CHADEMA, Endeleeni kukaza buti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, Endeleeni kukaza buti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurtu, Jul 16, 2011.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wengi wetu tunatambua wazi kuwa kazi inayofanywa na CHADEMA na baadhi ya vyama vya upinzani inahitaji kuungwa mkono. Tunatakiwa kuunga mkono juhudi za CDM kwa sababu nyingi, zikiwemo hizi zifuatazo:
  1. CDM wametufumbua macho sisi Watanzania kwamba Tanzania tuna raslimali nyingi ambazo zinawafaidisha wageni badala ya Watanzania. Raslimali za nchi hii zimetumiwa na wageni wanaokuja kwa jina la uwekezaji na kutuacha Watanzania tukiwa hoi. Sekta ya madini inaongoza katika kuwapatia wageni utajiri na kutuachia umaskini Watanzania. Kwa muda mrefu CDM wamekuwa wakipiga kelele kwamba sekta ya madini inawafaidisha sana wageni huku serikali haipati hata kodi kutoka kwa hao wageni zaidi mrahaba.

  2. Serikali ya CCM imekuwa ikitumia fedha nyingi katika matumizi kama ya posho wakati ikijidai haina uwezo wa kuongeza mishahara ya watumishi. Jambo hili lilivaliwa njuga na CDM hasa walipoanza na posho za wabunge. Mwanzoni Serkali ya CCM ilipinga jambo hilo hasa pale Waziri mkuu aliposema kuwa posho zile ni kidogo na kwamba wabunge wanazitumia kuwapa wageni wanaowatembelea pale Dodoma. Waziri mkuu alishindwa kuelewa kuwa Watanzania hatutaki kuwa omba omba na hatutaki wabunge wetu wawe mashirika ya wafadhili kwa wananchi.

  Hatimaye Waziri mkuu siku anahitimisha majadiliano ya bajeti ya ofisi yake alikiri kuwa serikali itatazama upya suala la posho hasa zile ambazo hazina tija. Je, huko siyo kusalimu amri? Kama kweli serikali italifanyia kazi suala hilo la posho basi CDM wanastahili pongezi kubwa sana.

  3. CDM walisisitiza sana suala la Katiba Mpya katika kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana. CCM walikaa kimya wakidhani huo ulikuwa wimbo wa CDM peke yao bila kujua kwamba wananchi walikuwa wanauitikia. Mh. Mnyika, mbunge wa ubungo(CDM) akaonyesha nia yake ya kuwasilisha hoja binafsi kuhusu katiba. Serikali ya CCM iilipoona mwelekeo wa hoja ya Mh. Mnyika na kwa kuogopa nguvu ya umma CCM ikasalimu amri. Serikali ya CCM ikaandaa muswada wa Mapitio ya Katiba ili kuhadaa wananchi. CDM wakagundua ujanja wa CCM na wananchi wakawaunga mkono CDM, hatimaye serikali ya CCM ikagundua kuwa hawawezi kupenya. CCM ikarudisha Muswada kabatini. Hadi leo Muswada wa Mapitio ya Katiba unasubiriwa utoke huo uliko. Wakati huo huo serikali imeshaanza kutoa ahadi kuwa katiba mpya itapatikana mwaka 2014. CDM endeleeni kuibana hadi kieleweke.

  4. Juzi juzi CCM walianzisha falsafa ya kujivua gamba. Jambo hilo halikuanzishwa na CCM kwa hiari yao bali kwa shinikizo la CDM hasa tangu ile list of shame ilipotolewa na viongozi wa CDM. CCM walipoanzisha falsafa hiyo walijikuta wameanza kulumbana wao kwa wao. Mara wamewaita watu watatu kama ndiyo vinara wa ufisadi, mara wakwepe kutaja majina yao, mara waseme wamewandikia barua, hatimaye juzi juzi Rostam Aziz amejiuzulu nafasi zake ndani ya CCM yaani ujumbe wa NEC na Ubunge. Hata hivyo jambo la kushangaza wahusika wakuu ndani ya CCM wanadai kuwa hawajapata taarifa rasmi. Kama Rostam alikuwa katika orodha ya watu wanaotakiwa kujivua gamba, walitegemea nini zaidi ya hilo alilolifanya? Au CCM wanafikiri kuwa alichokuwa anakitamka Rostam mbele ya waandishi wa habari ilikuwa ni kuwahadaa wao? Kwanini CCM hawajamwita na kumwomba barua yake ya kujiuzulu?

  Hivyo basi, kwa mwelekeo huo ambao CDM wameuonyesha wa jinsi walivyoibana vizuri serikali tutarajie zaidi mambo makuu ambayo hata kama serikali ya CCM haitakuwa na nia ya kuyatekeleza lakini italazimika kutekeleza.
   
Loading...