Huu ni mpango wa siri kweli wa kuitenganisha ccm na kagoda kama alivyosema Plato. Bwana Msemakweli inaonekana anajua mengi kuhusu CCM na ndo maana anaitetea na ninamnukuu kwenye barua yake kwa DDP" Watu hawa wamekuwa wakieneza uvumi kwamba fedha zillibiwa na kutumika kwa madhumuni ya kampeni ya CCM mwaka 2005 jambo ambalo si kweli. Lengo wa uongo huu ni kukishawishi chama tawala kutumia vyombo vya dola kunyamazizsha swala hili kwa kuhofia kwamba bila kufanya hivyo chama kitaumbuka.Ukweli ni kwamba mnamo tarehe 30 December 2005 na 2 January 2006 fedha hizo zilikuwa hazijatumika na zikahamishwa kutoka akaunti ya Kagoda Agriculture Limited kwenda kwenye kampuni ya Quality Finance Corporation Ltd na kutoka hapo zikaenda nje ya nchi kupitia Bureau dechange"Anachotaka kutulazimisha tuamini1. CCM haikuhusika na Kagoda na wala hela za kagoda hazina baraka za mkuu yeyote wa SerikaliAnachoshindwa kuikwamua CCM kwenye kashifa hii1. CCM imekubali kushawishiwa na kutochukua hatua kwa muda wote huo tangu 2005 mpaka leo miaka 6 kwa wahusika wa kagoda - Kwa hiyo mkono wa kagoda ni mrefu serikalini kuliko hata CCM yenyewe.2. Kwa nini chama kiogope kuumbuka kwa mambo ambayo hakikijua mwanzo wake na mwisho wake?3. Uzembe wa serikali ya CCM kushindwa kuthibiti taasisi za fedha kama bureau dechane.4. Bila kujali kama hela zilitumiwa na CCM kwa ajili ya uchaguzi au la lazima wizi wowote uchukuliwe hatua. Kushindwa kufanya ni kukumbatia.5. Pinda Waziri mkuu aliwahi kusema ni heri kufa kuliko kufuatilia swala la Kagoda; Je ni hatari kuifuatilia kagoda (John Kato na Baruti Goda)Hata CCM ifanyeje si safi hata kidogo katika kulinda pesa na rasirimali za taifa hili- Kagoda hatuwezi kuwafualitia- Wanyama waliotoroshwa serikali haijiu walipo- Wamiliki wa Dowans serikali haikuwajua- N.k kwa nini watake kujisafisha kwa bei rahisi kwa watanzania?
Hawawezi kuchoomoka hao kwenye hii issue.Hapa kuna usanii mkubwa ambao wananchi hawaujui nadhani wanatumiwa na wanasiasa!
Mnaambiwa saizi CCM haimo kwa hiyo CCM ni wasafi walikuwa wanasingiziwa tu?
Hoja ya msemakweli ina agenda ya siri.wakati ambapo inatolewa,wakati wote alikuwa wapi? Chombo iliporipotiwa,kujiita chadema,ni kwa malengo maalum.ili ionekane sasa kuwa tuhuma zinahusiana na chadema,lakini pia mwana chadema ameitenga kagoda na ccm.ametaja majina ya watu na makusudi kuyatenga na ccm.
Hii ieleweke anawashambulia wabaya wa mengi pekee kwa upande mmoja,na anafanya propaganda za ccm hapohapo.ndiyo maana ya yeye kujiita chadema,na kuwataja kina rostamu na manji kama watu binafsi akiwatenga na ccm kama msekwa na malechela wanavyotaka iwe.
Gazeti la uhuru leo limechekelea sana hoja hiyo
kuna conection na uchaguzi wa igunga ili ccm iseme chama siyo fisadi ila watu binafsi na ushahidi mpya ni huu wa mwanachadema.watu watakuwa bado wanakumbuka hii issue.
Sanze aliyekuwa anasifiwa kutoa andiko kuunganisha mkapa na kikwete ,rostamu na ccm amebezwa.
Msiseme hakuna jipya.lipo.anataka ushahidi wa siku zote unaounganisha ccm na kagoda uonekane feki.
Leo anajifanya anaenda kwa dpp.kwa kuwa ni mpango wa ccm dpp atafungua kesi jumatatu na mahakama itazuia suala la kagoda kujadiliwa igunga.
Nani bado anashangilia mbwembwe za huyu mnafiki? CHADEMA msishangilie ujinga huu wa CCM na msemakweli.toeni msisitizo wa uhusika wa ccm kwa vyombo vya habari mapema kabla hamjapigwa bao tena na ccm.
Msemakweli naye fisadi hatari