukalia kujibu mapigo yanayotolewa na viongozi wa CHADEMA.

Chama hicho kina madiwani wanane katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ambapo hivi karibuni walisusia upitishaji wa bajeti kwa madai ya kutopewa muda wa kupitia kabrasha kabla ya kikao.
 
Hongera mwenezi kwa kuwambia ukweli hao magamba nafikiri wamejisahau wanafikiri wao pia ni chama cha upinzani badala ya kuwaeleza wananchi wamefanya nini kwa miaka 50 wanazunguka kumwaga uzushi, watuambie kwanini kuna ugumu wa maisha watu wanalala bila kula.
 
Back
Top Bottom