CHADEMA Arusha yataka wanaotaka kuhama chama waondoke haraka

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Chadema mkoani Arusha imewapa mkono wa kwaheri viongozi wake wanaotoka kuhama na kuwataka waondoke sasa kwa kuwa chama hicho “kitakuwa na kazi kubwa ambazo zitahitaji kujitoa kwa dhati”.

Hadi sasa madiwani watano wa Chadema mkoani hapa wameshajiondoa. Madiwani hao ni Credo Kifukwe (Murieti), Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya (Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu).

Katika taarifa aliyoitoa jana kuhusu wimbi la kujiuzulu kwa madiwani, mwenyekiti wa Chadema wa mkoa, Aman Golugwa alisema kuondoka kwao hakuathiri chama hicho.

“Wana Chadema msisikitike, wamechelewa kuondoka na msione kuwa wanatushtukiza, hapana. Wao ndio wamekaa kwa mateso na sasa hawana budi kuondoka maana hawakuwa wa kwetu,” alisema.

Golugwa alisema bado kuna watakaoondoka na kwamba chama hicho hakitawazuia kwa kuwa kilijua kuna watu wataondoka na baadhi bado wapo njiani.

“Tuwaache waondoke wenyewe. Kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa na inahitaji waliojitoa hasa na wenye mapenzi mema na nchi hii kwa kuwa hila yao kwa kipindi walichokaa nasi na dhambi yao ya maneno ya uongo wakati wa kuondoka kwao, watailipa tu,” alisema.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema kujiuzulu kwa madiwani wa chama hicho katika kata hizo kunatokana na ushawishi wa fedha na madaraka, jambo ambalo limekanushwa na madiwani hao.

Katika taarifa walizotoa baada ya kujiuzulu, madiwani hao wamekuwa wakieleza kuridhishwa kwao na utendaji wa Rais John Magufuli na wasaidizi wake na hivyo kusema hawana sababu ya kupingana na Serikali iliyopo madarakani.

Katika uchaguzi uliopita, Chadema Mkoa wa Arusha ilifanikiwa kushinda majimbo sita kati ya saba na kuongoza halmashauri tano kati ya saba jambo ambalo halijawahi kutokea.
 
Hili tamko lilichelewa
Maana mtu mwenye akili timamu hawezi kujiuzulu kutoka chadema kwenda chama cha wizi wa madini CCM

Wajiuzulu wote waliopewa hela haraka
Na tutashinda tena kama kawaida

Arusha ni chadema tu
Ccm tupa kule na gambo wake
 
Hili tamko lilichelewa
Maana mtu mwenye akili timamu hawezi kujiuzulu kutoka chadema kwenda chama cha wizi wa madini ccm
Wajiuzulu wote waliopewa hela haraka
Na tutashinda tena kama kawaida

Arusha ni chadema tu
Ccm tupa kule na gambo wake
Diwani wa Muriet alisema anapumzika siasa...ina maana kaachana na chama cha kufuga mafisadi na kupumzika siasa.
 
hahahahaha..eti mtu anajiuzulu kwa kuridhishwa...hahahahah...comedy at work

Alafu wote sababu moja

Ukweli ni kuwa sasaivi udiwani hauna pesa...Hao walienda huko kwa malengo ya pesa..hazipo...so wamenunuliwa na vijisenti vichache wameamua kuwasaliti wananchi
 
Rushwa inawatafuna ni vizuri watoke waende ccm wakakatwe mikia na kuingizwa kwenye zizi la ng'ombe
 
Hawa kwa kweli hawakuwa wapinzani. Wanathibitisha ule usemi usemao "Kwenye msafara wa Mamba na Kenge wapo". Eti mtu ana sema yeye yuko upinzani halafu anasema anamuunga mkono mtu afanyaye yafuatayo:

1. Anapiga marufuku shughuli za siasa kama vile mikutano. Ina maana hawa madiwani wa upinzani hawataki kufanya shughuli za siasa kama vile mikutano? Sasa kama hawataki shughuli za siasa waliingiaje kwenye siasa na kuwa madiwani?

2. Anapiga marufuku watoto wa kike waliozaa kusoma. Ina maana huyo Josephine si mwanamke? Kama ni mwanamke ananiambie ni silaha gani ya kumkomboa mtoto wa kike au mwanamke zaidi ya elimu?

3. Analilia makinikia (mabaki) na kuacha dhahabu halisi ikiendelea kutoroshwa. Ina maana hao madiwani wanaona makinikia ni bora kuliko dhahabu halisi?

4. Anawaadhibu watumishi wa umma wenye vyeti feki lakini anawaacha wakuu wa mikoa, wilaya, wabunge na madiwani eti kwa hao vyeti feki havina shida. Je, hao madiwani wanakubaliana na hilo? Ina maana hao madiwani hawataki usawa kwa wote kwenye makosa?

5. Anawahusisha waislamu na mauaji ya kibiti, je, nalo hilo wanamuunga mkono? Hivi ni kweli yale mauaji yanafanywa na hawa waislamu wa uamsho? Hiyo si kukashfu dini na imani za watu?

Wewe kama kweli ni mpinzani wa kweli ambaye kazi yako ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani na kuonyesha njia sahihi ya kuendesha nchi unamuungaje mkono mtu anayefanya hayo yote?
 
Kwa nini Arusha tu? toeni tamko kwa Tanzania nzima kuwa wanaotaka kuhama wahame sasa.
 
"5. Anawahusisha waislamu na mauaji ya kibiti, je, nalo hilo wanamuunga mkono? Hivi ni kweli yale mauaji yanafanywa na hawa waislamu wa uamsho? Hiyo si kukashfu dini na imani za watu?"

Si sahihi kuwaita Kikundi cha kihalifu cha UAMSHO eti WAISLAMU WA UAMSHO!...Ni sawa na kuwa ita alqaeda au alshababu waislamu wa alqaeda au alshababu...uhalifu hauna dini...dini zote zinakataza uhalifu wa aina yoyote ili!
 
jingojames: Hao madiwani walijiita ni wanasiasa wa upinzani. Utaendeshaje siasa bila mikutano? Sasa badala ya kudai haki ya kufanya siasa iliyowaajiri wanamuunga mkono anayetakaza kufanya shughuli za siasa, halafu wanamfurahia na kumuunga mkono. Hap[o utamwelewaje huyo anayejiita mwanasiasa wa upinzani? Ina maana naye hataki kufanya shughuli za siasa kama vile mikutano? Sasa kwa nini aliingia kwenye siasa? Ni sawa na mtu anaingia kwenye huduma ya upadri au uchungaji halafu anamuunga mkono mtu anayepiga marufuku misa au ibada. Utamwelewaje huyo padri au mchungaji? Mtu anaingia kwenye kazi ya ualimu halafu anamuunga mkono mtu anayepiga marufuku kuingia darasani kufundisha, utamwelewaje huyo mwalimu. Je, kweli huyo ni mwalimu? Mtu anaingia kazi ya kuuza nyama ya ng'ombe, halafu anamuunga mkono mtu anayepiga marufuku ng'ombe kuchinjwa na pia anamuunga mkono mtu anayepiga marufuku bucha zisiwepo, utamwelewaje huyo muuza nyama? Anaelewa kazi yake?Bure kabisa. Kama ni mwanamume tunasema ameingia choo cha kike. Hao madiwani wakiume waliingia choo cha kike na yule diwani wa kike aliingia choo cha kiume, yaani waliingia kichwakichwa kwenye siasa za upinzani bila kujua maana yake nini.
 
Back
Top Bottom