Bailly5
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 16,402
- 35,083
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Vincent Mashinji amesema kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge ni sawa na kuling’oa meno bunge hilo.
Tofauti na mikutano miwili iliyopita ya Novemba 2015 na Januari/ Februari 2016, Serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli, iliamua kufuta matangazo ya moja kwa moja ya Bunge la Bajeti lililoanza vikao vyake Aprili 19 kwa maelezo kwamba ni gharama kubwa kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
Badala yake TBC huonyesha kipindi cha maswali na majibu pekee na hurekodi matangazo mengine na kurushwa katika kipindi cha ‘Leo katika Bunge’ saa nne usiku.
Suala hilo lilipingwa vikali na wabunge wa upinzani lakini uongozi wa Bunge ulitia chumvi kwenye kidonda baada ya kukataza vyombo vya habari kupiga picha za video, badala yake wanatakiwa kuchukua picha kutoka kwa televisheni ya Bunge.
Akizungumzia hali hiyo jana alipofanya ziara katika ofisi za gazeti hili zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam, Dk Mashinji alisema kuwa huu ni mkakati maalum uliosukwa na CCM ili kuvibana vyama vya upinzani.
“Siri ni kwamba Bunge la sasa halina meno….Kwa taarifa tulizonazo, CCM walifanya utafiti wakagundua kwamba wapinzani wamepata nguvu kubwa kupitia bungeni; yaani Bunge limekuwa njia kubwa ya utetezi wao. Kwa hiyo, njia pekee ni kulinyamazisha. Wakasema acheni tu kipindi cha maswali na majibu kwa sababu hakina kitu. Acha punda afe lakini mzigo wa bwana ufike,” alisema Dk Mashinji.
Dk Mashinji ambaye aliteuliwa mapema mwaka huu kuchukua nafasi hiyo iliyoachwa na Dk Willibrod Slaa aliyeamua kujiondoa katikati ya uchaguzi mkuu mwaka jana alisema licha ya kuweka mipango ya kupambana katika suala hilo, bado wanajua nyuma yake kuna mpango maalumu wa CCM.
Hata hivyo, alisema katika kupambana na hali hiyo chama chake kimeamua kurusha moja kwa moja majadiliano yanayofanyika katika mabaraza ya madiwani.
“Moja ya vitu ambavyo tunavifanya ni kuwaambia mameya wetu, mikutano yao ya mabaraza ya madiwani iwe ya hadhara. Arusha wameshaanza, wanarusha kwenye Radio 5, wamefunga na spika nje japokuwa uwezo wa kulipia televisheni bado ni mdogo,” alisema.
“Tumeshauriwa pia tufungue kesi lakini sasa suala ni kwamba, ukishafungua tu kesi tunajiweka kwenye wakati mgumu. Ukitaka tu kulisema utaambiwa liko mahakamani.”
Chanzo: Mwananchi