Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,146
- 48,386
- Thread starter
-
- #41
Soma uelewe mada. Siyo kila ukiona neno "fisadi" unawaza kwamba tunasema chadema ni ya mafisadi ama imekumbatia ufisadi.Kazi ya mahakama ya mafisadi nini? Usijitekenye ukacheka mwenyewe. "ZEZETA"
Soma uelewe mada. Siyo kila ukiona neno "fisadi" unawaza kwamba tunasema chadema ni ya mafisadi ama imekumbatia ufisadi.
Mkuu unachosema ni kweli, shida Tz siyo wabunifu hata kidogo.Lowasa na viongozi wa Chadema wanafanya ziara huko mikoani. Tulishauri Chadema kuanzisha vyombo vyao vya habari kwa ajili ya kueneza sera za chama na propaganda.Kuna Twitter,Facebook,Instagram na Youtube hizi ni platform za bure ambazo Chadema wameshindwa kuzitumia vizuri
Issue ya kukamatwa kwa Maxence Melo imeonyesha nguvu ya mitandao ya kijamii ,Chadema wangeweza kutumia nguvu hiyo kupiga kelele kuhusu kupotea kwa Ben Saanane lakini ni aibu uongozi wao umekaa kimya
ImefanyikaKwani operesheni kata funua wameitangazia wapi?
Huna uwezalo kama sii ujualo.Chadema kuitwa chama cha wachaga ni sawa kabisa.Kiliasisiwa na wachaga na ndio wanaokimiliki hata wagombea wao Tanzania nzima asilimia kubwa ni chagas.Hata wanaojaribu kuibomoa cuf nyuma ya Profesa ni chagas ili chadema itamalaki na hata wanaozishikilia rasilimali za CCM mikoani kwa mikataba ya kijanjajanja yenye lengo la kuua chama ukiwaangalia kwa umakini ndio haohao ili chama cha home kikamate fursa.So ukabila na ukanda ni ngumu sana kuvitenganisha na chadema.Hilo la udini siwezi kulisemea maana hata ccm kuna wabunge na DC ambao ni wachungaji.
Chadema ni kama Safina ya Nuhu.Baada ya kuingia jamii yote ya chadema safinani ndiposa "wakaingizwa"mbuzi kondoo na bata nk pamoja na watu wa aina yako.Huna uwezalo kama sii ujualo.
Ulitaka watokee wapi? Na kwanini?Kati ya Wakuu wa mikoa wallioteuliwa, tisa ni kutoka Usukumani.
Kupitia thread yako hiyo,nisamehe kwa yote niliyokutuhumu.Hakika leo nimetambua ww ni mtu unayeuelewa sana udhaifu wa chagadema.Karibu CCM tuijenge nchi yetu kwa Pamoja.Huko ulipo sasa ni kwa watu wa aina hiyo na walio na vigeugeu na wasio na msimamo ulio thabiti.Sasa utawezaje kuwapa nchi wakosaji hao?!Heko na asante kwa kulitambua hilo.Agenda bado ipo bali wao wenyewe mpaka sasa wameshindwa kuwaeleza wananchi jambo ambalo lipo wazi kuhusu Lowassa na ufisadi wa Richmond. Hawasemi ni "Ushahidi" gani waliokuwa nao hadi wakamwita Lowassa "fisadi" na ni ushahidi gani waliioupata baadaye uliohalalisha wao kukubali kumpitisha Lowassa kuwa mgombea Urais kwenye uchaguzi wa Mwaka 2015. Wako kimya tu.
Ninaposema CHADEMA, hapa namaanisha viongozi wenye dhamana ya kuzungumza kwa niaba ya wanachama wenzao, kwa maana nyingine wao ndiyo chama na wanaposema wao chama huwa kinakuwa kimesema. CHADEMA kila mara hujiweka kwenye kujihami badala ya kushambulia.
Kwa mfano mpaka sasa wapinzani wa CHADEMA wamefanikiwa kuwaaminsha watu kwamba CHADEMA ni chama kinachodhibitiwa na Wakristu na watu Kaskazini. Lakini wakati inashutumiwa hivyo, CCM inashutumiwa asilimia zaidi ya 60 Makatibu wa CCM walikuwa ni waislamu lakini CCM haikuitwa ni chama cha Waislamu!
Wakati huu ambapo CHADEMA inaitwa ya "kikanda" Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano ameteua watu wengi toka Kanda ya Ziwa na mikoa ya Jirani lakini CCM haiitwi ya Kikanda wala Magufuli hasemwi kuwa anateu watu wa "kwao" kama ambavyo inasemwa kwa Mbowe kuhusu CHADEMA na Uchaga.
Tatizo la CHADEMA ni kwamba wao huchukulia vitu vinavyoharibu chama kama ni vitu "vitu vidogo" kwa hivyo hawajishughulishi navyo. Leo mtu akiwa ni mchaga anataka kugombea nafasi ya uongozi wa chama huko mtwara anashindwa kugombea kwa kuwa itaonekana kwamba wachaga wanapandikiza watu wao kila sehemu ya nchi. Viongozi wanafanyaje kuondoa hizi propaganda kwamba bila kuwa mchaga au mtu wa kaskazini huwezi kuwa kiongozi ndani ya CHADEMA?
Wakati watu wa Kaskazini waliopo CCM wanaweza kuwa viongozi mahala popote ndani ya Tanzania, CHADEMA mtu ukiwa wa Kaskazini na ukiwa kiongozi nje ya mikoa ya kaskazini inajengwa picha na CCM kwamba CHADEMA ni ya watu wa Kaskazini na viongozi wa CHADEMA wanabaki wameduwaa hawana la kufanya! Ni lini CHADEMA itatoka na kuwaambia watu kwamba nchi hii mtu anaweza kuwa kiongozi wa chama cha siasa mahala popote bila ya kujali asili wala dini yake?
Ukiangalia suala la Ben Saanane, Mikutano ya hadhara, kufukuzwa Bungeni, CHADEMA siku zote huamini kwamba wananchi "wataelewa tu" kwamba CCM ni chama kibaya bila ya kufanya juhudi za kuonesha kwamba CCM ni chama kibaya na mabaya ya watanzania chanzo chake ni CCM!
Unataka kusema CHADEMA iumbe watu wapya? Tumia akili wewe usiwe hopeless material! Watanzania ni sisi hawahawa.Chadema ni dampo la ccm,
Wazee, mafisadi, wachawi,wazembe kazini kutoka ccm kimbilio lao ni Chadema!
Ukanda na ukabila dhidi ya Chadema ni single iliyochuja kaka, uko nchi gani wewe!! Hii walijaribu kuitumia sana 2010 lzm kilichowakuta ccm wanakijua wenyewe...... Propaganda za udini na ukabila zimebaki kuhubiriwa na wapumbavu wasiojielewawewe unajua kinachoongelewa ama unaleta ushabiki tu. Kimevukaje wakati mitaani wapo bize wajinga wanaoaminisha watu kwamba CHADEMA ni Kaskazini na wapo wanoamini?
Tumekuja mjomba , unasemaje ?Mhh ngoja waje wenyewe
Nipo Iringa. Hapa kwenye uchaguzi wa Mwaka jana hata watu ndani ya CHAADEMA wakati wa kura za maoni walikuwa wanahoji inawezekanaje Mmasai awe mgombea Ubunge jimbo la Isimani!! Mimi nipo field ndugu yangu.Ukanda na ukabila dhidi ya Chadema ni single iliyochuja kaka, uko nchi gani wewe!! Hii walijaribu kuitumia sana 2010 lzm kilichowakuta ccm wanakijua wenyewe...... Propaganda za udini na ukabila zimebaki kuhubiriwa na wapumbavu wasiojielewa