Cha usingizi

Jeho

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
5,069
Reaction score
5,556
Jamaa mmoja ambaye alikuwa ni cha usingizi sana, siku moja akiwa kanisani nyakati za usiku mchungaji akiwa anahubiri, jamaa kama kawaida akapata usingizi, lakini kutokana na muda huo kuwa usiku ilihitajika kuwe na umeme na siku hiyo umeme ulikuwepo tokea asubuhi kwa hiyo waumini hawakuwa na haja ya kuchukua tahadhari kwa kuandaa jenereta, ghafla mchungaji akiwa anaendelea kuhubiri umeme ukakata na mchungaji kulazimika kuhubiri gizani, kwa kuwa jamaa alikuwa amelala toka mwanzo wa mahubiri hata wakati umeme unakatika jamaa bado alikuwa usingizini. Jamaa alipoamka alikuta giza tupu na kwa kuwa hakujua kilichotokea alijua kuwa amekuwa kipofu, na alipojua kawa kipofu alipaza sauti akasema "mchungaji niombee nimepofuuuuuuuuka"
 
Kwa anayetumia umeme wa NGELEJA hawezi kustuka aamkapo na kukuta giza totoro, labda huyo si wa inji hii.
 
hilo nalo neno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…