CHADEMA: Fr. Kitima si mwananchama wetu

CHADEMA: Fr. Kitima si mwananchama wetu

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha madai ya Padri wa Kanisa Katoliki Dk Charles Kitima kuhusishwa na siasa za chama hicho kikieleza kwamba si mwanachama wa chama hicho na wala hajawahi kualikwa kufanya siasa za chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika chama hicho, Padri Kitima hana kadi ya chama hicho na hajawahi kualikwa katika vikao rasmi vya chama hicho wala kufanya kampeni yoyote inayokihusisha chama hicho kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya wananchi.

Katika barua iliyoandikwa na baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania kwenda ubalozi wa kanisa hilo hapa nchini imedaiwa Padri Charles Kitima amekuwa akijihusisha na siasa za CHADEMA jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kanisa hilo.

Waumini hao wameomba kuchukuliwa hatua dhidi ya Padri Kitima kwa kile kilichodaiwa kuharibu taswira ya kanisa hilo kwa kuonekana kujihusisha na harakati za kisiasa.
1767774991715.png

Chanzo: Nipashe
 
View attachment 3526553
Chanzo: Nipashe
yes ni kweli,
but huyo anafahamika vyema kwamba ni mamluki wa chadema ndani ya kanisa katoliki kupitia TEC :NoGodNo:
 
Mimi binafsi namuona km mpuuzi, kafiri Moja TU . Hana lolote zaidi ya ufala kumjaa kichwani. Wewe jitu Zima msomi unaabudu sanamu.
 
Wewe mbona unamwini muddy alonyonya fc libolo ya kijana ya madrasat
 
CHADEMA wawe straight!Wasijumuishe wananchi wote.Waseme ni wana-CCM ndiyo wanatengeneza uongouongo kwa Father Kitima ili kukwepa hasira za Watanganyika.Kwisha.
CHADEMA hawajuagi kutojumuisha. Wao wana neno "WOTE TU".
Utasikia eti watanzania wote hawamtaki Dr Samia. Weeeeeeeee! Acheni kudanganya dunia. Na acheni kauli ya WOTE....
 
CHADEMA na huyo Kitima wanatuona kama wapumbavu wenzao? Kitima, Bagonza na Mwamakula ni wanaCHADEMA. Hao hupanda hadi kwenye majukwa ya CHADEMA halafu sasa wanakana wao sio wanaCHADEMA. Upuuzi mtupu.
 
Ukiingia China kununua vitunguu mara hiyohiyo unakuwa mchina?
 
Back
Top Bottom